Mfumo wa kisiasa
Mfumo wa nchi
Jamhuri ya Watu wa China ni nchi ya ujamaa ya utawala wa kidemokrasi ya umma chini ya uongozi wa tabaka la wafanyakazi na kwenye msingi wa shirikisho la wafanyakazi na wakulima. Mfumo wa ujamaa ni mfumo wa kimsingi wa Jamhuri ya watu wa China.
Katiba
Katiba ni sheria kuu ya kimsingi ya taifa, ambayo huamua mfumo wa jamii wa nchi na kanuni za kimsingi za mfumo wa nchi, kanuni za kimsingi za jumuia na shughuli za idara za serikali, haki za kimsingi na majukumu ya raia, katiba pia inaamua bendera ya taifa, wimbo wa taifa, nembo ya taifa na mji mkuu pamoja na taratibu muhimu nyingine ambazo zinahusiana na pande zote za maisha ya nchi. Katiba ina madaraka makubwa ya sheria ambayo ni msingi wa sheria nyingi, sheria zote na kanuni zote haziruhusiwi kwenda kinyume na katiba.
"Mwongozo wa pamoja wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la umma la China" uliotangazwa kabla ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya watu wa China, si kama tu ni mwongozo wa muungano wa demokrasia ya umma wa China, bali pia unaonesha umuhimu wa katiba ya muda. "Mwongozo wa pamoja" ulipitishwa kwenye mkutano wa kwanza wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la umma la China, ambao ulitangazwa tarehe 29 Septemba mwaka 1949. Kabla ya kutangazwa kwa "Katiba ya Jamhuri ya watu wa China", mwongozo huo ulifanya kazi ya katiba ya muda.
Baada ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya watu wa China tarehe 1 Oktoba, 1949, katiba nne za Jamhuri ya watu wa China zilitungwa na kutangazwa mwaka 1954, mwaka 1975, mwaka 1978 na mwaka 1982.
Katiba ya 4 ya China yaani katiba ya sasa ilitangazwa tarehe 4 Desemba, 1982 kwenye Mkutano wa 5 wa Bunge la 5 la umma la China. Katiba hiyo ilirithi na kuendeleza kanuni za kimsingi za katiba iliyotangazwa mwaka 1954, kujumuisha maarifa ya China ya maendeleo ya ujamaa na kuigiza maarifa ya kimataifa, ambayo ni sheria kuu ya kimsingi yenye umaalum wa kichina inayolingana na mahitaji ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya ujamaa. Katiba hiyo imeweka bayana mifumo ya kisiasa na kiuchumi ya Jamhuri ya watu wa China, haki na majukumu ya raia, kuanzishwa kwa wizara za nchi na kazi za wizara hizo na majukumu ya kimsingi ya nchi ya siku zijazo. Umaalum wake wa kimsingi ni kuweka mfumo wa kimsingi na majukumu ya kimsingi ya China, kuthibitisha kanuni nne za kimsingi na sera ya kimsingi ya mageuzi na ufunguaji mlango. Katiba hiyo inaeleza kuwa, wananchi wa makabila mbalimbali na jumuiya zote za taifa zima yapaswa kuchukua katiba kuwa kanuni za kimsingi za shughuli zao, na jumuiya yoyote au mtu yeyote haruhusiwi kuwa na haki maalum zinazokiuka katiba na sheria.
Katiba hiyo inagawanyika kuwa sehemu tano za mwongozo wa jumla, haki za kimsingi na majukumu ya raia, wizara za nchi, bendera ya taifa, nembo ya taifa, na mji mkuu wa China, katiba hiyo ina milango minne na vifungu 138 kwa jumla. Tangu kutangazwa kwake, China ilifanya marekebisho manne kuhusu katiba hiyo ili kuikamilisha siku hadi siku.
Mfumo wa Bunge la umma la China
Mfumo wa Bunge la umma la China ni mfumo wa siasa wa kimsingi, ambao ni aina ya jumuiya ya utawala wa kidemokrasia wa umma wa China, pia ni mfumo wa siasa wa China. Bunge la umma la China ni tofauti na mabunge ya nchi za magharibi chini ya "nguzo tatu za utawala", bunge la umma la China limethibitishwa kwenye katiba ya China kuwa chombo chenye madaraka ya juu kabisa cha taifa. Kila raia mwenye umri wa zaidi ya miaka 18 ana haki ya kuchagua mjumbe wa bunge la umma au kuchaguliwa kuwa mjumbe wa bunge la umma. Nchini China, katika bunge la umma kwenye ngazi tofauti, wajumbe wa bunge la umma la ngazi ya tarafa na wilaya huchaguliwa moja kwa moja. Wajumbe wa ngazi juu ya tarafa na wilaya wanachaguliwa kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Bunge la umma la China linaundwa na wajumbe wanaochaguliwa kutoka mikoa, mikoa inayojiendesha, miji inayotawaliwa moja kwa moja na serikali kuu na jeshi. Muda wa kila awamu ya Bunge la umma la China kwenye ngazi mbalimbali ni miaka mitano, na kila bunge la China hukutana mara moja
Kwenye mkutano wa mwaka wa Bunge la umma la China, wajumbe wa bunge la umma wanasikiliza ripoti ya kazi ya serikali na ripoti nyingine muhimu kadhaa, wanatakiwa kuthibitisha ripoti hizo na kutoa maazimio husika. Katika kipindi cha kufungwa kwa mkutano wa bunge la umma, Halmashauri ya kudumu ya bunge la umma la ngazi mbalimbali inaendesha madaraka inayokabidhiwa kutoka kwa bunge la umma. Kwa mfano, madaraka ya Halmashauri ya kudumu ya Bunge la umma la China ni pamoja na kufafanua katiba, kusimamia utekelezaji wa katiba, kutunga na kurekebisha sheria zilizoko nje ya sheria zilizotungwa na bunge la umma, kuwajibika kwa bunge la umma la taifa na kutoa ripoti za kazi.
Madaraka ya kimsingi ya Bunge la umma la China ni pamoja na kutunga sheria, kufanya usimamizi, kutoa maamuzi kuhusu mambo makubwa na kuwateua viongozi au kuwaondoa viongozi madarakani. Nchini China, kutunga mipango ya maendeleo ya uchumi na jamii ya taifa wa kipindi cha miaka kadhaa kumekuwa sera muhimu ya kusukuma mbele maendeleo ya jamii ya China, lakini mipango hiyo inapaswa kuidhinishwa na bunge la umma la China ndipo itakapoweza kuonesha umuhimu wake wa kisheria. Sheria ya China inaeleza kuwa, viongozi wakuu wa China kama vile rais wa nchi, spika wa bunge la umma na wengineo wanapaswa kuchaguliwa na bunge la umma la China. Waziri mkuu wa serikali na mawaziri mbalimbali pia wanapaswa kuteuliwa na Bunge la umma la taifa. Bunge la umma la China pia linaweza kupitisha utaratibu kutoa mapendekezo ya kuwaondoa madarakani spika wa bunge la umma, rais wa nchi au waziri mkuu waliochaguliwa au kuthibitishwa nalo.
Utaratibu wa ushirikiano wa vyama vingi na mashauriano ya kisiasa
Utaratibu wa ushirikiano wa vyama vingi na mashauriano ya kisiasa chini ya uongozi wa Chama cha kikomunisti cha China ni utaratibu wa kisiasa wa kimsingi wa China.
China ni nchi yenye vyama vingi. Mbali na Chama cha kikomunisti cha China kinachotawala, pia kuna vyama vinane vya kidemokrasia. Vyama hivyo vya kidemokrasia vilikuwepo kabla ya kuzaliwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Kisiasa, vyama hivyo vinaunga mkono uongozi wa chama cha kikomunisti, hili ni chaguo lao la kihistoria katika mchakato wa kufanya ushirikiano wa muda mrefu na juhudi za pamoja na chama cha kikomunisti. Chama cha kikomunisti cha China na vyama mbalimbali vya kidemokrasia vinapaswa kufuata kanuni za katiba katika shughuli zao za kimsingi. Vyama mbalimbali vya kidemokrasia vyote vinajitawala katika jumuiya zao, ambavyo vina uhuru wa kisiasa, kijumuiya na hadhi sawa ya kisheria kutokana na katiba ya nchi. Sera ya kimsingi ya ushirikiano kati ya Chama cha kikomunisti cha China na vyama mbalimbali vya kidemokrasia ni "Kuwepo pamoja kwa muda mrefu, kusimamiana, kutendeana kwa udhati, kufaidika na mafanikio na kukabiliana na taabu kwa pamoja".
Vyama mbalimbali vya kidemokrasia vya China sivyo vyama visivyotawala wala vyama vya upinzani, bali ni vyama vinavyoshiriki mambo ya siasa. Vyama hivyo vinaweza kushiriki mashauirano kuhusu utoaji wa sera kuu za taifa na uchaguzi wa viongozi wa nchi, kushiriki usimamizi wa mambo ya taifa na kushiriki katika utekelezaji wa siasa, sera, sheria na kanuni za taifa.
Wakati serikali kuu inapochukua hatua kubwa au kuamua masuala muhimu kuhusu mambo ya nchi au maisha ya wananchi, Chama cha kikomunisti cha China hufanya mashauriano, kusikiliza maoni na mapendekezo na vyama vya kidemokrasia au watu wa kidemokrasia wasio na vyama, baadaye kutoa sera; wajumbe wa vyama vya kidemokrasia na watu wasio na vyama wanaweza kuchaguliwa kuwa wajumbe katika Bunge la umma la China, na kamati mbalimbali za kudumu, ili kushiriki vizuri zaidi katika mambo ya siasa na kufanya kazi ya usimamizi; vinaweza kufanya kazi muhimu katika Baraza la mashauriano ya kisiasa na kushika nyadhifa mbalimbali katika serikali za ngazi mbalimbali na idara za utekelezaji wa sheria.
Njia muhimu za ushirikiano wa vyama vingi na mashauriano ya kisiasa ni kama zifuatazo: Kwanza, Baraza la mashauriano ya kisiasa la umma. Baraza hilo ni baraza muhimu la kushiriki mambo ya siasa na utoaji wa sera za taifa kwa vyama mbalimbali, makundi mbalimbali ya umma na wajumbe wa sekta mbaimbali; Pili, makongamano na mikutano inayoendeshwa na Kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China na kamati za chama za ngazi mbalimbali. Kwenye makongamano na mikutano hiyo, Chama cha kikomunisti cha China husikiliza maoni na mapendekezo ya vyama mbalimbali na watu wasio na vyama kuhusu hali muhimu nchini, sera muhimu ya taifa, orodha ya wateule wa viongozi wa taifa na serikali za mitaa, orodha ya wateule wa wajumbe wa Bunge la umma na Baraza la mashauriano ya kisiasa; Tatu, wajumbe wa vyama mbalimbali vya kidemokrasia kwenye Bunge la umma la taifa wanaweza kushiriki kwenye mambo ya siasa na kufanya kazi ya usimamizi katika bunge la umma la China kwenye ngazi mbalimbali; Nne, kuwateua wajumbe wa vyama vya kidemokrasia kushika nyadhifa katika Baraza la serikali na wizara mbalimbali au serikali za mitaa na idara husika; Tano, kuwateua wajumbe wa vyama vya kidemrokasia kushika nyadhifa katika idara za uendeshaji wa mashitaka na mahakama mbalimbali.
|