• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hadithi ya Mfanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi wa Ng'ambo ya CGC Zemedkun Asfawkun

    (GMT+08:00) 2009-02-20 17:00:51

    Kiwanda cha vioo cha Hansom nchini Ethiopia ambacho kinawekezwa na kujengwa na Kampuni ya Ujenzi wa Ng'ambo ya China CGC, pia ni kiwanda cha kwanza cha vioo cha nchi hiyo.

    Bw. Zemedhkun Asfawkun aliwahi kusoma nchini China kwa miaka mitano na kufanya kazi hapa kwa mwaka mmoja. Anaweza kuongea kichina vizuri, pia anaipenda sana China sana. Baada ya kurudi Ethiopia, Bw. Zemedhkun alifanya kazi katika idara ya serikali ya Ethiopia kwa muda mrefu na kupata mafaniko mengi. Je, kwa nini baadaye Bw. Zemedhkun alichagua kazi ya Kampuni ya Ujenzi wa Ng'ambo ya China CGC? Alisema,

    "Nafurahi sana kujiunga na kampuni hiyo, zamani nilifanya kazi katika idara ya serikali, ingawa cheo changu ni cha juu, mwishoni nashiriki kwenye kampuni hiyo, kwa kuwa kampuni hiyo ina maana maalumu kwa Ethipotia. Kama tujuavyo, Misri na Afrika Kusini zina viwanda vya kioo, lakini katika sehemu ya katikati na mashariki mwa Afrika ni Ethiopia tu inayoanza kujenga kiwanda cha kioo. Naona furaha kuwa kampuni hiyo ni ya kwanza, na pia ni kubwa zaidi katika sekta hiyo."

    Ni kweli kabisa, kama Bw. Zemedhkun alivyosema zamani Ethiopia haikuwa na kiwanda cha kioo, na hali hiyo iliathiri vibaya maendeleo ya ujenzi ya Ethiopia. Kwa kutazama fursa hii ya kibiashara, Kampuni ya Ujenzi wa Ng'ambo ya CGC na Mfuko wa Maendeleo ya China na Afrika zinashirikiana kujenga kiwanda cha kioo cha kwanza nchini Ethiopia ambacho hivi sasa kimefika kipindi cha mwisho cha kukaguliwa na kutazamiwa kuanza kuzalisha vioo hivi karibuni.

    "Nchi za Afrika zikiwemo Ethiopia zinakaribisha sana makampuni za China za ujenzi kuja kuzisaidia kujenga miundombinu ambapo zinakaribisha na kuhitaji zaidi makampuni hayo kuja kuwekeza na kuwasaidia katika sekta ya maendeleo ya utengenezaji. Zinaitilia maanani sana sekta hiyo ambayo ni muhimu sana katika maendeleo ya uchumi wa Ethiopia."

    Kufuatia kuanza kwa mstari wa kuzalisha kioo, kiwanda hicho kitabadilisha historia ya kutozalisha kioo nchini Ethiopia hasa katika sehemu ya Afrika ya mashariki. Vioo vinavyotengenezwa hapa pia vinaweza kuuzwa katika nchi nyingine za Afrika Mashariki na kuchuma fedha nyingi zaidi za kigeni kwa Ethiopia. Hilo ni jambo zuri kwa serikali ya Ethiopia inayohitaji fedha za kigeni. Bw. Zemedhkun alisema,

    "Zamani tulinunua vioo kutoka nchi za nje, sasa tunaweza kutumia vioo vinavyotengenezwa nchini Ethiopia, baadayae tutaviuza katika nchi za nje. Jambo hilo lina umuhimu maalumu na ni jambo zuri kwa Ethiopia na uchumi wake."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako