• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chuo cha Confucius chajenga daraja la urafiki kati ya wananchi wa China na Afrika

    (GMT+08:00) 2009-02-27 15:50:36

    Hivi sasa wakati mchina anapotembelea mitaani katika miji mikubwa barani Afrika, anaweza kusalimiwa na waafrika kwa lugha ya Kichina. Kutokana na kukuimarishwa kwa nguvu halisi ya China, na kuinuka kwa kiwango cha kufungua mlango kwa nje, waafrika wengi zaidi wanapenda kujifunza lugha ya Kichina na kuelewa utamaduni wa China, na chuo cha Confucius ni njia muhimu kwa waafrika kujifunza Kichina na kuelewa utamaduni wa China, ambapo urafiki kati ya wananchi wa China na Afrika umeongezwa zaidi.

    Katika chuo cha Confucius cha chuo kikuu cha Nairobi, wanafunzi walikuwa wanasoma makala ya Kichina darasani. Maana ya maneno waliyosoma ni "Anaitwa Ding Libo, baba yake ni mcanada, mama yake ni mchina, na yeye ni mcanada." Mwanafunzi aliyeongoza wenzake kusoma makala anaitwa Kennedy. Kennedy alisema, alianza kusoma kwenye chuo cha Confucius na kujifunza utamaduni wa China, ni kutokana na sababu rahisi. Alisema,

    "Sasa naanza kujifunza lugha ya Kichina katika chuo cha Confucius, kwa sababu naona kuwa ni ngumu kutafuta ajira nchini Kenya. Lakini kama unajua lugha za kigeni ikiwemo lugha ya Kichina, unaweza kufanya kazi katika kampuni za China. Nina matumaini kuwa nitapata fursa ya kusoma nchini China baada ya kuhitimu kutoka chuo hicho. Naona kuwa kama ninajua kuongea lugha ya Kichina, labda ni rahisi kuzungumza na watu wengine nchini China."

    Bw. Kennedy mwaka jana alishiriki kwenye mashindano ya "daraja la lugha ya Kichina" ya wanafunzi wa shule za sekondari duniani, na kupata fursa ya kupewa mafunzo ya lugha ya Kichina kwa muda mfupi nchini China.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako