• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chemsha bongo kuhusu "Vivutio vya Sichuan"

    (GMT+08:00) 2008-11-18 15:40:23
    Wasikilizaji wapendwa, Raido China Kimataifa na Idara ya utalii ya Mkoa wa Sichuan,China zimeandaa Chemsha bongo kuhusu "Vivutio vya Sichuan". Mashindano hayo ya chemsha bongo yatamalizika tarehe 15 Aprili mwaka 2009.

    Kama ilivyokuwa kwenye mashindano ya miaka iliyopita, kamati yetu ya uthibitishaji itachagua wasikilizaji washindi wa nafasi ya kwanza, pili na tatu pamoja na nafasi maalum. Wasikilizaji washindi watakaopata nafasi maalum wataalikwa kuja China na kutembelea mkoani Sichuan nchini China.

    Kwenye chemsha bongo hii kuna maswali 14, tafadhali uchagua jibu sahihi kwa mujibu wa makala 7 tutakayowekwa kwenye tovuti yetu. Aidha unaweza kutoa maoni yako kuhusu picha uliyopata kuhusu Mkoa wa Sichuan.

    Baada ya kutoa majibu juu ya maswali, tafadhali uandike anuani yako, e-mail yako na jina lako ili tuweze kukuarifu kwa wakati

    Makala husika

    1. Kutembelea sehemu za peponi

    2. Sanxingdui yenye vitu vingi vya ajabu

    3. Utamaduni wa dini ya Kibuddha katika Mlima E Mei na Mlima Leshan

    4. Hifadhi ya Wolong mkoani Sichuan?maskani ya Panda wakubwa

    5. Yibin, Mji wa kwanza kwenye eneo la mtiririko wa mto Changjiang

    6. Ustadi mkubwa wa opera ya Sichuan

    7. Vyakula maarufu vya Sichuan

    Maswali na Majibu

    Maswali:

    1, Bonde la Jiuzhaigou lilipata jina hilo kutokana na kuwepo kwa vijiji 9 vya watu wa kabila la watibet ndani ya sehemu hiyo au la? A. ndio B. hapana

    2. Je, Bonde la Jiuzhaigou na Sehemu ya vivutio ya Huanglong zote zimeorodheshwa kuwa mali ya urithi wa mazingira ya asili duniani ? A. ndio B. hapana

    3. Sanxingdui ilistawi kwa miaka mingapi? A. miaka 2000 B. miaka 1000

    4. Miongoni mwa vitu vingi vilivyofukuliwa kwenye mabaki ya Sanxingdui, ni vitu vya aina gani, ambavyo vinaweza kuonesha kiwango cha ufundi wa wakati ule, je, ni vitu vya jade au ni vya shaba nyeusi? A. vyombo vya gade B. Vyombo vya shaba nyeusi

    5. Je Mlima E Mei ni moja kati ya sehemu takatifu za dini ya kibuddha nchini China?

    A. ndio B. hapana

    6. Sanamu ya Buddha mkuu ya Leshan ni sanamu kubwa kabisa duniani, je, urefu wake ni mita ngapi? A. zaidi ya mita 70 B. zaidi ya mita 60

    7. Je, Maskani ya Panda wakubwa nchini China yako Mkoani Sichuan?

    A. ndiyo B. hapana

    8. Katika eneo la hifadhi ya maumbile ya Wolong, kuna Panda wakubwa wangapi?

    A. zaidi ya 100 B. zaidi ya 90

    9. Sinema ipi iliyopata tuzo ya Academy Awards, ambayo filamu yake ilipigwa kwenye msitu wa mianzi wa Shunan?

    A. "Corouching Tiger, Hidden Dragon" B. "Kuzingirwa na maadui pande zote

    10. Je, Mji mdogo wa kale wa Lizhuang uko kwenye kando ya Mto Changjiang?

    A. ndiyo B. hapana

    11. Ustadi mkubwa kabisa wa opera ya Sichuan ni nini?

    A. badilisha vinyago usoni B. puliza moto kutoka mdomoni

    12. Katika mji wa Chengdu watu wanaweza kuona maonesho ya opera ya Sichuan kila siku?

    A. Wanaweza B. Hawawezi

    13. Wenyeji wa Sichuan wanapenda chakula gani? A. pilipili kali B. chachu na pilipili

    14. Vidonge vitatu vya michele inayonata sana yakiongezwa maji ya sukari guru, chakula hiki kinaitwa nini katika mkoa wa Sichuan? A. Sandapao B. Vidonge vya Lai

    Nyongeza:

    Maoni yako au pili uliyopata kuhusu Mkoa wa Sichuan

    Jina lako anuani yako

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako