Mkutano wa 16 usio rasmi wa wakuu wa jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi wa nchi za Asia na Pasifiki APEC ulifunguliwa tarehe 22 huko Lima, mji mkuu wa Peru. Rais Hu Jintao wa China alihudhuria mkutano huo na kutoa hotuba muhimu.
Rais Hu alisema ongezeko la uchumi duniani linakabiliwa na changamoto kubwa ya msukosuko wa fedha, nchi mbalimbali zinapaswa kuchukua hatua za haraka ili kuzuia kuenea kwa msukosuko huo, kutuliza soko la fedha na kuhimiza maendeleo ya uchumi, China inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kudumisha utulivu wa soko la fedha duniani, na pia inapenda kushirikiana na nchi wanachama wa APEC katika kuimarisha kubadilishana uzoefu na ujenzi wa uwezo katika mambo ya fedha.
Kuhusu masuala yanayokabili maendeleo ya uchumi na jamii duniani, rais Hu alitoa mapendekezo matano, yaani kuhimiza utaratibu wa biashara za pande mbalimbali uendelezwe vizuri, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa pamoja, kupambana na maafa ya kimaumbile kwa ushirikiano, kuelekeza makampuni kuongeza wajibu wa kijamii, na kuhakikisha usalama wa chakula na nishati.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |