• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua za wasikilizaji 0210

    (GMT+08:00) 2009-02-10 15:48:04

    Msikilizaji wetu Exaud John Makiyao wa S.L.P 8110 Moshi Tanzania yeye ametuandikia barua yake yenye kichwa cha habari mzozo wa kifedha duniani, ni kitendawili kisichoteguliwa kisiasa. Anasema masoko muhimu ya hisa yanaendelea kuanguka duniani kote, licha ya hatua kubwa zinazochukuliwa na serikali kadhaa katika juhudi za kuukabili mgogoro huo wa fedha.

    Pamoja na hatua hizo ni uamuzi wa serikali za Marekani na Uingereza kutenga mabilioni ya fedha kwa lengo la kujinusuru na mzozo huo.

    Uingereza (nchi inayoshikilia nafasi ya tatu katika nguvu za uchumi barani Ulaya), imeenda zaidi hadi kutangaza mpango wa kutaifisha sehemu ya mabenki makuu ya nchi hiyo.

    Lakini je, hilo ni suluhisho la kudumu la mzozo huu wa kefedha Duniani?

    Viongozi wengi wa kisiasa, wanakubaliana juu ya umuhimu wa kupata ufumbuzi.

    Hata mimi Makyao nahitaji kuona mzozo huu wa kifedha Duniani unapatiwa ufumbuzi, lakini cha msingi ni kutafuta ufumbuzi endelevu.

    Kwani nchi mbalimbali kuidhinisha mabillioni ya fedha kunatoa uhakika wa kutatua mzozo huo wa kifedha kwa kiwango gani kiuchumi?

    Mgogoro huu wa kifedha ukishughulikiwa kisiasa, utakwepa kujibu maswali ya msingi yafuatayo:-

    1. Mabunge ya nchi mbalimbali kukubali Kuidhinisha hayo mabillioni kutakuwa na athari gani kwa mwananchi wa kawaida mlipa kodi?

    2. Je kuokoa masoko ya fedha leo bila kuziba mianya iliyopelekea kitimtim hicho cha kifedha kutazuiaje tatizo hilo kuibuka tena baadaye?

    3. Sera za nje za mataifa makubwa hasa katika matumizi ya KIJESHI, hazikuchangia chochote katika kusababisha mzozo huu wa kifedha Duniani?

    4. Na je, wanauchumi duniani hawaoni kwamba mzozo huu wa kifedha una uhusiano na kuanguka kwa biashara ya uuzaji wa majumba nchini Marekani na kutokuwepo sera madhubuti za utoaji mikopo?

    Anasema kwa maoni yangu, Wanasiasa wanachofanya ni kupambana tu na athari za mzozo huu wa fedha na wala si kufanya chochote kuhusu chanzo chake. Ingekuwa vema watunga sera za kiuchumi duniani wakakaa pamoja na kuunda sera makini zitakazoleta suluhisho la muda mfupi na mrefu wa mzozo huu. Mimi nikiwa mwanauchumi naamini kwamba, kuna haja ya kudhibiti utendaji kazi wa masoko makubwa ya fedha duniani, taasisi kubwa za fedha, shirika la Fedha Duniani IMF na Benki ya dunia.


    1 2 3 4 5 6
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako