Rais Hu aliwasili Lima tarehe 19 mwezi huu na kufanya ziara nchini Peru. Wakati wa ziara yake hiyo, viongozi wa China na Peru wamefikia makubaliano kuhusu kuendeleza ushirikiano kwenye sekta mbalimbali, na kutangaza kuwa mazungumzo kuhusu mkataba wa biashara huria ya nchi hizo mbili yamekamilika kwa mafanikio, na nchi hizo mbili zimeanzisha rasmi uhusiano wa kiwenzi na kimkakati.
Rais Hu pia alihudhuria mkutano wa 16 usio rasmi wa wakuu wa APEC huko Lima, ambapo amefafanua msimamo wa serikali ya China kuhusu masuala ya kukabiliana na msukosuko wa fedha duniani, kusukuma mbele usalama wa nafaka na nishati, na kuunga mkono mazungumzo ya Doha.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |