• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanamke aomba msaada wa Polisi baada ya kujuta kuuza mtoto wake

    (GMT+08:00) 2020-09-02 20:32:34


    Hivi karibuni Idara ya polisi ya Wilaya ya Wuyi ya Mji wa Jinhua ilipokea simu kutoka kwa mwanamke mmoja, ambaye alitaja mambo kuhusu mauzo ya mtoto, hali ambayo iliwafanya polisi wawe na tahadhali.

    Mwanamke huyo alibeba ujauzito bila kupangwa. Kwa kuwa ana watoto wawili, hali ya kiuchumi ya familia yake si nzuri, na hakuwa na uwezo wa kulea mtoto mwingine, ndiyo maana aliwaambia wengine kuwa ataomba watu wengine kumlea mtoto wake baada kumzaa. Mwanamke mwingine Bibi Zeng alipata habari hiyo, na kuwa kuwa yeye ana mwana mmoja mwenye umri wa miaka 40 ambaye bado hajaoa, alitaka huyo mtoto wake amchukue mtoto wa Bibi Luo kuwa wake na kumlea.

    Mwanzoni mwa Mwezi Juni, Bibi Zeng alipata njia ya kuwasiliana na Bibi luo, na Bibi Zeng alikubali kumpa Bibi Luo fedha za awali, na kumpa fedha zinazobaki baada ya mtoto kuzaliwa. Katikati ya mwezi Juni walikutana na kujadiliana mambo kuhusu bei ya mauzo ya mtoto. Mwishoni mwa mwezi Juni, Bibi Luo alijifungua mtoto wa kike na kuchukuliwa na Bibi Zeng kama ilivyopangwa. Lakini baada ya hapo Bibi Luo alijuta kwa kumwuza mtoto wake.

    Mwanzoni mwa mwezi Julai Bibi Luo aliiba mtoto kwa kisingizio cha kumchukua mtoto kwenye kumpima damu. Baada ya pande hizo mbili kufanya majadiliano, mama ya Bibi Luo alimwahidi Bibi Zeng kurudisha fedha walizopewa, lakini Bibi Zeng alikuwa na wasiwasi kudanganywa, na kumzia mama wa Bibi Luo aondoke, ndiyo maana Bibi Luo aliomba msaada wa polisi. Lakini hawakujua kuwa walikuwa wamekiuka sheria. Hivi sasa pande hizo mbili zinashikiliwa kwa tuhuma za uhalifu wa biashara ya mtoto.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako