• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maisha ya Mwalimu Magreth Komba nchini China

    (GMT+08:00) 2009-02-06 15:19:36

    Bi. Magreth Komba anatoka Tanzania, ana uzoefu wa miaka kumi wa kufundisha. Sasa amefika hapa Beijing na anasomea digri ya udaktari wa ualimu na mitaala katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Beijing. Kwa kuwa yeye ni mwalimu wa muda mrefu, kwa hiyo anaipenda sana kazi yake. Upendo wake kwa kazi hiyo unamfanya atake kubobea zaidi katika ufundishaji na jinsi gani ya kuandaa mitaala, hivyo amekuja China kwa ajili hiyo.

    "Jina langu naitwa Magreth Komba, ni mzaliwa wa Tanzania katika mkoa wa Ruvuma ambao uko kusini mwa Tanzania. Nilikwenda kusoma masomo yangu ya ualimu katika chuo kikuu cha Mpwapwa. Halafu nikahamia chuo cha Dar es Salaam cha ualimu wa diploma, kwa hiyo nilipata stashahada mzuri ya kuweza kufundisha ualimu au sekondari. Baada ya hapo, nilipata kazi ya kufundisha walimu wa daraja la kwanza ambao wale walimu wanaandaa kufundisha watoto wetu wa shule ya msingi. Baadaye nikaenda Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo nikaweza kumaliza digri yangu ya kwanza ya ualimu na masomo ya arts, kwa hiyo baada ya hapo nikaenda kufundisha Chuo cha ualimu cha Dar ambacho kwa wakati ule kilikuwa kinaitwa cha ng'ombe TTC. Niliwafundisha wanafunzi ambao watakuwa walimu wa sekondari. Baada ya kufundisha nikaweza kuendelea na masomo ambapo niliweza kusoma digri ya pili. Sasa nikapata udhamini tena ndiyo maana nikaja kusoma udaktari wa ualimu na mitaala. Hapa Beijing nilifika mwaka jana yaani 2007, mwezi Septemba tarehe 5, na nimekaa mwaka mmoja na miezi minne sasa."

    Kutokana na mila na desturi tofauti, wageni wengi wanapokuja hapa China wanakumbwa na matatizo mengi katika maisha yao hasa kuhusu chakula na lugha. Na Bi. Komba je, amekizoea chakula cha kichina? Na "Huo Guo" ni chakula gani?

    "Kwa kweli mwanzoni nilikuwa na shida ndogo, lakini sasa hivi nimeshazoea. Chakula cha kichina ni kizuri, kiko aina mbalimbali. Kwa kweli ile milo ina vitu vingi sana, nakula sina shida. Nakula kila kitu, lakini nashidwa kula mbwa. Kwa mfano tukienda kula chakula cha jioni pamoja na marafiki, kuna ile "Huoguo", maana yake vitu vinachemka hapo. Unachukua nyama unaweka, hata dakika mbili hazijaisha unakula, ni kitu ambacho kwa kweli kule Tanzania hamna. "


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako