• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua za wasikilizaji 0310

    (GMT+08:00) 2009-03-17 19:03:48

    Hivi sasa mikutano miwili ya mwaka ya Bunge la umma la China na Baraza la mashauriano ya kisiasa inafanyika hapa Beijing. Kabla ya kufanyika kwa mikutano hiyo miwili, tuliwatumia barua pepe wasomaji wetu kwenye tovuti ya mtandao wa internet kuhusu masuala wanayofuatilia. Msikilizaji wetu mmoja alitutumia barua pepe akitaka kuelewa namna China inavyokabiliana na msukosuko wa fedha duniani, mwandishi wetu wa habari anayekusanya habari kwenye mkutano amemhoji naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wu Dawei tarehe 6, ambapo Bw. Wu alisema, msukosuko wa fedha duniani umeathiri uchumi wa dunia nzima, ambapo nchi zilizoendelea na nchi zinazoendelea zote zimeathiriwa vibaya, na msukosuko huo ni changamoto kubwa zinazotukabili. Anaona kuwa watu wa kila kizazi wanapambana na matatizo, tusiwe na hofu, kwani hauwezi kuepukika, njia pekee kwetu ni kuwa na moyo wa kushinda matatizo hayo. Kushinda tatizo moja, kuvuka kikwazo kimoja, sisi binadamu tukapiga hatua moja ya kusonga mbele.

    Bw. Wu amesema, kwa wachina, mambo muhimu ni kufanya vizuri shughuli za China kwanza. Katika miaka 30 baada ya mageuzi na ufunguaji mlango wa nchi yetu, watu wamekuwa na uzoefu mwingi, na msingi wa uchumi wetu umepata mabadiliko makubwa, zamani wananchi walikuwa nyuma katika uchumi, hivi sasa uchumi wa nchi yetu kwa ujumla umechukua nafasi ya tatu duniani, na bila shaka baada ya miaka kadhaa utakuwa wa pili. Kwa hivyo, lazima wananchi wajipe moyo na kufanya vizuri mambo yetu. Uchumi wa China ukitulia na kuweza kupata maendeleo kwa kasi kiasi na utulivu, utaweza kuisaidia dunia ijikwamue kiuchumi. Hali kadhalika, tunapaswa kushiriki kwenye ushirikiano wa kimataifa, na kufanya juhudi za pamoja katika kukabiliana na msukosuko wa fedha duniani.

    Ameongeza kuwa, mkutano wa wakuu wa nchi ishirini utafanyika mwanzoni mwa mwezi Aprili, ambao utajadili suala la msukosuko wa fedha, inatubidi tufanye ushirikiano wa pande mbalimbali za kimataifa ili kuhimiza mchakato wa kukomesha msukosuko wa fedha duniani. Hivyo, kutilia mkazo maendeleo ya uchumi wa nchini na kukabiliana na msukosuko wa fedha ni kazi moja muhimu kwa wizara ya mambo ya nje ya China. Wizara hiyo inatakiwa kufanya mambo mengi, hususani katika ubalozi wa China katika nchi za nje.


    1 2 3 4
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako