• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Lilian na Daniel: Mke na mume kusoma katika nchi moja kwa wakati mmoja

    (GMT+08:00) 2009-02-13 11:21:50

    Pili: Karibuni katika kipindi hiki cha Daraja la Urafiki kati ya China na Afrika. Leo hapa studioni, niko pamoja na wenzangu katika kipindi hiki.

    Lilian: Mimi ni Lilian, leo tuna mgeni wetu, tumkaribishe.

    Daniel: Jina langu ni Daniel Gustar Lyimo. Mimi ni Mtanzania, na ninasoma katika mji wa Wuhan, nimesoma masomo ya MBA kwa miaka miwili.

    Pili: Umefika hapa China mwezi gani?

    Daniel: Nimekuja China mwishoni mwa mwezi wa tisa mwaka 2008, na nimeanza rasmi masomo mwezi wa kumi. Na mpaka sasa ni karibu miezi mitatu.

    Lilian: Ninafurahi sana, mimi ni mke wa Daniel. Mimi nilikuja China mwishoni mwa mwezi wa tisa mwaka 2007, na mimi ninasoma masomo ya diplomasia katika chuo kikuu cha umma.


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako