• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Madaktari wa China waliotoa misaada ya matibabu barani Afrika

    (GMT+08:00) 2008-12-10 10:52:45

    Huu ni mwaka wa 45 tangu China itume kwa mara ya kwanza kikundi cha madaktari katika nchi za Afrika mwaka 1963, mpaka sasa madaktari zaidi ya elfu 20 wa China wametoa misaada ya matibabu barani Afrika na kazi zao zimesifiwa na kuheshimiwa na serikali na watu wa nchi za Afrika. Hivi karibuni kikundi cha 27 cha madaktari kilichoundwa na kutumwa na mkoa wa Heilongjiang nchini Mauritania kimerudi nchini China baada ya kumaliza majukumu yao ya miaka miwili.

    Bw. Li Weian ni kiongozi wa kikundi hicho cha madaktari, alituelezea hali ya kazi na maisha yao barani Afrika akiwa na tabasamu usoni, akisema:

    "Katika majira ya ukame, kiyoyozi kinaweza kupunguza halijoto ndani ya chumba kufikia nyuzi 35 hivi, halijoto ya kawaida barani Afrika wakati wa mchana ni nyuzi 45 hadi 50. Katika siku zenye joto kali kabisa, hata kipimo joto kiliharibika na huenda ilifikia nyuzi 70 hivi."

    Joto la barani Afrika ni tatizo lakini pia ni changamoto kwa madaktari wa China. Bw. Li Weian alisema, ikilinganishwa na hali ya hewa yenye joto na ukavu nchini Mauritania, majira ya joto ya maskani yake ni kama peponi. Bw. Li Weian alisema:

    "kutokana na watu kutoka jasho jingi katika kipindi cha jua kali, limejengwa bafu moja kwenye kambi yetu. Lakini baada ya maji kupelekwa kwenye chombo cha chuma nje ya chumba hicho, baada ya muda mfupi tu, maji huwa ya mto sana hata hayawezi kutumiwa kuoga."

    Ingawa hali mbaya ya hewa ni ya namna hii, lakini maisha ya miaka miwili yamewafanya wazoee hali ya huko, bado wanakumbuka vizuri hali waliyokumbana nayo walipofika nchini humo kwa mara ya kwanza. Mwezi Julai mwaka 2006 baada ya kusafiri kwa ndege kwa zaidi ya saa 10, madaktari wa China walilifika huko Nouakchott, mji mkuu wa Mauritania, baadaye walipanda gari na kusafiri kwa kilomita 700 jangwani, wakafika mji wa Selibaby.

    Hospitali ya mji wa Selibaby ambayo madaktari hao walifanya kazi huko ilijengwa kwa msaada wa China, na inatoa huduma za matibabu kwa wakazi laki moja wa sehemu hiyo. Wakati huo kwa upande wa Mauritania mkuu wa hospitali hiyo peke yake ni daktari, wauguzi wachache wa hospitali hiyo waliweza kufanya kazi za kawaida tu. Kazi nyingine zote zilifanywa na madaktari wa China, hawakuwa na mpango halisi wa muda wa kazi na walikuwa wanatoa huduma saa 24 kwa siku. Daktari Bi. Zhang Lixin alisema:

    "katika kambi yetu tulifuga mbwa kadhaa, wakati wa usiku tuliposikia wakilia, tunajua walikuja kuwa wagonjwa wanaohitaji matibabu ya dharura. Hatukuweza kuwasiliana na wagonjwa moja kwa moja, kwa kuwa Mauritania ina makabila manne, wagonjwa wanaongea lugha za kikabila, wauguzi wanafahamu kifaransa pamoja na lugha za kikabila, kwa hiyo wauguzi waliwasiliana kwanza na wagonjwa kwa lugha zao, halafu walitafsiri kwa kifaransa, tulifahamu kifaransa kiasi lakini pamoja na vitendo vya mikono na uzoefu, tukaweza kujua hali ya wagonjwa."

    Kwa upande wa maisha, hali ya mawasiliano mjini Selibaby ni mbaya na bidhaa chache tu zinapatikana sokoni. Kikundi cha matibabu chenye madaktari 7 kiligawanywa kuwa timu tatu, kila mwezi timu moja kati yao ilikwenda Nouakchott ambapo ni umbali wa kilimita 700 na kurudi na chakula na vitu vya mahitaji vinavyomudu mwezi mmoja, kwa kawaida ni mchele, unga wa mchele, mafuta ya kupikia na mayai. Lakini katika majira ya masika barabara hukatika, hivyo walikuwa wanaenda mjini kila baada ya miezi kadhaa. Katika hali hiyo, madaktari walifikiria kupanda mbaga wenyewe kwa kutumia mbegu walizoleta kutoka nyumbani China. wakashughulikia shamba kwa makini na kufurahia kila mmea ukichipuka, ukichanua maua na kuzaa matunda.

    Ingawa watu wa kikundi hicho wote ni madaktari, lakini nao pia hawakuzuilika kuugua. Mauritania ni nchi yenye idadi kubwa ya wagonjwa wa Malaria duniani, na mji wa Selibaby ni sehemu inayoathiriwa vibaya na ugonjwa huo nchini humo. Katika muda wa miaka miwili, madaktari wote waliwahi kuugua Malaria. Bw. Li Weian alisema:

    "mbu ni tatizo la mwaka mzima. Mbu wa huko wanaweza kuambukiza malaria, inzi pia wako kila mahali siku zote hata wanatua usoni mwa watu. Watu wa kikundi chetu wote waliwahi kuugua malaria."

    Maumivu hayo ya mwilini ni madogo tu yakilinganishwa na uchungu wa kukumbuka nyumbani wakiwa mbali namna hii. Bw. Li Weian alisema:

    "mwanzoni njia nilizotumia kuwasiliana na ndugu zangu ni simu moja, kompyuta moja, na barua ambayo ilikuwa inachukua miezi mitatu kufika nyumbani kwangu. Simu ni chombo cha ofisini, hivyo sote hatukuitumia kufanya mambo binafsi. Isipokuwa kompyuta iliyoweza kuunganishwa na mtandao wa Internet ilikuwa ni njia pekee, tulinunua kadi maalum na kupigia simu nyumbani kwenye mtandao wa Internet ingawa kwa njia hii hatukusikilizana vizuri."

    Katika muda wa miaka miwili, madaktari watatu wa kikundi hicho walifanya kazi kwa uhodari na walimaliza kwa pamoja upasuaji zaidi ya 800. Udhati na ustadi wao umeheshimiwa na kuaminiwa na wakazi wa Selibaby.

    Kutokana na kazi zao za uhodari, madaktari hao walikabidhiwa nishani ya heshima na waziri mkuu wa Mauritania ambayo iliidhinishwa moja kwa moja na rais wa nchi hiyo. Hii ni heshima ya juu zaidi nchini Mauritania, pia ni mara ya kwanza kwa kikundi cha madaktari cha mkoa wa Heilongjiang nchini humo kupewa heshima hiyo katika miaka 40 iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako