• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Kampuni inawaajiri wanafunzi wa vyuo vikuu kufuga kondoo 2018-02-11

  Hivi karibuni, kampuni moja ya kufuga kondoo kwa njia ya kisasa ya China imejulikana kutokana na kutoa mshahara wa Yuan laki 4.8, sawa na dola za kimarekani elfu 75 kwa mwaka, kuwaajiri wahitimu wa vyuo vikuu vya Tsinghua na Peking, ambavyo ni bora zaidi nchini China, kufanya kazi ya kufuga kondoo. Mshahara huo unawavutia sana wahitimu wa vyuo vikuu wa siku hizi wanaokabiliwa na shinikizo kubwa la kutafuta ajira.

  • Mahakama yaamuru mtoto alipe mamake malipo ya malezi 2018-02-02

  Mahakama ya juu zaidi kisiwani Taiwan, nchini China imeamuru kuwa mwanamume mmoja amlipe mamake zaidi ya dola za kimarekani elfu 750 kugharamia malezi na masomo ya kuwa daktari wa meno. Habari zimewahi kuripoti kuhusu wazazi kuwashtaki watoto wao ili kupata usaidizi wa kifedha lakini kesi hii ni tofauti kwa sababu inahusisha mkataba wa maandishi uliofikiwa kati ya mzazi na mwanawe

  • Utalii umekuwa motisha muhimu kwa ongezeko la uchumi duniani
   2018-01-17

  China hivi leo imetoa waraka kuhusu maendeleo ya utalii ya mwaka 2016-2017 nchini China na dunia nzima. Waraka huo wenye kauli mbiu ya "mageuzi na uvumbuzi wa sekta ya utalii ya China katika zama mpya", umetoa makadirio kuhusu maendeleo ya utalii katika mwaka 2017-2018 nchini China na dunia nzima, na kuchambua masuala nyeti ya maendeleo ya utalii.
  • Kutoka nyumbani bila ya pochi ni zoea jipya la wachina 2018-01-10

  Takwimu zimeonyesha kuwa kutokana na miamala mingi kufanyika kwa njia ya simu za mkononi, mtindo wa kimaisha wa wachina umebadilika kinyemela, na kutoka nyumbani bila a kubeba wallet kumekuwa ni mazoea mapya kwa wachina, na pia ni mtindo mpya duniani. Mwezi Machi maka jana miamala iliyofanyika kwa njia ya simu za mkononi ilichukua asilimia 82 ya malipo yote katika mtandao wa ulipaji wa Zhifubao yaani AliPay, na kuweka rekodi mpya. Sababu moja ya kuongezeka kwa ulipaji wa kutumia simu za mkononi, ni kutumika kwa wingi kwa code ya kulipa. Mamilioni ya maduka katika mitaa mbalimbali nchini China yametimiza maendeleo ya kidigitali katika mchakato wa kupokea pesa kwa kutegemea karatasi yenye code hii ya kulipia. Hivi sasa, haijalishi kama ni kulipia chakula kwenye mgahawa, au kufanya manunuzi madukani, na hata unaponunua matunda na mboga kando ya barabarani, unaweza kutumia simu za mkononi ku-scan code.

  • Je, kwa nini "darasa la maadili ya wanawake" limezusha hasira kote nchini China? 2018-01-10

  Katika miaka ya hivi karibuni, shule za kuwafundisha maadili wanawake kufuata zimeibuka katika sehemu mbalimbali nchini China, na zinasisitiza kuwa hadhi ya wanawake na kazi havipaswi kuwa pamoja, na kuwalazimisha wanafunzi wa kike kujifunza kazi za nyumbani. Shule moja inayoitwa "shule ya elimu na utamaduni wa jadi ya Fushun" iliyopo kaskazini mashariki mwa China imezusha malalamiko makubwa kutokana na kuwafundisha wanawake "maadili ya kike". Shule hiyo inasema wanawake wanapaswa kuwa tabaka la chini, hawapaswi kujibu wanapopigwa au kukerwa, hawapaswi kutaliki au kutalikiwa, kwani huko ni kwenda kinyume na maadili ya wanawake, kuagiza chakula na kutosafisha vyombo ni kinyume na maadili ya wanawake. Kutokana na kuongezeka kwa malalamiko katika jamii na mitandao ya kijamii, serikali ya mji huo imeagiza shule hiyo ambayo imekuwepo kwa miaka sita ifingwe.

  • Wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari wa China wanatumia saa 2.28 kila siku kufanya kazi za nyumbani 2018-01-02

  Unajua kwa nini wanafunzi wa China wanafanya vizuri katika mitihani? Ripoti inaonesha kuwa kila siku wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari wa China wanatumia karibu saa tatu kufanya kazi za nyumbani, muda ambao ni mara tatu ya kiwango cha wastani cha dunia. Unaonaje kuhusu habari hii, na unaona muda wanaotumia kufanya kazi za nyumbani unaweza kufanikisha masomo yao na kupata kazi nzuri baada ya kuhitimu?

  More>>
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako