23: Ala za Muziki

Ala za Muziki kwa Upinde

Banhu

Banhu ni kinanda kinachotoa sauti kwa upinde kama fidla, sauti yake inafaa kuonesha hisia za msisimko na hisia za upendo.

Banhu imekuwa na miaka 300, boksi lake la kukuza sauti ni la mbao nyembamba.

Kinanda hicho kinatumika zaidi katika sehemu ya kaskazini ya China, na hakiwezi kukosekana katika opera za kienyeji.

Sauti ya Banhu inajitokeza sana katika bendi, kwa hiyo inafaa kuongoza muziki wa ala nyingi.

Kinanda Chenye Sanamu ya Kichwa cha Farasi

Kinanda hicho kilitoke katika karne ya 13 miongoni mwa watu wa kabila la Wamongolia.

Nyuzi za kinanda hicho ni manyoya kumi kadhaa ya mkia wa farasi na kinatoa sauti kwa upinde uliofungwa kwa manyoya ya mkia wa farasi, na kinanda hicho kina sanamu ya kichwa cha farasi.

Hapo mwanzo sauti ya kinanda hicho ilikuwa ndogo, lakini baadaye wanamuziki walifanya mageuzi na kukifanya kinanda hicho kiwe na sauti kubwa.

Kinanda hicho kina aina ukubwa wa mbili, na kila aina ina sauti tofauti na maeneo tofauti ya sauti.

Kinanda Leiqin

Leiqin ni kinanda kilichotokea katika miaka ya 20 ya karne ya 20.

Kinanda hicho kilibuniwa na mwanamuziki Wang Diayu. Wang Dianyu alikuwa mkazi wa Mkoa wa Shandong, familia yake ilikuwa maskini na alikuwa mlemavu wa macho. Mwishoni mwa miaka ya 20 ya karne ya 20 alibuni kinanda hicho na katika mwaka 1953 kinanda hicho kilipewa jina la Lieqin .

Leiqin ni kama kinanda Erhu , ina nyuzi mbili za chuma cha pua, kinanda hicho kikubwa kina urefu wa sentimita 110 na kidogo kina urefu wa sentimita 90.

Mpigaji wa kinanda hicho anatumia mkono wa kushoto kurekebisha sauti na kuvuta upinde kwa mkono wa kushoto.

Leiqin ina eneo kubwa la sauti na sauti yake pia ni kubwa, inaweza kuchezwa peke yake na pia kushirikiana na bendi na inaweza kuiga sauti ya binadamu.

Kinanda Niutuiqin

Niutuiqin ni ala ya muziki iliyoenea katika mikoa ya Guizhou na Guanxi miongoni mwa kabila la Wadong. Nyuzi zake mbili zinatengenezwa kwa usumba na upinde pia unatengenezwa kwa kifungu cha nyuzi za usumba.

Sauti ya Niutuiqin ni tofauti na sauti ya vinanda vingine, kwamba sauti yake ni ya kukauka kidogo, lakini sauti hiyo inafaa kushirikiana na sauti za waimbaji, kwani sauti hiyo inafanana na sauti ya binadamu.

Kinanda hicho kiliwahi kufanyiwa mageuzi mara nyingi, kinanda cha siku hizi kinatoa sauti kubwa.

Watu wa kabila la Wadong hutumia kinanda hicho kuwasaidia waimbaji ili kuleta utamu zaidi.

Kinanda Gaohu

Gaohu ni kinanda kinachofanana na Erhu , lakini kinatumika zaidi katika muziki wa Kiguangdong.

Muziki wa Kiguangdong ni muziki ulioenea sana mkoani Guangdong. Katika miaka ya 20 ya karne ya 20 mwanamuziki Lu Wencheng na kukifanya kinanda hicho kiwe ala muhimu katika muziki wa Ki-guandong.

Kinanda cha Gaohu kinafanana na Erhu ila tu boksi lake ni jembamba na refu kidogo, kwa kufanya hivyo sauti imekuwa nyembamba na kubwa.

Sauti ya kinanda hicho ni kama sauti ya juu ya waimbaji wanawake. Kinanda hicho ni muhimu katika muziki wa Kichina.

Kinanda Erhu

Kinanda Erhu ni ala muhimu ya muziki wa Kichina, kilianza kutokea katika karne ya saba hadi kumi Enzi ya Tang. Katika miaka zaidi ya elfu moja iliyopita, kinanda hicho kilikuwa kinatumika katika muziki wa opera.

Kinanda Erhu kina urefu wa sentimita 80, na kina nyuzi mbili, na kwenye sehemu ya chini kuna boksi la kukuza sauti kama kikombe, kinatoa sauti kwa upinde. Mpigaji anakaa na kuvuta upinde, baadhi ya watu wanakiita kinanda hicho kuwa ni "fidla ya Kichina".

Baada ya Jamhuri ya Watu wa China kuasisiwa mwaka 1949, kinanda hicho kiliwahi kufanyiwa mageuzi mara nyingi. Hiki ni kinanda ambacho kinaweza kuchezwa peke yake, lakini kinatumika zaidi kwa kushirikiana na ala nyingine katika muziki wa Kichina.

Erhu ni ala ya muziki iliyoenea sana miongoni mwa Wachina kutokana na sauti yake tamu.


1 2 3 4 5 6 7