|
Wakati teknolojia mpya zinapoleta urahisi mbalimbali kwa maisha ya watu, pia zinawatatiza wazee wengi. Hasa katika maambukizi ya virusi vya Corona, mambo mengi yanatakiwa kufanywa kupitia mtandao wa Internet, hivyo wazee wengi wanaoishi maisha ya mtindo wa jadi wameathiriwa kutokana na kutofahamu namna ya kutumia simu za kisasa.
Kwa mujibu wa ripoti ya takwimu za maendeleo ya mtandao wa Internet wa China, hadi mwezi wa Machi mwaka huu, idadi ya watumiaji wa mtandao wa Internet wa China imefikia milioni 904, na kiwango cha uenezi wa mtandao wa Internet kimefikia asilimia 64.5, lakini kiwango cha watumiaji wenye umri wa miaka 60 na zaidi ni asilimia 6.7 tu. Kutokana na takwimu kutoka idara ya takwimu za taifa, hadi mwishoni mwa mwaka jana, kiwango cha wazee wenye umri wa miaka 60 na zaidi katika watu wote kilikuwa asilimia 18.1 hivi. Takwimu hizo zimeonesha kuwa wazee zaidi ya milioni 100 nchini China wamekosa fursa ya kutumia teknolojia mpya. Mbali na hayo, wazee wengi zaidi vijijini hawafahamu namna ya kutumia teknolojia hizo.
Wadau wa sekta ya tekolojia mpya wamesema, uwezo wa kusikia, kuona na kukumbuka wa wazee umedhoofika, na hivi sasa simu za mkononi zinatilia maanani katika vijana ambazo hazijafikiria sifa za watumiaji wazee katika ubunifu.
Kwa wazee wasio na tatizo la kiafya na wenye mahitaji ya kujifunza, njia ya kutatua tatizo hilo ni kwamba jamaa wa wazee wanawafundisha namna ya kutumia teknolojia hizo. Lakini njia hiyo inawataka wakufunzi kuwa na wakati na uvumilivu huku wazee wakiwa na hamu kubwa ya kujifunza.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |