• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanafunzi wa Marekani waanzisha "Corona Party" atakayekuwa wa kwanza kuambukizwa Corona atapata pesa

    (GMT+08:00) 2020-08-13 18:15:26


    Hivi karibuni, sehemu nyingi nchini Marekani ikiwemo majimbo ya Florida, Texas, California yanakabiliwa na maambukizi makubwa ya virusi vya Corona, na idadi ya watu waliothibitishwa kuwa na virusi vya Corona imezidi laki 3.2 na kushika nafasi ya kwanza nchini humo.

    Wakati huohuo, habari kutoka shirika la habari la Marekani ABC zimesema wanafunzi wa mji wa Tuscaloosa wa jimbo la Alabama walianzisha "Corona Party", ambapo mtu atakeyeshinda kwa kuwa wa kwanza kuambukizwa virusi vya Corona atapata pesa. Diwani wa mji huo Bi. Sonya McKinstry aliliripoti jambo hilo kwa bunge la mji, na bunge la mji likapitia amri ya kuwalazimisha watu kuvaa barakoa katika maeneo ya umma.

    Hii si mara ya kwanza kwa tukio kama hilo kutokea nchini Marekani. Tarehe 24 Machi, gavana wa Jimbo la Kentucky Bw. Andy Beshear alipotangaza hali ya maambukizi ya virusi vya Corona alisema, vijana kadhaa wenye umri wa miaka 20 walithibitishwa kuwa na virusi vya Corona baada ya kushiriki kwenye "Corona Party". Na Gazeti la Washington post pia limeripoti kuwa, "Corona Party" inayowashirikisha watu 400 ambayo inalenga kuambukiza virusi inafanyika kwenye jimbo hilo, na kuzusha hofu kwa wenyeji wa huko.

    Ofisa mwandamizi wa Hospitali moja iliyoko mjini San Antonio, ameeleza kuwa mgonjwa mwenye umri wa miaka 30, alifikiri kuwa maambukizi ya virusi vya Corona ni "udanganyifu", na kushiriki kwenye "Corona Party" kwa makusudi, ili kuthibitisha kama maambukizi hayo ni ya kweli au la. Baada ya hapo aliambukizwa virusi hivyo na kufariki.

    Naibu waziri wa afya na huduma za umma ya Marekani anaona chanzo muhimu cha kusambaa kwa kasi kwa virusi vya Corona kwenye sehemu ya kusini na magharibi nchini Marekani ni kutovaa barakoa au kutoweka umbali kati ya watu na watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako