• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua za wasikilizaji 0217

    (GMT+08:00) 2009-02-17 15:41:31

    Msikilizaji wetu Bi Halima Ijeiza wa sanduku la posta 14, Ndori Kenya

    Ametuletea barua akisema, pokeeni salamu zangu nyingi za mwaka mpya wa 2009, nikiwa na wingi wa matumaini kuwa nyote hamjambo, nami pia ni mzima. Nimejawa na furaha nyingi kutokana na kupokea zawadi toka kwenu za kadi ya "commerative card of 2008, beautiful Guanxi knowledge contest",kadi za salamu na bahasha iliyolipiwa. Nashukuru sana ila ningeomba mnitumie na kalenda ya mwaka huu.

    Ingawaje siku hizi sisikilizi vipindi vyenu mara kwa mara kutokana na kuwa saa nne usiku hunikuta nikiwa nimeshalala lakini "wengi wape" ninaamini kuwa ipo siku na muda mwafaka kwa wote wanoipenda idhaa hii.

    Nikimalizia naomba kutumiwa majibu sahihi ya chemsha bongo ya mwaka 2007. Naamini ipo siku bahati itakuwa yangu kushinda katika mshindano haya ya chemsha bongo, na kuweza kusafiri kuja nchini China kujionea kwa macho nchi ya maajabu hususan studio za CRI.

    Sina mengi zaidi ya hayo, nawatakia heri na fanaka katika mwaka huu.

    Asanteni na kwaherini.

    Msikilizaji wetu Ramadhani Hamisi wa sanduku la posta 14 Ndori Kenya ametuletea barua akisema, watangazaji wapendwa , salamu nyingi za heri na fanaka ya mwaka mpya wa 2009,kutoka kwangu na familia yangu. Sisi ni wazima wa afya, hofu juu yenu tu.

    Naandika barua hii nikiwa na furaha nyingi kutokana na zawadi mlizonitumia, ikiwa ni kadi ya mwaka mpya, bahasha iliyolipiwa na "commemorative card of 2008, beautiful Guanxi knowlegde contest" Nashukuru sana ila kilichokosekana ni kalenda ya mwaka huu tu. Ningependa kutoa dukuduku langu juu ya muda wa kusikiliza Radio China Kimataifa, kwani saa nne ninakuwa nimelala.Hata hivyo sina la kufanya kutokana na wasikilizaji wengi wanendelea kuipata vyema.

    Ninapenda kutia tamati huku nikiwa na wingi wa matumaini kuwa tutaendela kuwasiliana mara kwa mara.Aidha ninaamini kuwa siku moja nitaweza kupata nafasi maalum katika chemsha bongo ambapo nitaweza kutembela vivutio mbalimbali nchini China, hususan Radio china kimataifa.

    Asanteni na kwaherini.


    1 2 3 4 5 6 7
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako