Ikulu ya Senegal tarehe 2 ilitoa taarifa ikisema, rais Abdoulaye Wade wa nchi hiyo tarehe 1 alimwandikia barua mwenyekiti wa "kamati ya demokrasia na maendeleo ya taifa" Kepteni Diarra Camara na kumhimiza kuamua tarehe ya kufanya uchaguzi mkuu haraka iwezekanavyo.
Taarifa inasema, kutokana na Bw. Camara kutoamua tarehe ya uchaguzi mkuu, rais Wade ameamua kuahirisha ziara yake nchini Guinea.
Baada ya mapinduzi ya kijeshi kufanyika nchini Guinea, rais Wade wa Senegal aliunga mkono serikali ya kijeshi ya Guinea, na kutuma mjumbe maalumu kwenda nchini humo. Rais Wade atafanya ziara nchini humo na kutoa wito kwa nchi jirani za Guinea kutoingilia kati mambo ya ndani ya Guinea.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |