• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Moses mwenye uwezo wa kuimba vizuri nyimbo za Kichina

    (GMT+08:00) 2008-12-12 15:09:46

    Emanuel Moses Onasaa ni mkazi wa Dar es Salaam, na wazazi wake walitoka mkoa wa Kilimanjaro. Miaka mitatu iliyopita, Moses alikuja nchini China, sasa anachukua kozi ya uchumi wa kiamtaifa na biashara katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Beijing.

    Moses anapenda sana kujua lugha, anapenda kusoma lugha za aina tofauti. Sasa anajua kuongea vizuri kwa lugha ya Kichina.

    Kabla ya kuja China, Moses amejua machache tu juu ya China kwa kupitia filamu za kungfu kama watu wengine walivyo. Lakini baba yake aliwahi kusoma Beijing na Shanghai nchini China, hivyo Moses anajua hali ya China zaidi kuliko wengine.

    Katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Beijing, wanatumia lugha ya kichina darasani, ambapo waliamu wanawafundisha kwa Kichina, wanafunzi wanasoma na kufanya mtihani kwa Kichina, mpaka sasa Moses amezoea sana kutumia Kichina katika masomo yake.

    Moses anapenda kuimba nyimbo za Kichina, katika kipindi chetu, Moses aliimba wimbo wa Kichina "hadithi ya watoto". Moses alijulisha kuwa, huu ni wimbo mmoja ambao unajulikana sana nchini China, mwaka jana na mwaka juzi, ulikuwa wimbo maarufu sana, unaimbwa na kijana mmoja kutoka Taiwan. Wimbo huu umeeleza hivi, mtu mmoja aliyeachana na mpenzi wake alimwomba amwambie afanye nini ili kusahihisha kosa lake.


    1 2 3 4
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako