3: Uchumi wa China

Mkakati wa Maendeleo

Mwezi Oktoba mwaka 1987, mkutano mkuu wa 13 wa chama cha kikomunisti cha China ulitoa mkakati wa "hatua tatu" wa ujenzi wa mambo ya kisasa ya China, kama ifuatavyo:

Hatua ya kwanza, toka mwaka 1981 hadi mwaka 1990, ambapo jumla ya thamani ya uzalishaji mali nchini ilitakiwa kuongezeka maradufu na kuondoa tatizo la njaa nchini. Hatua ya pili ni kuanzia mwaka 1991 hadi mwishoni mwa karne ya 20, jumla ya thamani ya uzalishaji mali ilitakiwa kuongezeka mara dufu tena, na maisha ya wananchi yafikie kiwango cha maisha bora. Hatua ya tatu, hadi kufikia katikati ya karne ya 21, wastani wa thamani ya uzalishaji mali nchini kwa mtu, ifikie kiwango cha nchi za wastani za viwanda, ambapo watu wataishi maisha mazuri na kutimiza mambo ya kisasa. Mwezi Septemba mwaka 1997, mkutano mkuu wa 15 wa chama cha kikomunisti cha China ulikamilisha zaidi hatua ya tatu ya lengo, ambayo katika miaka kumi ya kwanza ya karne ya 21, jumla ya thamani ya uzalishaji mali nchini itaongezeka maradufu kuliko ile ya mwaka 2000, wananchi wataishi maisha mazuri zaidi na kuwa na utaratibu bora wa uchumi wa masoko wa ujamaa; Kujitahidi kwa miaka kumi mingine kufanya uchumi wa taifa kuwa na maendeleo makubwa zaidi na kuwa na utaratibu bora wa aina mbalimbali; na ifikapo mwaka 2050, China itatimiza mambo ya kisasa, na kuwa nchi ya ujamaa yenye nguvu, demokrasia na ustaarabu.


1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12