Ustawishaji wa Vituo vya Viwanda vya Zamani
Kituo cha viwanda cha zamani cha sehemu ya kaskazini mashariki ya China kilikuwa muhimu sana kwa uchumi wa taifa na maendeleo ya jamii. Mwanzoni mwa kipindi cha uchumi wa mpango, uzalishaji wa mitambo na sekta ya uzalishaji wa chuma na chuma cha pua, ilitoa mchango mkubwa kwa ujenzi wa uchumi wa China. Lakini, kwa kuwa kituo cha viwanda vya sehemu ya kaskazini mashariki kiliundwa miaka mingi iliyopita, hivi sasa baadhi ya sekta za uzalishaji mali zimeingia katika kipindi cha kuzorota. Nguvu zake za ushindani zimepungua, lakini sekta mpya za kuzibadilisha bado hazijaimarika, hususan baadhi ya miji yenye rasilimali inakabiliwa na matatizo mengi. Kuhusu matatizo hayo, serikali ya China imeamua kuharakisha marekebisho, mageuzi na ustawishaji wa kituo cha viwanda cha zamani cha sehemu ya kaskazini mashariki.
Kwa kukariri maneno ya waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao, ustawishaji wa kituo cha zamani cha viwanda cha sehemu ya kaskazini mashariki, utarekebisha muundo wa uchumi, ambao ni pamoja na kurekebisha muundo wa sekta ya uzaliishaji mali, muundo wa utaratibu wa umilikaji wa vyombo vya uzalishaji mali na muundo wa uchumi wa taifa. Hii ni miongozo muhimu katika kustawisha kituo cha viwanda cha zamani. Kuhimiza mageuzi ya kiteknolojia katika viwanda ni shughuli muhimu. Kuleta maendeleo ya pande zote yenye uwiano na endelevu ni sera za muda mrefu; Kukamilisha ujenzi wa mfumo wa ajira na dhamana ya jamii ni dhana kwa ustawishaji wa kituo hicho cha zamani; na Kuharakisha maendeleo ya sayansi, teknolojia na elimu ni matakwa muhimu ya ustawishaji wa viwanda vya zamani vya sehemu ya kaskazini mashariki ya China.
Hivi sasa, serikali ya China inaandaa sera ya mpango wa marekebisho ya kituo cha viwanda cha zamani cha sehemu hiyo, mikoa mitatu ya sehemu ya kaskazini mashariki nayo inafanya utafiti ili kubuni mpango wa marekebisho na mageuzi wa sehemu hiyo.
|