• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mustakabali wa Guinea bado haujajulina wazi

    (GMT+08:00) 2008-12-25 17:35:58

    Kiongozi wa wanajeshi waliofanya mapinduzi nchini Guinea, capatain wa jeshi la serikali la Guinea Moussa Dadis Camara tarehe 24 alijitangaza kuwa mkuu wa nchi, akisisitiza, amepata uungaji mkono mkubwa wa pande mbalimbali. Lakini kutokana na dalili zilizopo hivi sasa, mustakabali wa Guinea bado haujajulikana wazi.

    Wanajeshi wa Guinea waliofanya mapinduzi tarehe 24 walitangaza katika radio ya taifa, wameunda kamati ya demokrasia na maendeleo ya taifa, Bw. Camara ni kiongozi wa kamati hiyo, na kusema, "atakuwa rais wa Guinea". Taarifa inasema, tokea tarehe 24 kila siku kuanzia saa 2 usiku hadi saa 12 alfajiri ya siku ya pili ni marufuku kutoka nje ili "kuhakikisha utulivu wa jamii". Lakini baadaye ilisema, marufuku hayo yataanza tarehe 26 ili kuwawezesha wananchi washerehekea sikukuu ya Krismas. Mapema ya siku hiyo, wanajeshi hao walitoa taarifa katika radio ya taifa kuwa uchaguzi mkuu wa nchi utafanyika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka 2010. Walisema, uchaguzi mkuu utakaofanyika wakati huo utakuwa wa haki, kuaminika na uwazi.

    Wanajeshi elfu kadhaa waliofanya mapinduzi siku hiyo walifanya mandamano huko Conakry, mji mkuu wa nchi hiyo, ambapo Camara alisimama katika gari la kwanza, akifunikwa na bendera ya Guinea, na aliwapungia mkono watu waliotoka kuwaangalia.

    Waziri mkuu wa Guinea, Bw. Ahmed Tidiane Souare, ambaye hajulikani mahali alipo baada ya kuzuka mapinduzi, tarehe 24 alizungumza kwa njia ya simu na waandishi wa habari, serikali yake bado inadhibiti hali ya nchi hiyo, Camara hajadhibiti jeshi zima, na wingi mkubwa wa wanajeshi wanatii serikali. Kutokana na katiba ya nchi ya Guinea, spika wa bunge la taifa, Aboubacar Sompare angechukua madaraka ya rais, amekuwa akitoa wito wa kutaka jumuiya ya kimataifa izuie jaribio la mapinduzi ya wanajeshi wa Guinea.

    Jumuiya ya kimataifa inaona mapinduzi ya nchini Guinea ni kujitwalia madaraka ya urais, hayaambatani na katiba ya nchi, ambayo yamesababisha msukosuko wa jamii na kuleta athari mbaya kwa dunia. Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika lilitoa taarifa tarehe 24 usiku likisema, mapinduzi yaliyofanywa na wanajeshi katika miaka ya karibuni yamekuwa tisho kwa amani na usalama wa Afrika, na ni pigo kubwa kwa mchakato wa demokrasi unaoendelezwa barani Afrika. Taarifa inaitaka kamati ya Umoja wa Afrika, ambayo ni idara ya utendaji ya umoja huo, iweke kazi ya kukinga mapinduzi ya wanajeshi katika ajenda ya kazi za idara ya utungaji sera ya Umoja wa Afrika, kuchukua hatua kutoka pande mbili za sheria na kutoa onyo mapema ili kuzuia kuzuka tena kwa mapinduzi ya wanajeshi wa Afrika. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Bw. Robert Wood alidokeza siku hiyo, Marekani inakaa chonjo juu ya mabadiliko ya hali ya Guinea, na itafanya uamuzi katika siku chache zijazo kuhusu kukatisha au la utoaji wa misaada kwa nchi hiyo. Marekani inatarajia Guinea itaweza kurejesha utawala wa kikatiba haraka iwezekanavyo.

    Mbali na hayo, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya uchumi wa nchi za Afrika ya magharibi, ECOWAS, zimetoa matamko zikitaka pande mbalimbali za nchini Guinea ziache kutumia nguvu za kimabavu.

    Nchi ya Guinea iko kwenye sehemu ya magharibi ya Afrika, ilipata uhuru wake mwaka 1958. Nchi hiyo ina maliasili nyingi zikiwa ni pamoja na dhahabu, almasi na shaba, hususan ni bauxite, ambayo inachukua nafasi ya kwanza kwa wingi duniani. Lansana Conte alijitwalia madaraka ya urais baada ya kufanya mapinduzi mwaka 1984, na alitawala kwa miaka 24. Takwimu inaonesha, katika miaka ya 90 ya karne ya 20, kiasi cha mfumuko wa bei za vitu nchini Guinea kilikuwa 4%, hivi sasa ni 20%, ongezeko la uchumi linapungua kwa mfululizo na ghasia zinatokea mara kwa mara katika nchi hiyo.

    Mchambuzi alisema, katika hali ya hivi sasa, jumuiya husika za kikanda na kimataifa zinatakiwa kutoa hatua zenye ufanisi haraka, kuhakikisha utulivu wa Guinea, kuhakikisha mawasiliano kati ya vyama vya kisiasa na jeshi, na kuepusha matukio ya kumwaga damu, la sivyo, mapinduzi ya kijeshi yatatokea moja baada ya nyingine, na madaraka ya serikali yatadhibitiwa na wanajeshi waliofanya mapinduzi. Katika miaka michache ijayo, Guinea itashika njia ya kurejesha utawala wa kikatiba na kufanya uchaguzi mkuu mapema iwezekanavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako