• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kinshasa-Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ateua mnadhimu mpya wa jeshi

    (GMT+08:00) 2008-11-19 09:26:25

    Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo jioni ya tarehe 17 alitangaza kumteua Bw. Didier Etumba kuwa mnadhimu mpya wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

    Bw. Kabila alimwondoa madarakani mnadhimu wa zamani wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jenerali Dieudonne Kayembe, Bw. Etumba alipandishwa cheo kutoka Brigadia Jenerali mpaka Luteni Jenerali.

    Wachambuzi wa wanaona kuwa, katika wiki kadhaa zilizopita jeshi la serikali ya nchi hiyo lilikuwa katika hali ngumu ya mapigano na jeshi la upinzani la Nkunda mkoani Kivu Kaskazini ambayo iko sehemu ya mashariki ya nchi hiyo, mji wa Goma ambao ni mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini unatishiwa vibaya na jeshi la Nkunda, na baadhi ya askari wa jeshi la serikali waliwapora wakazi wa sehemu hiyo kwa pamoja, hiyo Bw. Kabila aliamua kubadilisha mnadhimu wa jeshi ili kurekebisha jeshi la nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako