• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyakula maarufu vya Sichuan

    (GMT+08:00) 2008-12-15 14:38:46

    Sichuan inachukuliwa na Wachina wengi kuwa ni sehemu yenye vyakula vingi vitamu, vitoweo vya Sichuan ni moja kati ya makundi manne maarufu ya vitoweo nchini China, vinapendwa na watu wengi wa nchini na wa nchi za nje kutokana na mapishi yake maalumu. Vitoweo vya Sichuan vinapikwa kwa vitu vingi, huvyo vina ladha za aina nyingi, laini Wenyeji wa Sichuan wanapenda vitoweo vyenye ladha za Huajiao(unga wa mbegu za Chinese prickly ash) na pilipili hoho zinazowasha sana, hata kufikia hali ambayo, watu wakitaja vitoweo vya Sichuan, wanakumbuka mara moja radhi za Huajiao, pilipili na tamu pamoja na harufu ya kunukia vizuri. Basi, mbona wenyeji wa Sichuan wanapenda vitoweo vya ladha za Huajiao na pilipili? Profesa wa chuo kikuu cha Sichuan ambaye ni mtaalamu wa mambo ya mila na desturi za makabila, Bw. Mao Jianhua alisema, hii inahusiana na umaalumu wa historia na jografia wa mkoa wa Sichuan.

    "Sichuan iko kwenye bonde, hewa ya huko huwa ni yenye unyevunyevu mwingi, hivyo, ni rahisi kwa watu kuugua ugonjwa wa baridi yabisi. Huajiao na pili pili kali zinafanya kazi ya kuondoa baridi na kuchangamsha damu mwilini, hivyo wenyeji wanaoishi katika mazingira hayo ya kijiografia na hali ya hewa ya namna hii, wanapenda kula vitoweo vyenye radhi hizo. Watu wanaopenda ladha hizo siyo watu wa kabila la Wahan peke yao, hata watu wa makabila mengine madogo ya Waqiang na Wayi wanaoishi huko pia wanapenda sana kula vitoweo vya aina hiyo."

    Kutokana na takwimu zisizokamilika, vitoweo vya Sichuan viko zaidi ya aina 4,000, vitoweo vile maarufu zaidi ni pamoja na nyama ya kuku iliyokatwa kuwa vipande vidogo sana vikipikwa pamoja na karanga na mboga(diced chicken with peanuts), nyama ya bata yenye ladha ya chai(Smoked Tea Duck Sichuan Style), nyama ya nguruwe iitwayo Huiguorou, na nyama ya nguruwe yenye ladha ya samaki(Fish-flavored pork), vitoweo hivyo maarufu vinapikwa kwa ustadi mkubwa na vinapendeza sana kwa rangi, harufu na kwa ladha yake.

    Mapo Doufu ni kitoweo kingine maarufu cha Sichuan, "doufu" ni mgando wa maharege yenye maji yaliyosagwa(soybean curd), kitoweo hiki kinatumia doufu nyeupe na laini, ikiongezwa nyama ya ng'ombe ya rangi nyekundu iliyokatwa katika vipande vidogo sana, vipande vidogo vya vitungu vya rangi ya kijani na mafuta ya piliili ya rangi nyekundu, mtu akila kitoweo hicho, anasikia doufu laini mdomoni na harufu ya kunukia vizuri, tena anaona ladha ya Huajiao na pilipili. Meneja wa mgahawa wa vitoweo vya Sichuan wa Laofangzi, Bw. Wang Bing alisema, kitoweo cha Mapo Doufu kilikuweko zaidi ya miaka 100 iliyopita, tena kilikuwa na hadithi moja.

    "Awali kabisa, kitoweo hicho kilipikwa katika mgahawa mmoja mdogo ulioko karibu na daraja ya Wanfu ulioko upande wa kaskazini wa mji wa Chengdu, jina la ukoo la mwenye mgahawa ni Chen, ambaye alioa mwanamke mwenye kovu za ndui usoni mwake, mtu mwenye kovu za ndui usoni huitwa na watu kuwa ni Mazi kwa dhihaki, hivyo watu walimwita Chen Mapo, maana yake ni mke mwenye kovu za ndui wa Chen. Chen Mapo alikuwa anapenda kupika doufu pamoja na masalio ya nyama iliyosagwa, lakini kitoweo hiki ni kizuri na kitamu pia, tena kinaendelezwa hadi hivi leo."

    Hivi sasa, Mapo Doufu imekuwa kitoweo maafu hata katika dunia, isipokuwa mahali pa asili pa kitoweo hicho chenye ladha nzuri zaidi ni katika Chendu. Chakula kingine maarufu kama Mapodoufu ni nyama na mboga zilizotiwa katika maji yaliyochemka(Sichuan hot pot). Watu husema mtu aliyefika Sichuan na bila kula chakula cha Huoguo, ni sawa na mtu, ambaye hajafika Sichuan, maana ya chakula cha Huoguo ni chakula kilichoivishwa katika sufuria yenye maji yaliyochemka.

    Wenyeji wa Sichuan wanapenda sana kula chakula cha Huoguo, baadhi ya watu wanakula pamoja wakiizunguka sufuria yenye maji moto, vitu vinavyotumika katika chakula cha Huoguo ni vingi, kwanza kabisa viungo vya aina nyingi vinachemshwa katika maji, baada ya supu kukolea, wanatia vitu mbalimbali katika maji moto, mboga na nyama zilizoiva zinaliwa baada ya kuongzezwa mafuta ya pilipili, Huajiao, chumvi na mafuta ya simsim. Dada Zuo Yanmei, ambaye ni mfanya kazi katika mgahawa maarufu wa Huoguo mjini Chengdu, alitufahamisha,

    "Chakula halisi cha Huoguo ni chenye ladha tamu, harufu ya kunukia na chenye lishe bora. Supu za Huoguo ziko aina mbili za nyekundu na nyeupe, ile nyekundu ni yenye ladha ya pilipili, lakini siyo ya kuwasha sana, supu nyeupe ni yenye uwezo mkubwa zaidi ya kujenga mwili na kutunza ngozi. Baadhi ya chakula chenye umaalumu ni pamoja na nyama za ng'ombe na kuku zilizokatwa kuwa vipande vyembamba huwa ni laini hata kama zinachmshwa kwa muda mrefu; Watu wanaokula chakula cha Huoguo mara kwa mara, wanafahamu sana vyakula vitatu vya utombo wa ng'ombe, matumbo ya bata bukini na mshipa wa koo wa ng'ombe ni vitu visivyoweza kukosekana katika chakula cha Huoguo. Mbali na hayo, mazao mengine maarufu ya misitu ya mlimani kama ya uyoga wa Songrong na Niuganjun pia ni vitu vizuri katika chakula cha Huoguo."

    Chakula kingine kinachopendwa na watu kilichotokana na chakula cha Huoguo ni Chuanchuan Xiang, tofauti ya Chuanchuanxiang na chakula cha Huoguo ni kuwa vitu vya Chuanchuanxiang vinatungwa pamoja kwa vijiti vyembamba vya mwanzi, kisha vinatiwa viungo vya chakula, halafu vinachemshwa katika maji moto yaliyowekwa katika sufuria kama chakula cha Huoguo. Bw. Feng Qingshu, ambaye ni meneja wa tawi moja la mgahawa maarufu wa chakula cha Chuanchuanxiang mjini Chengdu, alisema, chakula cha Chuanchuanxiang kinaliwa kwa urahisi zaidi, ni tamu na cha bei rahisi zaidi, hivyo kinapendwa na watu wengi.

    "Chakula cha Chuanchuanxiang kinapendwa na watu wengi wawe wazee na watoto. Chakula hiki ni chenye ladha nzuri na ya bei ya chini. Nyama za n'gombe zilizokatwa kuwa vipande vidogo, uyoga, matumbo ya bata bukini na mboga nyingine zote zinaweza kutungwa katika vijiti vya mwanzi, halafu kuchemshwa. Umaalumu wake ni kutumia fedha ndogo kupata vyakula vya aina nyingi."

    Vyakula vya rahisi kuliwa pia ni moja ya vyakula vya kuwavutia walaji mkoani Sichuan. Maandazi ya vinyunya(Dumpling) yenye matunda au vidonge vya Laitangyuan vilivyochemshwa katika maji, Longchaoshou(Wonton), Zhongshuijiao, tambi za Dandan na chakula cha Sandapao ni vyakula vya rahisi kuliwa na kupendwa na watu wengi sana. Kati ya vyakula hivyo, chakula cha Feichangfen, ambayo ni makoloni yaliyoongezwa na matumbo makubwa ya nguruwe ni chakula kinachopendwa na watu wengi zaidi..

    "Makaloni ya chakula cha Feichangfen yanatengenezwa kwa unga wa viazi vikuu. Viazi vikuu vinasagwa na kukaushwa vikawa unga, na kutengenezwa kuwa makoloni. Chakula cha Feichangfen kinatumia supu iliyopikwa kwa mifupa na matumbo makubwa ya nguruwe, makoloni yale yakipikwa katika supu hiyo yanapendeza zaidi."

    Bw. Hu alisema, ingawa chakula cha Feichangfen ni chakula chepesi sana, lakini mapishi ya chakula hicho yana ufundi wake maalumu unaohifadhiwa, alishauri kuwa wakati watu wanapokula chakula cha Feichangfen, bora watumie pia Shaobing(chapati ndogo iliyookwa katika moto), kwani kula hivyo walaji wanaburudika zaidi.

    Vyakula vya rahisi kuliwa vya mkoa wa Sichuan vilitokea miaka mingi iliyopita, licha ya kuwa vyakula maalum, vina hadithi nyingi. Aina ya chakula cha rahisi kuliwa cha Sandapao, maana yake katika lugha ya Kichina ni milio mitatu ya mizinga, mtu anaposikia jina la chakula hicho ni vigumu kufahamu hicho ni chakula gani. Profesa wa chuo kikuu cha Sichuan, aliye msomi wa mila na desturi za makabila, Bw. Mao Jianhua alisema, chakula hicho cha Sandapao ni vibonge vya aina ya mchele inayonata sana, vinavyoongezwa maji ya sukari guru. Haya basi, mbona chakula hicho kinaitwa kuwa Sandapao? Hii ina sababu yake.

    "Mapishi ya Sandapao ni ya kipekee, kwanza vinatengenezwa vibonge vya mchele inayonata sana, hatua inayofuata haihusiani na ladha yake isipokuwa ni ya kiufundi, yaani kwa ajili ya kuwa na umbo la kupendeza. Mpishi anatupa kwa nguvu vibonge hivyo katika sinia tatu za shaba, kila anapotupa kwa nguvu hutoka sauti kubwa, halafu vibonge hivyo vinaingia katika chekeche ya mwanzi, ambamo kuwekwa unga wa simsim na maharage, halafu vibonge hivyo huzolewa katika beseni yenye maji ya sukari guru. Kumbe jina la Sandapao linatokana na sauti ya milio hiyo mitatu."

    Kwa kawaida watu wanachukulia miji ya Chengdu na Chongqing kuwa ni mahali asilia pa vitoweo vya Sichuan, lakini vyakula vya sehemu nyingine za mkoa wa Sichuan pia ni vya aina nyingi na vyenye umaalumu. Kwa mfano, katika mji wa Yibin, sehemu ya kusini ya Sichuan, mji huo unajulikana sana kwa kuwa na aina nyingiza vyakula vya rahisi kuliwa. Mfanyakazi wa idara ya utalii ya mji wa Yibin, Bi. Xiong Longfang alisema, mapishi ya tambi katika mji wa Yibin yako aina kumi kadhaa, endapo mtu anakula tambi katika milo yote mitatu ya siku, mapishi yake hayarudii katika muda wa nusu mwezi, chakula cha tambi maarufu zaidi ni kile cha tambi ya Ran, maana yake katika lugha ya Kichina ni tambi zinazowaka moto.

    "Tambi ya Ran ya mji wetu ni maarufu sana kwenye sehemu ya kusini ya Sichuan, chakula hiki kinapikwa kwa kazi kubwa, na kinapendeza kwa rangi, harufu na ladha. Mbona tambi hizo zinaitwa tambi zinazowaka moto? Kwa sababu mafuta yanayowekwa katika tambi hizo ni mengi, yenye ladha kali ya pilipili, mafuta ya karanga na ufuta wa Yibin. Aidha tambi hizo huwekwa pia mboga ya Yachai na karanga. Kama tambi zinachomwa kwa moto, zinaweza kuwaka, hivyo tambi hizo zinaitwa tambi ya Ran maana yake ni tambi zinazowaka moto."

    Wachina husema, chakula tamu kiko Sichuan. Watalii wanaotoka sehemu mbalimbali za dunia wanapojiburudisha kwa mandhari nzuri za Sichuan, vilevile wanafurahishwa na vyakula vitamu vya Sichuan. Bw. Cui Guangsuo kutoka Korea ya Kusini alipofanya matembezi mkoani Sichuan katika likizo lake, alisifu sana vyakula vitamu vya Sichuan.

    "Kitu kinachonivutia sana mkoani Sichuan ni mandhari nzuri, lakini nilifurahishwa sana na vyakula tamu vya Sichuan. Vyakula vingi vya Sichuan ni vyenye ladha ya pilipili kali zinazowasha, ambayo ninaipenda sana, hususan nilipata kula Mapodoufu halisi ya Sichuan, ninafurahi kweli kweli. Nina matumaini kuwa watu wa nchi nyingine pia wanaweza kuitembelea Sichuan, kushuhudia mandhari nzuri na kuonja vyakula vitamu, nina uhakika kuwa watakaa kwa furaha sana."


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako