23: Ala za Muziki

Ala za Muziki kwa Kupiga Nyuzi

Yangqin

Yangqin ni ala inayotumika sana katika muziki wa Kichina, inaweza kupiga muziki peke yake, inaweza kutumiwa pamoja na ala nyingine na inatumika katika muziki wa opera.

Kwa mujibu wa kitabu cha Rekodi ya Historia, ala hiyo ilikuja kutoka nchi za kale za Kiarabu, hadi Enzi ya Ming (1368-1644) ala hiyo ilianza kutokea katika Mkoa wa Guangdong na baada ya kufanyiwa mageuzi imekuwa Yangqin ya leo.

Yangqin inatengenezwa kwa mbao, ina umbo la kipepeo, boksi lake la kukuza sauti ndio bodi lake lililotiwa nyuzi, na linapigwa kwa vijiti viwili vinavyogonga nyuzi.

Yangqin inafaa kupiga muziki wenye uchangamfu.

Yangqin imekuwepo kwa miaka zaidi ya miaka 400, katika muda huo wanamuziki walifanya mageuzi mara nyingi kwa ajili ya kuongeza eneo lake la sauti, kukuza sauti na kuzifanya sauti ziwe za kukolea masikio.

Kutokana na kuboreshwa katika muda mrefu Yangqin imekuwa ala inayopendwa sana na Wachina kwa ajili ya kupiga muziki wa Kichina.


1 2 3 4 5 6 7