• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua za wasikilizaji 0303

    (GMT+08:00) 2009-03-03 17:02:26

    Msikilizaji wetu Gulam Haji Karimu wa sanduku la posta 504 Lindi Tanzania ametuletea barua akisema kuwa, anachukua nafasi hii kutoa salamu za mwaka mpya wa 2009. Kutokana na athari mbaya ya uchumi ulimwenguni, tunaitakia mafanikio kabla kumalizika tupate nafuu ya hali ya uchumi. Kwa kweli muda mrefu sijaandika barua kutokana na hali ya mazingira ya hapo nilipo hata kusikiliza ni kwa baadhi ya siku tu, sipati muda mzuri lakini najitahidi kufuatilia, tayari nimeshapokea masuali ya chemsha bongo kuhusu vivutio vya Sichuan najaribu kupata muda nisikilize mwaka wa 2009 uwe wa amani, ushirikiano na umoja. Pokea na nitolee salamu za kirafiki kwa wafanyakazi na watangazaji wote. Shukrani.

    Tunamshukuru sana Bw. Gulam Haji Karimu kwa barua yake, yeye kweli ni msikilizaji wetu tangu zamani ambaye ametufuatilia kwa miaka mingi, ingawa hana nafasi nyingi lakini bado anadumisha mawasiliano kati yetu, hii inatutia moyo sana, na tunamtakia kila la heri katika mwaka huu mpya wa 2009.

    Msikilizaji wetu Jim Godfrey Mwanyama wa Sanduku la posta 1097 Wundanyi Taita Kenya ametuletea barua akisema kuwa, watangazaji wote na watayarishaji wa vipindi vyote studioni pokeeni wingi wa salamu kutoka kwangu na mashabiki wangu nilio nao hapa kwetu Kenya hasa wale hutegea idhaa hii ya Kiswahili ya Radio China Kimataifa. Pongezi nyingi kwenu kwa kuendesha vipindi kwa njia mwafaka bila wasiwasi wowote, tunavipokea vyema sana bila matatizo tunawaomba muendelee na moyo huo huo wa kututumikia hasa upande wa salamu na habari motomoto kutoka duniani kote. Kwa hayo nawakia kazi nzuri.

    Tunamshukuru sana Bw. Jim Godfrey Mwanyama kwa barua yake ya kututia moyo na kutuhimiza tuendelee kuchapa kazi kwa ajili ya wasikilizaji wetu.

    Msikilizaji wetu Mutanda Ayub Shariff ametuletea barua pepe akitoa maoni yake mbalimbali. Anasema, ningependa kutumia fursa hii kutuma salamu zangu za dhati pamoja na za familia yangu kwa idhaa ya Kiswahili, wachina na wananchi wote wa China. Nikiwa na matumaini kuwa siku kuu ya mwaka mpya wa jadi imemalizika vyema na kwa sasa wafanyikazi wako katika pilipilika za kurejea kazini mwao.

    Wakati huu nina furaha kuwafahamisha kuwa Kipindi maalumu kuhusu wachina washerekea siku kuu ya mwaka mpya wa jadi kilitufikia vizuri sana. Huu ukiwa mwaka wa Ng'ombe vile tulivyofahamishwa kulingana na majina ya wanyama kumi na mbili. Hii ikiorodheshwa kulingana na kalenda ya kilimo ya China ikiwa na maana kuwa China ni nchi ya kilimo. Vilevile sina budi kuwafahamisha kuwa Wanafunzi wa Tanzania katika chuo kikuu cha Beijing Bw Ramadhan Mutoro, Bw.Emmauel Moses Onasaa pamoja na Bi Mwinyi. Habari iliyonifurahisha ni vile hawa wanafunzi wameweza kujifunza kichina na kufahamu mengi kuhusu desturi na utamatuni wa wachina pamoja na mila zao. Wakiwa watangazaji wa CRI tunaendelea kuwazoea polepole kwani wameonesha ujasiri wao na umaarufu katika njia hii ya utangazaji.


    1 2 3 4
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako