Ala za Muziki kwa Kukwaruza Nyuzi
Kinanda Rewapu
Kinanda cha Rewapu ni ala ya muziki yenye nyuizi na inatoa sauti kwa kukwaruzwa. Kinanda hicho kimekuwepo kwa miaka zaidi ya 600 na kinawavutia sana watu wa kabila la Uygur, Tajik na Uzbek mkoani Xinjiang.
Kinanda hicho kinatengenezwa kwa mbao, sehemu ya chini ni boksi la kukuza sauti lenye umbo la nusu mviringo.
Kuna kinanda cha aina yenye nyuzi tatu, tano, sita hadi tisa.
Kinanda hicho kinapigwa kwa mkono wa kulia na mkono wa kushoto unadhibiti sauti kwa vidole.
Kuna aina nyingine za kindanda cha kwa tofauti za nyuzi na maumbo, na sauti pia zinatofautiana ingawa si sana
Kinanda cha Liuqin
Liuqin inafanana na Pipa , inatengenezwa kwa mbao, ni kinanda kinachotutumiwa sana na watu wa mikoa ya Shandong, Anhui na Jiangsu, na kinatumika zaidi katika opera ya kienyeji.
Kinanda hicho kinatoa sauti kwa kukwaruzwa na vidole, mpiga anakiweka kifuani na kushika kinanda kwa mkono wa kushoto na kupiga kwa mkono wa kulia.
Mwishoni mwa 1958 mafundi wa kiwanda cha kutengenezea kinanda hicho waliongeza nyuzi za kinanda hicho kutoka mbili hadi tatu, sauti zikawa zimeongezeka. Katika miaka ya 70 kinanda hicho kimeongezwa nyuzi na kufikia nne. Kinanda hicho kimekuwa na historia ya miaka 200 nchini China. Hivi leo kinanda hicho kimekuwa ala muhimu katika vikundi vya muziki wa Kichina, sauti yake ni kama Mandolin, na kikichanganywa na ala za muziki za Kimagharibi muziki unapata utamu mahsusi.
Kinanda Guqin
Kinanda hicho kimekuwa na miaka zaidi ya 3000 nchini China.
Sauti ya kinanda Guqin ni nene na nyororo. Watu wa kale walikuwa wanaoga na kuvaa nguo safi kabla ya kupiga kinanda hicho, walikaa na kuweka kinanda hicho mapajani, walipiga kwa mkono wa kushoto na kudhibiti sauti kwa mkono wa kulia.
Katika China ya kale wapigaji wa kinanda hicho wengi walikuwa ni wasomi, walitoa mchango mkubwa katika ufundi wa kupiga kinanda hicho.
Utengenezaji wa kinanda hicho ni kazi ya sanaa kubwa. Kutokana na kuwa kinanda hicho kinatengenezwa kwa mikono tu, ufundi uliachwa kurithisha. Katika miaka ya karibuni ufundi huo ulipatikana na kubadilishwa kidogo, sauti ya kinanda hicho imekuwa nyororo zaidi.
Kinanda cha Jiayeqin
Kinanda hicho kinapigwa zaidi na watu wa kabila la Wakorea lililoko katika sehemu ya kaskazini mashariki ya China. Kinanda hicho kilivumbuliwa mwaka 500 na watu wa kabila la Wakorea.
Kinada hicho kimekuwa na miaka 1500. katika zama za kale kinanda hicho kilitengenezwa kwa mbao nzima kwa kuchongwa, lakini sauti yake ilikuwa ndogo, baadaye watu wa kabila la Wakorea walibadilisha kidogo na kukifanya kinanda hicho kiwe na sauti kubwa, na kinatengenezwa kwa mbao tofauti katika sehemu tofauti.
Sasa kinanda hicho kimekuwa na nyuzi 21, na boksi la kukuza sauti limekuwa kubwa zaidi, na sauti imekuwa kubwa zaidi.
Kinanda Jiayeqin kinaweza kuonesha hisia mbalimbali za furaha, hasira na huzuni. Zamani waliokuwa wapiga kinanda hicho walikuwa wanaume, lakini sasa wengi wamekuwa wanawake.
Wapiga kinanda hicho huwa wengi kwa pamoja, wanapiga huku wanaimba.
mnasikiliza: mshujaa Aliran
Kinanda Huobusi
Kinanda Huobusi ni ala ya muziki inayopigwa sana na watu wa kabila la Wamongolia.
Umbo la kinanda hicho ni kama kijiko kikubwa, urefu wake ni sentimita 90, mpini wa kinanda hicho umenyooka, boksi lake la kukuza sauti linawambwa kwa ngozi ya chatu.
Katika Enzi ya Ming kinanda hicho kilikuwa hutumika katika karamu ya wafalme, na katika Enzi ya Qing kilikuwa ni ala muhimu katika muziki uliopigwa katika kasri la kifalme.
Kutokana na sababu fulani baada ya Enzi ya Qing, kinanda hicho kilitoweka, na kilirudi baada ya Jamhuri ya Watu wa China kuasisiwa. Baada ya kufanyiwa mageuzi, sauti yake imekuwa kubwa na eneo la sauti limekuwa kubwa zaidi.
Kinanda Dongbula
Kinanda Dongbula kimeenea sana miongoni mwa watu wa kabila la Kazak mkoani Xinjiang, karibu kila mmoja anaweza kupiga muziki fulani.
Kinanda hicho kina historia ndefu kutokea karne ya tatu.
Kinanda hicho kinatengenezwa kwa mbao, umbo lake ni kama kijiko kikubwa ambacho kinachongwa kwa mbao moja. Nyuzi zake mbili ni mishipa ya mbuzi.
Mpiga kinanda hicho anashika kinanda kwa mkono wa kushoto na kukwaruza nyuzi kwa mkono wa kulia.
Kinanda Ruan
Kinanda hicho kilianza kutengenezwa katika karne ya tatu, Enzi ya Qin. Boksi lake la kukuza sauti ni la duara kama ngoma ndogo.
Katika karne ya tatu alikuwepo mwanamuziki mmoja aliyevumbua ala hiyo. Kutokana na kuwa jina la mwanamuziki huyo aliitwa Ruan, watu waliipatia ala hiyo jina la Ruan.
Kinanda hicho kina sehemu tatu yaani kichwa cha kinanda, fimbo ya kinanda na boksi la kukuza sauti, kwenye kichwa vinachomekwa vijiti vinne kwa pande mbili, kila kijiti kinafungwa uzi mmoja, jumla kuna nyuzi nne.
Katika miaka ya karibuni kinanda hicho kilifanyiwa mageuzi, na sauti zake zimekuwa nyingi.
Sauti ya kinanda hicho ni nyororo, na katika bendi hutumia vinanda hivyo viwili.
Kinanda kikubwa Ruan kinafanana na fidla kubwa na sauti yake ni nene.
Kinanda Konghou
Kinanda Konghou kimekuwepo kwa miaka zaidi ya elfu mbili. Katika Enzi ya Tang (618-907), kutokana na ustawi wa uchumi, ala hiyo pia ilienea sana na hata ilijulishwa nchini Japan na Korea. Lakini katika karne ya 14 ala hiyo ilikuwa haitumiki sana na hatimaye ilitoweka, na ilionekana tu kwenye picha.
Kwa kufanya utafiti, wanamuziki wa China walifanikiwa kutengeneza ala hiyo katika miaka ya 80 ya karne iliyopita.
Kinanda hicho kina nyuzi 36 ziko juu ya boksi la kukuza sauti.
Eneo la sauti ya kinanda hicho ni kubwa, mpigaji anapiga kinanda hicho kwa mikono miwili. Mnasikiliza:Mwanzi wa Hunan
|