• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ibrahim Elias mwanafunzi wa Tanzania hapa Beijing

    (GMT+08:00) 2009-01-09 14:56:56

    Mwanafunzi mmoja wa Tanzania anayesoma katika chuo kikuu hapa Beijing, China. Ili kujua mengi zaidi kuhusu mwanafunzi huyo endelea kututegea sikio, kwanza kabisa hebu tumsikilize kwanza anavyojitambulisha

    "Mimi naitwa Ibrahim Elias, ni mwanafunzi wa hapa, chuo kikuu cha mawasiliano cha Beijing. Mimi natoka Tanzania, Geita, Mwanza. Nimefika hapa mwaka 2006, miaka mitatu sasa. Hapa nasoma kozi ya mawasiliano, ni shahada ya kwanza."

    Mawasiliano ni jambo muhimu katika sehemu yoyote duniani, ndiyo maana mwandishi wetu wa habari alivutiwa sana na kumdadisi Bw. Ibrahim kuhusu hali ya mawasiliano kwenye sehemu ile aliyoishi nchini Tanzania: Alisema,

    "Hali ya mawasiliano ni nzuri. Hamna tatizo. Kwa sababu ndio ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Tanzania. Wanatumia simu ya mkononi, internet. Kwa sababu ndio tuseme ni mji wa kibiashara ambao umezungukwa na ziwa Victoria. Kwa hiyo ni mji maarufu ukifika Tanzania."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako