• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chakula kitamu cha Yinchuan

    (GMT+08:00) 2009-03-16 17:58:36

    Watu wengi waliofika mji wa Yinchuan ulioko sehemu ya kaskazini magharibi ya China, hisia zao huwa zinaweza kupita vipindi vinne vya "kuridhika, kusifu, kukumbuka na kujulisha" chakula kitamu cha huko. Yinchuan ni mji mkuu wa mkoa unaojiendesha wa kabila la Wahui wa Ningxia nchini China, chakula cha huko licha ya kuwa na umaalumu wa kiislamu, vilevile ni chenye sifa ya chakula cha kichina, kiwe chakula cha nyama au chakula cha unga wa ngano, kiwe chakula cha haraka au karamu, vyote ni vyenye ladha nzuri na vya kutimiza shauku.

    Tukitaja chakula kitamu cha Yinchuan, sina budi kuelezea nyama ya kondoo ya Ningxia. Kondoo wa Ningxia ni kondoo wa aina maalumu ya Tan. Kutokana na mazingira maalumu ya jiografia ya Ningxia, yaani "maji, majani, chumvi na magadi", nyama ya kondoo ya Tan ni laini, mbichi, bila kidusi na yenye ladha nzuri sana. Toka enzi ya Qing ya China ya zaidi ya miaka 200 iliyopita hadi sasa, wataalamu wa chakula wa vipindi mbalimbali wote wanasifu sana ladha nzuri ya nyama ya kondoo ya Ningxia. Hivi sasa, baadhi ya nchi za kiislamu za sehemu ya mashariki ya kati, zikiwemo Jordan na Umoja wa nchi za falme za kiarabu, zinaagiza kwa wingi nyama bora ya kondoo wa aina hiyo

    Yinchuan ikiwa ni mji mkuu wa mkoa wa kipekee unaojiendesha wa kabila la Wahui wa nchini China, chakula chake chenye sifa nzuri na kuvutia zaidi ni nyama ya kondoo iliyopikwa kwa mbinu mbalimbali, hususan aina ya chakula cha haraka kilichotengenezwa kwa viungo mbalimbali vya kondoo, ambacho wakazi wa huko wanakiita "Yangzasui". 20% ya wakazi wa Yinchuan huwa wanakula "Yangzasui" katika chakula cha asubuhi. Chakula cha "Yangzasui" ni viungo vya kondoo vilivyotiwa katika supu, vikichanganika na vipande vya chapati na tambi, na kutiwa vipande vidogo vya pilipili na vitunguu vya kijani. Msichana Zhao Zinan mwenye umri wa miaka 24 ni mwanafunzi wa chuo kikuu, akizungumzia "Yangzasui", alisema kwa furaha,

    "Yangzasui ya Ningxia inanukia vizuri, ambayo harufu yake inachochea shauku ya watu kutokana na nyama nzuri ya kondoo ya Ningxia, mafuta na pilipili, mtu akila hutokwa jasho jingi, na kutaka nyingine tena."

    Vitu vya "Yangzasui" ni nyama za sehemu nyingi za kondoo zikiwa ni pamoja na kichwa, makwato, maini, matumbo na damu. "Yangzasui" licha ya kuwa na ladha nzuri kinywani, pia ina uwezo wa dawa na kujenga mwili. Kwa mfano, maini ya kondoo yanaimarisha nguvu za ubongo na macho. Supu ya nyama inapikwa kwa viungo mbalimbali vya kondoo, ambayo ina harufu kali ya kuvutia, na nyama ni laini sana, tena bei yake ni rahisi, hizo ndizo sifa za "Yangzasui".

    "Yangzasui" ni chakula cha haraka kinachojulikana zaidi katika Ningxia, ambaco kilipata sifa ya kuitwa "chakula maarufu cha jadi cha kiislamu cha taifa". Ladha yake nzuri inahamasisha shauku ya washairi kutunga mashairi. Mkurugenzi wa idara ya utalii ya mkoa unaojiendesha wa kabila la Wahui wa Ningxia, Bw. Xue Gang ni mshairi mashuhuri katika sehemu ya kaskazini magharibi ya China, ambaye anapenda sana kula "Yangzasui". Kila anaposoma shairi lake liitwalo: "Yangzasui", anakuwa na hisia kubwa juu ya chakula hicho cha kwao katika maneno ya shairi.

    "Kunywa supu, washa! Kula viungo, tamu! Giligilani ya bakulini, kijani! Vitungu vilivyoelea, ng'ra! Wenyeji wa huko wanasema: inaweza kukatiza hamu; wageni wanasema: ni vigumu kusahauliwa!"

    Ikiwa tunasema "Yangzasui" inayopatikana kila mahali katika Ningxia kimekuwa sehemu moja ya maisha ya wakazi wa huko. Basi nyama ya ndama ya kondoo inayokaangwa kwa moto mkubwa ni chakula kingine chenye sifa kubwa.

    Vipande vikubwa vya nyama ya kondoo ya kahawia, tambi zilizoiva sawia, vipande vya figili ya rangi ya kijani kibichi, supu nzito ya rangi nyekundu, na harufu ya nyama tamu ikichanganyika na ya mafuta inagonga pua……..nyama ya ndama wa kondoo iliyokaangwa ikiwa na ukakamavu wa kipekee wa sehemu ya kaskazini magharibi ya China, takriban imekuwa chakula kinachopendwa zaidi na wakazi wa Ningxia, na ni chakula kinachochaguliwa kwanza kwa kukirimu mgeni. Bw. Duan Guohai mwenye umri wa zaidi ya miaka 40, alieleza kwa furaha sifa za kitoweo hicho akisema:

    "Wakazi wengi wa Yinchuan wanapenda kula nyama ya ndama wa kondoo, kutokana na ulaini wake. Nyama hiyo hukaangwa na pilipili kali ili kuondoa kidusi. Nyama hiyo ikitiwa unga wa maharage, itapendeza zaidi iwe kwa rangi na ladha yake. Watu wengi wakipata wageni, wanawachukua kula kitoweo hicho katika mikahawa, au wanawenda mikahawa wao wenyewe katika siku za mwisho wa wiki.

    Nyama ya kondoo ya Ningxia ni nzuri ya kipekee, ikipikwa kwa mapishi ya jadi yaliyoendelea kwa zaidi ya miaka 100, nyama ya kitoweo hiki ina ladha ya nyama ya kuku, tena ni laini kama nyama ya sungura.

    Mbali na vitoweo vilivyopikwa kwa nyama ya kondoo, katika Yinchuan, mji mkuu wa mkoa unaojiendesha wa kabila la Wahui wa Ningxia, kuna vyakula vya aina mbalimbali vinavyotengenezwa kwa unga wa ngano. Hususan ni "Youxiang", chakula kinachoonekana kimeungua kidogo juujuu, lakini ndani yake ni laini.

    Inasemekana kuwa "Youxiang" ni chakula kilichoanzishwa na mwanzilishi wa dini ya kiislamu, mtume Muhammad, iliingia nchini China zaidi ya miaka 700 iliyopita. Hadi sasa, waislamu wa nchini China hutumia chakula hicho iwe katika sherehe na kuwakaribisha wageni, au katika ndoa, mazishi. Msichana Zhao Jing, ambaye ni mkazi wa Yinchuan alisema,

    "Chakula hicho ni kitamu sana, kikitiwa kinywani kinaonekana ni laini sana. Chakula hiki hakiharibiki hata kikiwekwa kwa nusu mwezi, tena kingali bado ni laini."

    Dada Zhao Jing alisema, aina mbalimbali za keki na "Shanzi" ni sehemu moja ya chakula cha "Youxiang".

    "Chakula cha Youxiang cha Ningxia licha ya keki na Shanzi, kuna Huahua, ambayo unga unapokandwa ukitiwa maji, unaongezwa sukari guru na sukari nyeupe, hivyo baada ya Huahua kutengenezwa tayari, huwa na rangi mbili nyeusi na nyeupe na kuwa na maumbo ya vipepeo na wanyama mbalimbali".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako