• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua za wasikilizaji 0203

    (GMT+08:00) 2009-02-03 16:36:28

    Msikilizaji wetu Francis Njuguna wa Nairobi Kenya ambaye anuani yake kwenye mtandao wa internet ni osnjuguna@yahoo.com ametuletea barua akisema kuwa, ningependa kupata anuwani ya offisi ya Radio China Kimataifa jijini Nairobi, Kenya, ama email yao, ama simu yao, ningependa kuwasiliana nao.

    Tena naomba nipate kutuma salaamu zangu kwa mama mary waniu akiwa kibichoi, divisheni ya Githunguri, wilayani Kiambu, mkoa wa kati, ndugu yangu, samuel karago akiwa kijiji cha Kibichoi, wilyani kiambu, Wanjiku wa Karago akiwa Kibichoi, wilayani Kiambu, Hanna Nyawira akiwa shule ya secondari ya Nembu, wilayani Gatundu, na mwisho David Wakaba ambaye pia yuko katika kijiji cha Kibichoi, wilayani Kiambu.

    Ujumbe wake unasema, Radio China Kimataifa ni nambari moja inaongoza na zingine zinafuata.

    Na mwisho kwa mtayarishaji, naandika ili nipate kuitakia Radio China Kiamtaifa kila la heri na fanaka katika kipindi hiki cha mwaka huu mpya wa 2009. Hakika radio hii tuipendayo imepata kufanya mengi katika vipindi vya hapo nyuma na ni matumaini yetu kwamba itaendelea kufanya mengi katika kipindi hiki cha mwaka huu mpya kwa kila njia

    Mungu aibariki Redio China kimataifa, ili ipate kuhudumia wasikilizaji wake wote ulimwenguni ambapo lugha hii ya kiswahili inatumika.

    Tunakushukuru sana msikilizaji wetu Francis Njuguna kwa dua zako za kuiombea Redio China Kimataifa, na daima CRI itakuwa mbele katika kuwaelimisha na kuwaburudisha wasikilizaji wetu wote popote pale walipo. Kuhusu anuwani ya ofisi yetu ya Nairobi tutakuambia kwa barua pepe.

    Na msikilizaji wetu Ng'ang'a wa Gatibui wa sanduku la posta 120 Kibichoi, wilayani Kiambu, Mkoa wa Kati ametuletea barua pepe akisema kuwa, kwanza pokea salaam zangu kutoka Nairobi, Kenya, naomba nafasi nipate kuipongeza Radio China Kimataifa kwa kazi yake maridhawa kabisa juu ya upashanaji habari na mambo mengine kuhusu nchi ya China na mataifa mengine ulimwenguni.


    1 2 3 4 5 6 7
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako