• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua za wasikilizaji wetu

    (GMT+08:00) 2008-12-31 17:40:38

    Kuanzia mwezi huu wa Desemba, tovuti ya Idhaa ya Kiswahili imepangiliwa upya, wasomaji wetu wameandika maoni yao kwenye tovuti yetu. Bw. Ali Juma anaomba kuwe na vipindi vya mpira wa miguu kwa timu za China.

    Thabiti Mugemangango wa Africa 93.5 Kigali anasema, kwa kweli mmefanya mabadiliko makubwa saana, tovuti hii inapendeza zaidi. Tovuti ya CRI ambayo naipenda sana kwa habari zake. Niko tayari tufanye kazi pamoja, kwa kuwapa habari za hapa Rwanda.Nawatakia kazi njema. Email yangu ni bobthab@yahoo.com

    Bw. Xavier L. Telly-Wambwa wa P.O Box 2287, Bungoma, KENYA anasema, ni wazo langu kuwa sura ya tovuti yetu ni ya kupendeza mno. Tutaendelea kuzoea na wasikilizaji wenzangu kuhusu kusoma vipindi kem kem katika tovuti yetu nzuri ya sura mpya

    Mogire Machuki wa Village sanduku la posta 646 Kisii Kenya anasemea, bila shaka ni salamu za kila la kheri kutoka hapo Kisii Kenya. Nina furaha kuingia kwenye tovuti hii mpya kabisa ya Radio China Kimataifa, ambayo inavutia na kuliwaza lakini kwa mtazamo wangu ile ya awali ilikuwa na habari kemkem kushinda hii hata hivyo sura ya hii ya sasa inapendeza. Hongera si haba kwa kazi njema kila la kheri kutoka Kisii Kenya.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako