• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua 0106

    (GMT+08:00) 2009-01-13 15:21:57

    Msikilizaji wetu Wambulwa M. Evans ambaye barua zake huhifadhiwa na DanielNgoya wa sanduku la posta 1674, Bungoma Kenya ametuletea barua akisema, ni matumaini yangu kuwa nyote hamjambo na mnaendelea na kazi huko mliko. Ningependa kuwashukuru wafanyakazi wote wa CRI kwa kazi nzuri ambayo mnatufanyia sisi wasikilizaji wenu, tena ninamshukuru mungu kwa kuyajibu maombi yangu. Nilikuwa nikiomba mungu kuniwezesha kuyajibu maswali ya chemsha bongo ambayo mlituandalia kwa njia nzuri.

    Nashukuru sana CRI kwa kutoa ama kuchagua mawakala wenu huko Bungoma ambao wamejulikana sana kwa sababu ya CRI. Kwa kweli nilimpata mmoja wao ambaye anaitwa Daniel Ngoya ambaye amekuwa karibu sana kwa mambo yote ambayo yanahusu CRI. Amenisaidia sana mpaka hizi kadi za salamu yeye ndiye huwa anazituma huko kwenu. Amekuwa msaada kwangu sana kwani amenielekeza hata jinsi ya kujaza na kutuma chemsha bongo, namuombea Baraka ili naye awe mshindi.

    Ni matumaini yangu kuwa Mungu akinijalia nikiwemo nitaweza kukutana na watu mashuhuri. Nakumbuka katika kitabu cha Joshua mlango wa nane mstari wa kwanza unasema kwamba "Msiogope, maana mimi ni Mungu wa Israel niko nawe sasa natumaini kuwa atakuwa nami pia. Asanteni kwa kuniletea maswali ya chemsha bongo na Mungu aibariki CRI iendelee.

    Tunamshukuru msikilizaji wetu Wambulwa M. Evans kwa barua yake ya kueleza usikivu wake na nia yake ya kushiriki kwenye chemsha bongo. Ni matumaini yetu kuwa ataendelea kusikiliza kwa makini matangazo yetu na kutoa maoni na mapendekezo yake ya kutusaidia kuboresha matangazo yetu.

    Msikilizaji wetu Martin Wekesa Wanyama wa Bungoma Kenya ametuletea barua akisema, ningependa kutoa shukrani nyingi kwa zawadi mlizonitumia kutokana na ushindi nilioupata wa chemsha bongo iliyopita ya tukutane Beijing 2008 kwenye Michezo ya Olimpiki. Hakika zawadi ni nzuri sana.

    Napenda kutuma pongezi sana kwa nchi ya China kwa ujumla kwa kupitia Redio ya CRI, kimaendeleo, kimichezo, kisayansi na kitekinolojia na jinsi nchi ya China inavyokuwa kimaendeleo. Sifa ya China inavutia kila pande za dunia, hasa Kenya na Sudan kwa uwekezaji rasilimali na kuinua nchi hizo zilizoathiriwa kwa kutoa misaada na kudumisha amani na uzinduzi wa teknolojia za kisasa ambayo imefanya China kuogopwa na mataifa makubwa hasa Amerika

    Shukurani zangu nyingi ni jinsi mnavyokuwa nasi pamoja wakati wa mgogoro uliopita wa hapa Kenya, naomba muendeleee na moyo huohuo.


    1 2 3 4
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako