• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua za wasikilizaji 0224

    (GMT+08:00) 2009-02-24 15:33:27

    Msikilizaji wetu Martin Y. Nyatundo wa sanduku la posta 3701 Kisii Kenya ametuletea barua akipenda salamu nyingi zitufikie toka Kenya, anasema, mimi hapa sina neno ila ni kuendelea kuchapa kazi huku tukiendelea kutegea sikio matangazo ya idhaa yetu ya Radio China kimataifa. Ni huzuni ilioje kwa wale wasioweza kuitegea radio hii.

    Ni pongezi na shukrani sana kwa kubadilisha muda wa matangazo katika Radio KBC Nairobi toka saa tisa mchana hadi saa nne usiku.Hii ni kwa sababu watu wengi wako kazini ,lakini saa nne watu wengi wako mapumzikoni nyumbani.Ni ombi langu kuwa katika kitumbuizo cha matangazo ya muda wa saa tisa au saa nane,tafadhali rekebisheni au mbadilishe .Hilo ndio ombi langu.

    Kabla ya kuhitimisha tafadhali nitumieni CD ya kuwa nami jifunze kichina, VCD za nyimbo za kichina, picha za watangazaji, nakala ya china Today na ikiwezekana kofia ya CRI.

    Shukrani sana msikilizaji wetu Martin Y. Nyatundo kwa barua yako, maoni yako ya kubadilisha tangazo la muda wa vipindi tumeyapokea na tutajitahidi kurekebisha ili tusichanganye watu na kuhusu ombo lako la kukutumia hizo CD tunatazama uwezekano na baadaye tutakuarifu.

    Msikilizaji wetu Abdillahi Shabani wa sanduku la barua 2667,Kakamega Kenya ametuletea barua akisema, pokeeni wingi wa salamu toka Kenya, ama baada ya salamu mimi sijambo, ningependa kushukuru mungu kwa kuweka uhusiano mzuri kati yetu hadi mwaka unapoelekea ukingo

    Leo nina ujumbe ninaopenda kutetea watoto na kuhimiza wazazi kuwapatia elimu ,ujumbe wangu uko katika njia ya shairi, kichwa cha shairi ni "kunyanyasa watoto"

    Wakubwa msiudhike ,leo ninauliza,

    Wala msibabaike,haki yetu leo natetea,

    Swali langu lisikike,msidhani nakosea,

    Watoto kuwanyanyasa,ni kosa au ni haki?

    Watoto wanateseka,kila pembe ya dunia.

    Wengine wanawacheka,kuwaona kwenye njia,

    Ni pengi wanawabaka,mabaya kuwatendea.

    Watoto kuwanyanyasa,ni kosa au ni haki?

    Watoto kuwaajiri,kazi ngumu kufanyia,

    Hamuoni ni hatari,shule kuwaharibia,

    Mambo hayo si mazuri,mabaya kuwatendea,

    Watoto kuwanyanyasa ,ni kosa au haki?

    Wengi wanawapiga,bila kosa kutokea,

    Utadhani wawapiga ng'ombe punda na ngamia,

    Kuwatesa wataaga,dunia kuiachia,

    Watoto kuwanyanyasa,ni kosa au ni haki?

    Wana wetu tuwatunze,wae wakifurahia

    Mambo mengi wajifunze,ya elimu na dunia,

    Kuwapenda na tuanze,wape haki asilia,

    Watoto kuwanyanyasa,ni kosa au ni haki?

    Tunakushukuru sana msikilizaji wetu Abdillahi Shabani kwa barua yako ambayo inasisimua kutokana na shairi zuri ambalo umeliandika, ni kweli watoto wengi wamekuwa wakinyanyaswa na kunyimwa haki zao za msingi kama kupata elimu, kucheza, kusikilizwa n.k lakini tujiulize nani ambaye anawatendea yote hayo, jibu ni sisi wazee, hivyo ni jukumu letu kuwalea kwa misingi mema na kuwapa haki zao zote na kubwa ni kuwapatia elimu kwani huo ndio muongozo wao wa maisha..


    1 2 3 4
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako