• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpango wa miaka 20 wa China "tutunze maini yetu katika maisha yote"

    (GMT+08:00) 2008-12-10 11:07:06

    Mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu idara husika za China zilianzisha mpango uitwao "Tunza ini lako katika maisha yote" kwa ajili ya wagonjwa wenye matatizo ya ini. Mpango huo utakaotekelezwa kwa miaka 20 utawapatia wagonjwa wenye matatizo ya ini nchini China taarifa mpya kuhusu kinga na matibabu ya magonjwa ya ini, misaada ya matibabu na hata kutoa matibabu bila malipo.

    Mpango huo ulianzishwa kwa pamoja na shirikisho la mfuko wa kinga na tiba ya homa ya manjano la China na tovuti ya kutunza ini ya China, na unalenga kuelekeza wagonjwa wenye matatizo ya ini na jamii nzima kujenga mtizamo na ufahamu sahihi kuhusu kinga na tiba ya magonjwa hayo, na kuwawekea mazingira bora ya maisha na kazi katika miaka 20 ijayo. Mwanachama wa taaluma za matibabu na dawa katika taasisi ya uhandisi ya China ambaye pia ni katibu wa taasisi ya magonjwa ya ini ya kanda ya Asia na Pasifiki Profesa Zhuang Hui alisema:

    "kwa mujibu wa uchunguzi mmoja uliofanyika mwaka 2002, kila mgonjwa mwenye matatizo ya ini, ikiwemo saratani ya ini, kwa wastani anatoa gharama za matibabu yuan 30,477 kila mwaka. Utafiti umeonesha kuwa, wagonjwa wa homa ya manjano ya aina ya B wakipewa matibabu mwafaka huenda watapata nafuu na hata kupona ugonjwa huo, na kupunguza uwezakano wa kubadilika kuwa saratani ya ini. Lakini takwimu husika pia zimeonsha kuwa, asilimia 19 tu ya wagonjwa wa matatizo ya ini nchini China ndio waliopewa matibabu ya kuangamiza virusi."

    Gharama kubwa za matibabu, wagonjwa kukosa matibabu mwafaka na ufahamu sahihi kuhusu kinga na tiba ya magonjwa ya ini, pamoja na tofauti za kiwango cha matibabu kwenye sehemu mbalimbali zimekuwa masuala dhahiri yanayozikabili kazi za kinga na tiba ya magonjwa ya ini nchini China. lakini kwa upande wa vifaa vya upimaji, dawa na wataalamu hodari wa matibabu, kiwango cha jumla cha matibabu ya magonjwa ya ini nchini China kinalingana na kile cha kimataifa. Kutokana na hali hiyo, mpango huo wa kutunza ini unalenga kuwapatia matibabu mwafaka wagonjwa wengi zaidi wenye matatizo ya ini, na kueneza zaidi ufahamu kuhusu magonjwa hayo katika jamii. Ofisa wa shirikisho la mfuko wa kinga na tiba ya homa ya manjano ya China Bi. Wang Zhao alisema:

    "kuanzishwa kwa mpango huo kunalenga kutatua hali ya watu wa China ya kukosa ujuzi kuhusu kinga na matibabu ya matatizo ya ini, na wagonjwa wa matatizo ya ini kutokuwa na mtizamo sahihi kuhusu matibabu, pia kunalenga kukidhi mahitaji makubwa ya matibabu mwafaka ya magonjwa hayo. Aidha mpango huo pia unajitahidi kueneza mtizamo wa kisayansi wa kinga na matibabu ya magonjwa hayo, ili kufanya jamii itilie maanani magonjwa ya ini, kuhamasisha na kuelekeza wagonjwa wapewe matibabu mwafaka na kuhakikisha utekekezaji wa hatua mbalimbali za kinga na matibabu."

    Ofisa CEO wa tovuti ya kutunza ini ya China Bw. Yang Yong alieleza kuwa, mpango huo una sehemu tatu yaani kutoa misaada kwa wagonjwa, huduma za utoaji taarifa na kuanzisha utaratibu wa mawasiliano. Mpango huo utatoa fursa kwa wagonjwa na umma wanaofuatilia na kushiriki kwenye mpango huo kufahamu na kujifunza ujuzi kuhusu magonjwa ya ini, na pia utatoa huduma mbalimbali kwa wagonjwa hatua kwa hatua. Mbali na hayo, tovuti hiyo pia itatoa nafasi za mawasiliano bila malipo kati ya madaktari na wagonjwa. Kuhusu utoaji misaada kwa wagonjwa, Bw. Yang Yong alisema:

    "kwa mujibu wa mpango huo, kutokana na magonjwa tofauti ya ini na hali tofauti za mapato ya familia, katika miaka 20 ijayo, kila mwezi tutachagua wagonjwa wasiozidi 500 na kutoa misaada ya yuan 100 hadi 300, na madaktari wa magonjwa ya ini watatoa maelekezo ya kimatibabu na ya kisaikolojia kwa wagonjwa hao. Kwa wale ambao hali zao za magonjwa ni mbaya na familia zao zina matatizo ya kiuchumi, kila mwaka pande tatu za hospitali za ushirikiano, shirikisho la mfuko na tovuti yetu tutachagua wagonjwa wenye hali hiyo na kuwalipia gharama zote za matibabu."

    Tarehe 1 Oktoba mwaka huu ambayo ni sikukuu ya 59 ya taifa ya China, kundi la kwanza la wagonjwa lililopewa misaada kutokana na mpango huo lilichaguliwa rasmi, wagonjwa 20 kutoka mikoa na miji 17 nchini China walipewa misaada. Bw. Wei Deshan kutoka mkoa wa Liaoning ni mmoja kati ya wagonjwa hao 20, alithibitishwa kwamba ana saratani ya ini, Bw. Wei Deshan alisema misaada iliyotolewa na mpango huo imemletea matumaini. Alisema:

    "magonjwa ya ini ni makubwa, matibabu yake pia yanahitaji gharama kubwa. Nadhani mpango huo ni mzuri, kwa kuwa nimepata misaada kutoka kwa watu wema, si kama tu ni misaada ya fedha, nafurahi sana kupewa misaada. Naona jamii ina watu wengi wema. Nimeona matumaini na kujisikia upendo wa jamii."

    Inakaridiwa kuwa katika miaka 20 ijayo, watu zaidi ya laki moja watanufaika kutokana na mpango huo. Bw. Yang Yong pia alisema, hospitali za ushirikiano wa mpango huo zitafikia mia moja na ziko kwenye sehemu mbalimbali za China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako