• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utafiti kuhusu enzi ya kifalme yenye mambo mengi yasiyofahamika

    (GMT+08:00) 2009-03-02 17:46:57

    Mwanzoni mwa karne ya 11, enzi moja mpya ya kifalme ilinyanyuka kwenye sehemu ya kaskazini magharibi ya China ya hivi sasa, kwa muda fulani enzi hiyo ilizuia mashambulio ya magharibi ya jeshi kubwa la Mongolia, ambalo lilizikumba Ulaya na Asia hapo baadaye, mabaki adimu ya vitu vya utamduni yanayohifadhiwa hadi hivi sasa ni vitu vya mbao vilivyochongwa maneno ya Kichina na kutumika katika kuchapa vitabu (moveable type) pamoja na vitabu vya sheria za nchi. Watu wanaita enzi hiyo ya kifalme yenye mambo mengi yasiyofahamika kuwa ni "Xixia".

    Katika muda wa miaka 200 kati ya mwanzoni mwa karne ya 11 na mwanzoni mwa karne ya 13, Wadangxiang, ambao walikuwa wa tawi moja la kabila la Waqiang, waliasisi enzi ya kifalme ya Xixia kwenye sehemu ya kaskazini magharibi ya mkoa unaojiendesha wa kabila la Wahui wa Ningsha wa China ya hivi sasa, enzi hiyo ilikuwa na nguvu kubwa sawa na enzi nyingine mbili za Jin na Nansong zilizokuweko wakati ule nchini China, na iliendelea kwa miaka 200, hatimaye iliangamizwa na jeshi la Mongolia, na kuungananishwa na kabila la Wahan na makabila mengine ya nchini China.

    Watu wa Xixia walivumbua ustaarabu wa kiwango cha juu. Walibuni maandishi ya kipekee, teknolojia ya kimaendeleo, yote hayo yanadhihirishwa na vitabu pamoja na mabaki ya kiutamaduni na kihistoria. Hususan makaburi ya ukoo wa mfalme wa Xixia yaliyoko kwenye mashariki ya mlima Helan, kiunga cha magharibi cha mji wa Yinchuan, mji mkuu wa mkoa unaojiendesha wa kabila la Wahui wa Ningxia. Eneo la makaburi ni kiasi cha kilomita za mraba 53, ambapo makaburi 9 ya wafalme yalijengwa kwa utaratibu mzuri, pamoja na makaburi 253 ya watu waliouawa kwa ajili kuwahudumia wafalme baada ya vifo vyao. Eneo hili ni moja kati ya maeneo makubwa ya makaburi ya wafalme yaliyohifadhiwa vizuri nchini China, na kusifiwa kuwa ni "piramid ya mashariki".

    Mtafiti Niu Dasheng wa taasisi ya utafiti wa mabaki ya utamaduni ya enzi ya Xixia hadi hivi sasa bado anakumbuka sana jinsi alivyoshangazwa sana wakati alipoyaona makaburi ya wafalme wa Xixia mara ya kwanza. Alisema,

    "Nilipofika huko,niliona eneo lile ni kubwa sana, hali yake ni ya pori kabisa, lakini inaonekana ni lenye mambo mengi yasiyofahamika, kwani sehemu niliyoweza kuona ni ndogo sana ikilinganishwa na eneo lenyewe……"

    Vichuguu mia kadhaa vya udongo wa rangi ya manjano ilionekana kama vilima vidogo kwenye ardhi hiyo ya pori ya Mlima Helan. Ingawa vilima hivyo vya udongo vilipigwa na upepo na mvua katika miaka karibu elfu 1 iliyopita, na baadhi ya sehemu zake zimemomonyoka, lakini bado vipo.


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako