Hivi sasa akili bandia inatumiwa katika kuwasimamia wafanyakazi kwenye maeneo ya ujenzi nchini China. Ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Sayansi ya China imesema, viwanda vya ujenzi vya China vinatumia teknolojia ya akili bandia kusimamia hali ya usalama wa wafanyakazi, pia inaweza kugundua kama wafanyakazi wanafanya kazi wanavuta sigara ama kutumia simu za mkononi.
Teknolojia hiyo vilevile inaweza kutoa tahadhari wakati ajali au hatari, kwa mfano wafanyakazi wanaposahau kofia zao za usalama, au kuingia kwenye maeneo yaliyowekwa vizuizi, na kuwafuatilia watu wanaoshughulikia mambo yasiyoruhusiwa. Teknolojia hiyo inaweza kumsimamia mfanyakazi yeyote wa eneo la ujenzi kwa utambuzi wa sura.
Mfanyabiashara wa Kampuni ya ujenzi wa nyumba ya mji wa Guangzhou ameeleza kuwa, teknolojia kama hiyo inachangia kusaidia kupunguza mzigo kwa wasimamizi wa usalama. Anasema, "Baadhi ya wafanyakazi wanafanya uvivu kwenye eneo la ujenzi, wengine wanatumia simu za mkononi wakati wa kuendesha mashine, watu pia wanaweza kufanya makosa lakini mashine hazifanyi makosa, ndiyo maana matumizi ya teknolojia ya akili bandia yanaweza kuepusha ajali nyingi."
China ina nguvu kazi nyingi kwenye sekta ya ujenzi duniani, mwanasayansi wa Canada Bw. Vaclav Smir amekadiria kuwa, ndani ya miaka mitatu ijayo, matumizi ya saruji ya China yatazidi yale ya Marekani kwa karne moja, na kwamba muda wa miradi mingi ya ujenzi utakuwa mfupi, na ajali zinatokea mara kwa mara.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |