• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua za wasikilizaji

    (GMT+08:00) 2009-01-06 20:47:41

    Msikilizaji wetu Kituyi M.Peter ambaye barua yake huhifadhiwa na Daniel Ngoya wa sanduku la posta 1674 Bungoma Kenya ametuletea barua akisema kuwa, ni matumaini yake kwamba tu wazima hapa tulipo na tunaendelea vizuri na kazi yetu ya utangazaji wa kuwapeperushia wasikilizaji wetu matangazo ya kuboresha maisha yao, na hao wangependa kujiunga nasi.

    Anasema, hii ni mara yake ya kwanza kuomba usajili kutoka kwetu na ana matumaini kuwa atafurahi kama atapata usajili maana huwa anatamani sana kujiunga nasi, lakini huwa hapati mtu wa kumsaidia. Kwa bahati nzuri, mwezi huu alimpata rafiki yake wa ndani ambaye ni Daniel Ngoya wa sanduku la barua 1674 Bungoma Kenya. Yeye ni kama ajenti wetu huko Bungoma. Alimpa habari kemkem kuhusu CRI na kumshauri kuwa atamsaidia hadi apate usajili kutoka kwetu. Naomba tu Maulana ibariki CRI na watangazaji wote wa CRI maana wanachangia pakubwa sana kuboresha maisha yake, anashukuru kazi nzuri tunayofanya.

    Tunamshukuru kwa dhati Bw. Kituyi M.Peter kwa barua yake ya kuomba kujiunga nasi, sisi tunamkaribisha kwa mikono miwili. Ni matumaini yetu kuwa ataendelea kusikiliza matangazo yetu na kutoa maoni na mapendekezo yake.

    Msikilizaji wetu Francis Onderi wa sanduku la posta 81 Kisii Kenya ametuletea barua akisema, pokea salamu kutoka Kisii ni matarajio yangu kwamba nyote ni wazima. Hapa Kisii tunaendelea vema na ni pongezi jinsi mnavyotangaza michezo ya Olimpiki ambayo iliendelea vizuri mjini Beijing. Ni pongezi kwa nchi ya China kwani imeonesha mfano mwema kwa kunyakua medali nyingi na kwa kuonesha heshima kuu kwa wageni, pongezi sana.

    Anasema, tangu nianze kutegea sikio matangazo yenu mwezi Machi mwaka huu sasa nimepata kunufaika sana kwa habari kuhusu China na dunia yote kwa jumla. Kuhusu Michezo ya Olimiki kwa kweli imepiga hatua kuu kwa kutumia kila mbinu kuifanya hii michezo kuwa ya kiwango cha hali ya juu. China imeonesha dunia ya kwamba ilikuwa katika nafasi njema kwa kutunukiwa hii zawadi ya kuandaa hii michezo, hongera sana kutoka kwangu.

    Kuhusu matangazo yenu usikivu ni mzuri kabisa na kwa kusema ukweli wengi wamefaidika kwa njia moja au nyingine kutoka kwa vipindi vyenu. Radio China Kimataifa imekuwa ni kituo cha pekee kwa kutoa habari kamili juu ya michezo ya Olimpiki kila mahali watu wanafungua Radio China Kimataifa kupata habari nyingi za Kimataifa.

    Mwisho anatutakia mema na ni matarajio yake kwamba katika mashindano ya chemsha bongo ya mwaka huu atajaribu bahati yake akiwa na matarajio ya kupata nafasi maalum ili kualikwa kutembelea China nchi ambayo tangu utotoni anaipenda, na ndoto yake ni kupata fursa ya kuitembelea japo siku moja maishani mwake kwa hivyo anaomba tumtumie bahasha ambazo zimelipiwa, Tshirt yenye nembo ya Radio China Kimataifa, kalamu, Jarida la China today na vipandikaji kofia.

    Tunamshukuru kwa dhati Francis Onderi kwa barua yake ya kutuelezea usikivu wake wa matangazo yetu hasa kuhusu Michezo ya Olimpiki ya Beijing, na kupongeza kwa dhati kazi yetu. Asante sana. Ni matumaini yetu kuwa atashiriki kila mara mashindano ya chemsha bongo ili kupata mafanikio mazuri. Lakini muhimu zaidi ni kushiriki.

    Msikilizaji wetu Devotha Mashalla wa sanduku la posta 434 Shinyanga Tanzania ametuletea barua akisema, habari za siku nyingi? Poleni sana na shughuli za utangazaji wa idhaa yenu ya Kiswahili ya Radio China Kimataifa japo ni siku nyingi hatujawasiliana ila ana tumai Mwenyezi Mungu yuko nasi katika shughuli zetu. Mimi rafiki yenu si jambo kabisa ila nimebanwa sana na shughuli za kimasomo kwani niko kidato cha sita, hivyo najiandaa na mtihani wa mwisho ambao tunatarajia kufanya kuanzia hapo mwakani yaani 2009 mwezi wa pili, ndio maana nilishindwa kuwasiliana na nyie kwa muda mrefu sana.

    Anasema, dhumuni la barua hii hasa ni kutaka kuwaeleza nia yangu ambayo ni ndoto yangu katika maisha. Napenda sana kazi ya utangazaji wa radio au televisheni tangu nilipokuwa mdogo nilikuwa na ndoto za kuwa mtangazaji mkubwa na maarufu nchini Tanzania au hata duniani. Kutokana na kupenda sana kazi hiyo nilianza kufanya mazoezi ya utangazaji katika sherehe ndogondogo kama za kuzaliwa nilipokuwa shule ya msingi na nilipokuwa sekondari. Hivyo napenda kuwaomba kunisaidia kuitimiza ndogo yangu ya kuja kuwa mtangazaji napenda sana kwani ndio ndoto yangu ambayo kila siku naiota na ninaamini siku moja itatimia naombeni ushirikiano wenu na ushauri wenu marafiki zangu , natarajia nitakapomaliza masomo yangu ndio kozi ninayoipenda kuisomea nitakapoenda chuo kikuu.

    Tunamshukuru Devotha Mashalla kwa barua yake ya kutuelezea ndoto yake ya kuwa mtangazaji wa radio au televisheni. Maelezo yake yanatufurahisha sana. Kwani yeye ana ndoto tena ana nia ya kufanya bidii kuwa mtangazaji. Lakini tunaona sasa tunaweza tu kumwambia kuwa jambo muhimu la sasa kwake yeye ni kusoma kwa bidii masomo yake ili siku za usoni aendelee na masomo katika chuo kikuu, na kutimiza ndoto yake ya kuwa mtangazaji, anatakiwa kushikilia nia yake bila kulegalega.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako