Biashara ya Nje
Kutumia Mitaji ya Nje
China inatumia mitaji ya nchi za nje kwa njia za aina mbalimbali, ambazo kwa jumla zinaweza kugawanyika katika mafungu matatu. Fungu la kwanza ni kupata mikopo ya nchi za nje, ikiwa ni pamoja na kukopeshwa na serikali za nchi za nje, mashirika ya fedha duniani, benki za biashara za nchi za nje na kutoa hati zenye thamani za dhamana ya serikali kwa nchi za nje. Fungu la pili, kuwekezwa moja kwa moja na wafanyabiashara wa kigeni, vikiwemo viwanda vya ubia, vya ushirikiano na vya wafanyabiashara wa kigeni; Fungu la tatu ni uwekezaji wa aina nyingine wa wafanyabiashara wa kigeni, ambao ni pamoja na ukodishaji, biashara yenye ruzuku, kazi za usindikaji na uuzaji wa hisa.
Kutoka mwaka 1990 hadi mwaka 2001, China ilitumia mitaji ya nchi za nje dola za kimarekani bilioni 510.8, ambayo ile iliyowekezwa moja kwa moja na wafanyabiashara wa kigeni ilikuwa dola za kimarekani bilioni 378. Mitaji ya kigeni iliyotumiwa na China mwaka 2002, ilikuwa dola za kimarekani bilioni 55, ambayo ile iliyowekezwa moja kwa moja na wafanyabiashara wa kigeni ilikuwa dola za kimarekani 52.7, China ilichukua nafasi ya kwanza katika kutumia mitaji ya nchi za nje. Mwaka 2003, uwekezaji wa wafanyabiashara wa kigeni nchini China ulidumisha ongezeko kubwa, ambapo kampuni 41,081 za wafanyabiashara wa kigeni ziliidhinishwa kuanzishwa nchini China, kiasi hiki kilikuwa ni ongezeko la 20.2% kuliko mwaka uliopita; Thamani ya mikataba ya biashara iliyosainiwa ilikuwa dola za kimarekani bilioni 115.1, ambazo ni ongezeko la 39.0%; Mitaji iliyotukika hasa ilikuwa dola za kimarekani bilioni 53.5, ikiwa ni ongezeko la 1.4%.
Kampuni Muhimu za Kimataifa Zilizoko Nchini China
Kampuni ya magari ya Volkswagen ya Ujerumani katika miaka karibu 20 iliyopita, ilianzisha viwanda viwili vya ubia vya magari katika miji ya Shanghai na Changchun, na baadhi ya viwanda vinavyozalisha vipuri vya magari, pamoja na mfumo wa vituo zaidi ya 100 vya vipuri vya magari.
Kiwanda cha Volkswagen cha Shanghai, ambacho kiliwekezwa Yuan za Renminbi zaidi ya bilioni 18.9, hivi sasa kinazalisha magari madogo namna miongo kadhaa ya aina tano ambazo ni Santana, Santana 2000, Passat, Polo na Golf. Kiwanda cha magari cha Changchun, ambacho kiliwekezwa dola za kimarekani zaidi ya Yuan bilioni 11.1, kinazalisha magari ya nembo za aina mbili za Audi na Volkswagen na aina ya tano ya Audi A6. A4, Bora, Jetta na Golf. Volkswagen imekuwa kampuni kubwa kabisa ya magari nchini China na kuwa na wateja wengi kutokana na mabadiliko ya aina za magari na huduma bora.
Hivi leo, China imekuwa soko la pili kwa ukubwa la Kampuni ya Volkswagen duniani. Katika muda wa miaka mitano ijayo, kampuni hiyo itawekeza Euro zaidi ya bilioni 5 nchini China.
BOEING
Kampuni ya Boeing imekuwa na uhusiano mzuri wa Ushirikiano na China toka mwaka 1972. Kampuni ya Boeing inatoa mafunzo nchini China kuhusu uendeshaji na utunzaji wa ndege pamoja na usimamizi ili kutoa dhamana kwa shughuli za usafirishaji wa ndege. Kampuni ya Boeing imeanzisha mfumo wa huduma za uwakilishaji uwanjani, mahitaji na teknolojia nchini China, na kusaidia Shirika la Ndege la China kuinua kiwango cha usimamizi wa mawasiliano na usalama wa anga.
Aidha, Kampuni ya Boeing imekuwa na ushirikiano mkubwa katika uzalishaji na sekta ya uzalishaji wa ndege nchini, na kujenga viwanda vipya vya ubia vya vifaa, marekebisho, utunzaji na ukarabati wa ndege, pamoja na kuanzisha shughuli za uuzaji wa vipuli vya ndege.
Vipuri muhimu vya ndege za Boeing 33,000 vinazotumika hivi sasa, vilizalishwa nchini China.
NOKIA
Kampuni ya Nokia ilianzisha uhusiano wa kibiashara na China tangu miaka ya 50 ya karne iliyopita. Mwaka 1985, kampuni ya Nokia ilianzisha ofisi yake mjini Beijing. Tokea katikati ya miaka ya 90 ya karne iliyopita, kampuni hiyo ilijenga viwanda vya ubia hapa China, na kuviendeleza kuwa vituo vyake muhimu vya uzalishaji duniani. Baada ya kuingia karne mpya, Kampuni ya Nokia ilishiriki zaidi katika maendeleo ya sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano (IT) ya China kwa kufanya ushirikiano na sekta mpya ya teknolojia ya upashanaji wa habari, na kujitahidi kuiendeleza China kuwa kituo chake cha kuandaa wataalamu wa Kampuni ya Nokia.
Nchini China, Kampuni ya Nokia imejenga vituo viwili vya utafiti vya kilimwengu, kuanzisha ofisi zake katika sehemu mbalimbali na kuwa na wafanyakazi zaidi ya 4,500. Bidhaa zote muhimu za kampuni hiyo sasa zinazalishwa hapa China, zikiwa ni pamoja na simu mpya za mikononi, vituo vya upashanaji wa habari, mitambo ya udhibiti ya vituo, kituo cha kubadilishana mawimbi, zana za kupokea mawimbi, zana za ubadilishanaji wa tarakimu na simu zenye uwezo wa aina nyingi.
MICROSOFT
Kampuni ya Microsoft iliingia China mwaka 1992, na ilitenga fedha nyingi kuanzisha vitengo vyake vya utafiti vya ngazi ya kimataifa, vikiwa ni pamoja na kituo cha utafiti cha Microsoft nchini China, taasisi ya utafiti ya Microsoft katika Asia na kituo cha teknolojia cha Microsoft duniani, na kuifanya kampuni ya Microsoft nchini China kuwa tawi lake lenye uwezo mkubwa duniani.
Hadi hivi sasa, Kampuni ya Microsoft imejenga viwanda viwili vya ubia nchini China. Kampuni hiyo ikiwekeza Yuan za Renminbi milioni 19, ilianzisha Kampuni ya Software ya Zhongguancun kwa ubia na Kampuni ya Sitong, na kuanzisha Kampuni ya Softwere ya Weichuang ya Shanghai kwa kufanya ubia na Kampuni ya Uwekezaji ya Lianhe ya Shanghai. Aidha, Kampuni ya Microsoft imeingia ubia pamoja na Chuo Kikuu cha Mawasiliano cha Shanghai, Kampuni ya Uwekezaji ya Lianhe ya Shanghai na Kampuni ya Soft Weare ya Pudong, Shanghai, kuanzisha Chuo cha Softwere cha Chuo Kikuu cha Mawasiliano cha Shanghai na Kampuni ya huduma ya sayansi na teknolojia ya Chuo Kikuu cha Mawasiliano cha Shanghai. Kampuni ya Microsoft kwa jumla iliwekeza Yuan za Renminbi milioni 4, zikichukua 10% ya mitaji yote iliyowekezwa.
Mbali na hayo, Kampuni ya Microsoft imehamisha uzalishaji wa X-box, ambazo ni bidhaa zinazopendwa na watu wengi, hapa China. Pia imeweka uzalishaji wa mouse huko Guangdong, ambao thamani ya uzalishaji imezidi dola za kimarekani milioni 100 kwa mwaka.
|