• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sanduku la Barua

    (GMT+08:00) 2008-12-23 15:48:50
    Barua za wasikilizaji

    Msikilizaji wetu Paul Mungai Mwangi wa sanduku la posta 69 Injinia-North Kinangop Kenya ametuletea barua akisema, kwanza anapenda kuwasalimu wasikilizaji na wafanyakazi wa CRI huku akitumai kuwa sote hatujambo. Aidha, anawapongeza wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI wakiwemo watangazaji kama vile Chen, Fadhili Mpunji, Pomboo, Jeni Luteserwa na Josephine Liomba. Sauti zao humpendeza sana zinapomfikia akiwa na jamaa zake moja kwa moja kupitia redioni kwao. Hapa tunamwambia kuwa, Fadhili Mpunji, Jeni Luteserwa na Josephine wote hawapo sasa kwenye idhaa ya Kiswahili, lakini kama wanatusikiliza, watapata salamu zako, asante sana.

    Anasema, Redio China Kimataifa ni kama daraja la urafiki kati ya China na Afrika. CRI inawapamba kweli kweli wakiwa hapo kwao injinia kwa habari na matukio motomoto kutoka kila pembe ya dunia.

    Anaomba watangazaji wake aliowataja hapo juu wamtumie picha zao ili anapotazama sura zao na kusikiliza sauti zao nyororo aweze kujihisi kama yuko karibu sana nao.

    Anasema, wakenya na Afrika kwa jumla wamehuzunishwa na uhalifu uliotekelezwa na waandamanaji wa kundi la Dalai Lama tarehe 14/3/2008 huko Lasa, mji mkuu wa Mkoa wa Tibet. Vitendo vya kuua watu na kuchoma maduka na majengo bila shaka vilifanywa na watu walio nyuma kistaarabu. Yasikitisha zaidi kuona kwamba Dalai Lama hudai kuwa yeye ni kiongozi wa dini. Dini gani hii isiyothamini maisha ya binadamu na mali zao?


    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako