• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Erick Araka Mokua mwanafunzi wa Kenya mjini Beijing

    (GMT+08:00) 2009-01-23 16:29:50

    Katika vipindi vilivyopita vya Daraja la Urafiki kati ya China na Afrika, tunapata fursa ya kusikiliza maelezo ya wageni mbalimbali, kufahamishwa hali yao, na maisha yao hapa China. Katika kipindi cha leo tutawaletea mahojiano kati ya mtangazaji wetu Pili Mwinyi na Bw. Erick Araka Mokua kutoka Kenya anayesoma katika chuo kikuu cha safari ya anga ya juu na usafiri wa ndege cha Beijing. Mahojiano hayo yalianzia ufungaji wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing.

    Pili: Ulishiriki ukiwa kama mwigizaji siku ile ya ufungaji kwenye uwanja wa michezo ya taifa "kiota". Unaweza kutuelezea kidogo uliigiza kitu gani, ama ulishiriki kwenye kikundi gani?

    Erick: Katika ule uigizaji, mimi nilikuwa nikiwakilisha waafika wote duniani. Tulikuwa na watu watatu. Ilikuwa ni baada ya lile "gari la London", na kisha ilikuwa kuagana na Wachina waliokuwa wametukaribisha. Na pale tulipokuwa tunaigiza, Wachina walitupa zawadi. Kisha tulipopanda ngazi ya kuingia ndege, tuliweza kufungua ile zawadi, tuweze kujua ni zawadi gani marafiki zetu wa China wametupa, na zawadi ilikuwa ni siku 16 za Michezo ya Olimpiki.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako