• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua za wasikilizaji 0323

    (GMT+08:00) 2009-03-24 15:39:53

    Msikilizaji wetu Moses Kipkesis Kiboi wa sanduku la posta 5 Cheptais Kenya ametuletea shairi likisema hivi:

    Radio China Kimataifa, idhaa ya hidaya

    Toka Asia-uchina, mataifa kutumikia

    Mengi kututangazia, vivutio vya Beijing

    Taarifa itatujuvya, toka Asia hadi Afrika

    Bara Hindi hadi Ulaya na pia America

    Mengi kututangazia, vivutio vya Sichuani

    Walimwengu tukafahamu, mkoa wa Sichuani

    Kwa utalii ni muhimu, namba wani ulimwenguni

    Mengi kututangazia, vivutio vya Jiuzhaigou

    Mesheheni elimu, watu kuwatalamisha

    Historia na unajimu, wa wanasichuan kufahamisha

    Mengi kututangazia, vivutio vya Jiuzhaigou

    Tamati ndiyo akhiri, nilonena mwabaini

    Radio China Kimataifa, hutufunza makini

    Wasiojua wajue, Kichina na Kiswahili

    Mengi kututangazia, vivutio vya mto Changjiang

    Tunamshukuru kwa dhati Bw. Moses Kipkesis Kiboi kwa shairi lake la kuelezea maoni yake baada ya kushiriki kwenye chemsha bongo kuhusu vivutio vya Mkoa wa Sichuan, asante sana.

    Msikilizaji wetu Paul Mungai Mwangi wa sanduku la posta 69 Injinia Northi Kinangop Kenya ametuletea barua akisema kuwa, kwanza nataka kuwasalimia wafanyakazi na wasikilizaji wa Radio China kimataifa. Ni matumaini yangu kuwa nyote hamjambo.

    Maelezo yaliyotolewa na watangazaji wetu Chen pamoja na Pili Mwinyi na Emanuel Moses kuhusu mkesha wa siku kuu ya mwaka mpya wa jadi wa China yalikuwa ya kusisimua sana. Hadithi tamu aliyosimulia Moses kuelezea asili ya mila ya kukesha na kupiga fataki usiku wa kuamkia sikukuu ya Spring pia ilisisimua.

    Utamaduni huu ulioanza miaka 2000 iliyopita hudhihirisha umuhimu wanaotilia wachina kwa shughuli za kilimo. Wachina wote huikaribisha sikukuu hii kwa shamrashamra nyingi ambazo ni pamoja na kubandika karatasi nyekundu zenye maandishi yenye maneno ya baraka kwenye pande mbili za milango. Kila familia hujawa na furaha na upendo kuonesha matumaini na matarajio juu ya mwaka mpya wa jadi wa China kwa kalenda ya kilimo ya Chin. Chakula wanachokula kabla ya alfajiri ya sikukuu hii huwaletea baraka za Spring. Nawatakia wachina wote mwaka wa ng'ombe wa 2009 wenye mafanikio katika shughuli zao za kilimo.

    Na mwisho nataka kuwasalimia wafuatao:

    Peter Mwangi Mungai na mkewe Wairimu walioko Mombasa Kenya, Patrick Ndugi Mungai na mkewe Hellen Mwiyeria wa Kahawa Garrison, Isaac Gichimu Mungai na mkewe Wangari walioko Injinia Kenya, watoto kariuki na Patience wa Injinia, Joyce Waithera Mungai wa Injinia, Esther Njeri ambaye ni mwalimu wa shule ya Mwiteithia, Injinia Kenya na Bramwel Sirali wa Kitale Kenya.

    Shukrani sana Bw. Paul Mungai Mwangi kwa barua yako inayoeleza jinsi ulivyofurahia mfululizo wa vipindi vyetu maalumu vya mwaka mpya wa jadi wa China, ingawa muda umepita toka sherehe hiyo kumalizika lakini kwa niaba ya wachina wote tunasema ahsante kwa kututakia heri ya mwaka mpya wa jadi wa China.

    Msikilizaji wetu Kilulu Kulwa Sanduku la Posta 161 Bariadi Shinyanga Tanzania ametuletea barua akisema, Wapendwa Marafiki, wafanyakazi wa Radio China Kimataifa, salamu nyingi ziwafikie kutoka hapa Tanzania. Kama inavyofahamika Mwezi Februari mwaka huu wa 2009, siku chache mara baada ya sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China ambayo huwa ni sherehe kubwa inayoambatana na shamrashamra nyingi za kuvutia na kuburudisha sana. Rais Hu Jintao wa China alizuru Saudi Arabia, Mali, Senegal, Tanzania na Mauritious. Ambapo kulingana na ripoti za waandishi wa habari, ziara hiyo imepata mafanikio makubwa sana katika nchi zote alizozuru mheshimiwa Rais Hu Jintao na ujumbe wake.

    Nikirejea Tanzania sijui nitumie maneno, misemo au msamiati gani kueleza furaha kubwa na matumaini yangu na ya watanzania wenzangu kuhusiana na ziara aliyoifanya Rais wa Jamhuri ya Watu wa China mstahiki Hu Jintao. Ni maneno gani mazuri na muafaka ninayoweza kutumia kuwasilisha ama kuwakilisha furaha yangu kubwa kwa ajili ya ugeni huo mzito uliofanywa na Rais Hu Jintao nchini Tanzania. Hakika tumefurahi sana na tunamshukuru sana Rais Hu Jintao pamoja na mwenyeji wake mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania kuwa mambo mengi waliyofanya kwa manufaa ya wananchi wa mataifa haya mawili. Tumeweza kuona na kushuhudia misaada mingi ya hali na mali na ushirikiano mkubwa hadi sasa tangu kuanzishwa uhusiano baina ya Jamhuri ya Watu wa China na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

    Uhusiano na ushirikiano huu wenye takribani miaka 45 sasa, umezaa matunda mengi na kuleta matokeo mazuri na mema yanayojionesha wazi hata kujenga imani kubwa isiyoelezeka baina ya wananchi wa pande zote mbili. Aidha ziara hii ya Rais Hu Jintao ambayo ni ya kihistoria katika nchi yetu, pamoja na kuhuisha na kudumisha ushirikiano huo wa enzi na enzi lakini pia imefungua ukurasa mpya na kipindi kipya kabisa cha kuungana mkono baina ya China na Tanzania. Vilevile imeongeza kasi ya kujenga ushusiano na undugu wa wananchi wa pande hizi mbili.

    Mimi sikuwepo Dar es Salaam wakati Rais Hu Jintao alipotua na kuwasili mjini Dar es Salaam Tanzania, lakini vyombo vya habari vya Radio na Televisheni nchini Tanzania na pia Radio China Kimataifa vilitutangazia kwa ukamilifu na uhakika ziara ya Rais Hu Jintao wa China barani Afrika. Watanzania wana msemo na wanaamini kuwa kaya au familia inapofikiwa au kutembelewa na mgeni au wageni hupata baraka kutoka kwa mwenyezi Mungu, kwa mantiki hii, kutembelewa na mgeni huyu mashuhuri Rais Hu Jintao bila ya shaka nchi yetu na watu wake wataendelea kupata baraka, mafanikio na heri nyingi katika awamu mbalimbali vizazi na vizazi, na hata karne na karne.

    Tutaienzi na kuitunza vizuri kazi kubwa yenye thamani iliyoasisiwa na viongozi wetu waliotangulia ambao walijitahidi sana kujenga msingi imara ulioleta matunda na mafanikio mengi ambayo tunayaona na kuyashuhudia leo. Kwa mara nyingine tena tunamshukuru sana Rais Hu Jintao pamoja na ujumbe wake wote na wananchi wote wa China kwa mikakati na juhudi zake kubwa katika diplomasia ya kimataifa ya China.

    Tunafarijika mno na kuona kuwa Jamhuri ya Watu wa China ni mshirika na mdau mkubwa kabisa katika ustawi na maendeleo ya Tanzania bara na Zanzibar na Afrika nzima kwa ujumla. Tunashukuru sana na asante.

    Bw. Kilulu Kulwa amesema katika barua yake nyingine kuwa, Wapendwa marafiki, wahariri na watangazaji wa idhaa ya kiswahili ya CRI, bila shaka hamjambo sana na mnaendelea vyema na shughuli za kutuhudumia sisi wasikilizaji wenu kwa kutupasha na kutuhabarisha vipindi mbalimbali vinavyoandaliwa na idhaa ya kiswahili ya radio china kimataifa.

    Wapendwa marafiki nilikuwa najiandaa kuwaandikia makala maalum kuhusu mwaka wa ng'ombe wa china,kama mlivyotusimulia katika vipindi vyenu mwanzoni mwa mwaka kuhusu mwaka huu wa 2009 kuwa ni mwaka wa ng'ombe kwa kalenda na utaratibu wa marafiki zetu wachina, mimi binafsi nilivutiwa sana ndio maana nilitarajia kuandika makala maridhawa kuhusu jambo hilo.

    Lakini wakati najiweka sawa kufanya hivyo,basi nikasikia kuwa rais Hu Jintao wa China amewasili Tanzania,nikajawa na furaha nyingi na kuamua kuandika makala kueleza hisia na maoni yangu kuhusu ziara hiyo murua ya rais wa china hasa kwa kuzingatia kwamba China na Tanzania zimekuwa na urafiki wa jadi ambao umedumu miaka mingi.Makala hiyo ambayo ni ndefu kidogo ninaituma pamoja na barua hii,nitafurahi kama mtaamua kuifanyia kazi.Kama vile kuitafsiri kwa lugha ya kichina na kuiwakilisha kwa wahariri wa gazeti la wasikilizaji wa CRI linalochapishwa kwa kichina au gazeti lolote muhimu la China kama vile Daily China, The messenger(CRI) nakadhalika, mnaweza kuitumia kwa hali yoyote mnayoona inafaa, nadhani ni suala zuri tu,ninawatakia mafanikio mema.

    Wapendwa marafiki tutaendelea kuwasiliana na kushirikiana kwa moyo wa kindugu na kirafiki zaidi.Ninawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayoifanya ambayo inatuvutia na kutuchangamsha sana.Ahsanteni sana

    Tunakushukuru sana Bw. Kilulu Kulwa kwa barua zako maridhawa ulizotutumia, kwa kweli tumefurahishwa sana na barua zako zinazogusia ziara ya rais Hu Jintao nchini Tanzania. Nchi hizi mbili zina urafiki mkubwa ulioanzia tangu enzi na dahari, hivyo hatuna budi kuuenzi na kuundeleza, kuna methali isemayo urafiki unashinda undugu kwa hiyo hivi sasa nchi hizi ziko zaidi ya ndugu kwa kusaidiana na kuungana mkono pale linapotokea tatizo, na hili limejidhihirisha wazi kwani rais Hu kwenye ziara nchini humo aliahidi kuisaidia Tanzania hata kama dunia hivi sasa imekabiliwa na msukosuko wa fedha na hata Tanzania nayo ilikuwa mbele kuisaidia China pale ilipokumbwa na maafa ya tetemeko la ardhi lilotokea mwaka jana huko Sichuan. Kwa hiyo si watanzania pekee ambao wanafurahia ziara hiyo bali hata wachina pia. Na kuhusu makala yako uliyoitayarisha usijali tutaifanyia kazi.

    Shule mbili za vijijini zasaidia kutimiza uwiano kati ya mambo ya elimu mijini na vijijini

    Mkutano wa pili wa mwaka 2009 wa Bunge la 11 la umma la China ulifungwa hapa Beijing hivi karibuni. Kwenye mkutano huo, waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao alipotoa ripoti ya kazi ya serikali alisema kuhimiza uwiano wa elimu na kutomfanya hata mtoto mmoja aache shule kutokana na matatizo ya kiuchumi ya familia yake kumekuwa jukumu kuu la kuendeleza mambo ya elimu. Mkoa unaojiendesha wa kabila la Wahui la Ningxia wakati unapoeneza elimu ya lazima ya shule ya msingi na ya sekondari, pia umejenga shule ya sekondari ya juu ya Liupanshui na Shule ya sekondari ya Yucai huko Yinchuan, ambazo zinapunguza ada za shule na kutoa elimu bora kwa wanafunzi hodari kutoka familia zenye matatizo ya kiuchumi katika sehemu za milima na vijiji, ambapo umepiga hatua nyingine katika njia ya kuhimiza uwiano wa elimu.

    Xihaigu ni sehemu moja ya milima yenye ardhi kame iliyoko kusini mwa mkoa wa Ningxia, huko kuna milima na mabonde makubwa, na mara kwa mara kunakumbwa na maafa ya ukame, hali ya mazingira ya asili ni mbaya sana. Aidha, miundombinu ya mawasiliano na upashanaji habari ya sehemu hiyo ni hafifu sana, na sehemu hiyo iko nyuma kiuchumi na kimaendeleo, hata ilithibitishwa na Umoja wa Mataifa kuwa ni "sehemu isiyofaa kwa maisha ya binadamu". Ingawa kutokana na uungaji mkono wa kifedha wa serikali, kiwango cha maisha ya wakazi wa huko kimeboreka kidhahiri, lakini kama sehemu hiyo inataka kuondokana na umaskini, inapaswa kutilia maanani kuendeleza mambo ya elimu. Mjumbe wa bunge la umma la China ambaye ni katibu wa kamati ya chama cha kikomunisti ya mkoa unaojiendesha wa Ningxia Bw. Chen Jianguo alisema, sehemu hiyo itaweza kupata maendeleo na kuondokana kabisa na umaskini endapo itawapatia fursa ya elimu watoto wa sehemu za milimani sawasawa na watoto wa mijini. Bw. Chen Jianguo alisema:

    Sauti 1

    "misaada iliyotolewa kwa sehemu ya kusini ya milimani inaweza kutatua kwa muda tatizo la chakula na mavazi la wakazi wa huko, lakini haitaweza kutatua suala la maendeleo ya siku zijazo. Tunaweka mkazo katika kuendeleza mambo ya elimu, na kuwapatia fursa watoto wa sehemu za milima za kusini kupata elimu bora, ili waweze kwenda sehemu nyingine kujiendeleza na kubadilisha maisha yao, na kubadilisha hali ya maisha ya familia zao, baadaye kupunguza umaskini wa sehemu hiyo."

    Ndiyo kutokana na wazo hilo, mkoa wa Ningxia ulijenga shule hizo mbili mwaka 2003 na 2005 mjini Yinchuan. Mbali na kufuta ada za masomo na za kulipia mabweni, mkoa huo pia unatoa msaada wa yuan elfu moja kwa kila mwanafunzi wa kijijini kila mwaka. Mpaka sasa shule hizo mbili kwa jumla zimeandikisha wanafunzi zaidi ya elfu 10 kutoka sehemu ya kusini ya milimani, ambapo asilimia 40 ya wanafunzi hao ni wa kabila la wahui.

    Tatizo kubwa kabisa linalozikabili mambo ya elimu ya sehemu maskini ni upungufu wa walimu, lakini shule za Liupanshan na za Yucai zimetumia raslimali bora za mji wa Yinchuan na zimevutia walimu wengi hodari ili kuhakikisha watoto wa milimani wanapewa pia elimu bora. Mjumbe wa Bunge la umma la China ambaye ni mkurugenzi wa idara ya mambo ya fedha ya mkoa wa Ningxia Bw. Wang Heshan alisema:

    Sauti 4

    "walimu wengi vijana walikwenda vijijini, lakini kwa miaka mingi bado hawajatatua suala la ndoa, huduma mbalimbali za maisha ikiwemo nyumba bado zina pengo na zile za mijini, hali hii pia imewafanya wasiweze kufundisha kwa utulivu vijijini. Baadhi yao waliondoka baada ya kufundisha kwa muda mfupi tu, hali hiyo pia imeathiri masomo ya watoto. Kwa hiyo tukajenga shule za sekondari ya juu mjini Yinchuan, kwa upande mmoja suala la walimu likatatuliwa, kwa upande mwingine ni kwa ajili ya masomo ya watoto."

    Walimu hodari, miundombinu ya kisasa ya ufundishaji na wanafunzi wenye bidii, yote hayo yamefanya wanafunzi wa shule hizo mbili wajitokeze haraka kwenye mkoa huo. Mwaka 2006 wanafunzi 414 kati ya 604 wa shule ya Liupanshan waliandikishwa na vyuo vikuu, na wanafunzi 243 kati yao waliendelea na masomo katika vyuo vikuu muhimu.

    Mafanikio ya shule hizo yamejulikana kote mkoani Ningxia, wazazi wa watoto wengi wana matumaini kuwa watoto wao wataweza kujiunga na shule hizo mbili. Bw. Yang Xueli ni mkulima wa wilaya ya Yanchi ya mji wa Wuzhong, mwaka jana mwanawe alifanikiwa kujiunga shule ya sekondari ya Liupanshan, na binti yake sasa bado anasoma katika darasa la tisa. Alisema:

    Sauti 5

    "binti yangu alisema yeye pia ana matumaini ya kusoma katika shule hii, nafurahi sana fursa hii iliyotolewa na serikali yetu kwa watoto wangu."

    Kwa mujibu wa takwimu husika, toka shule hiyo ianzishwe hadi sasa, kwa kusaidiwa na serikali kuu ya China mkoa wa Ningxia umewekeza zaidi ya yuan milioni 600 kuendeleza shule hizo mbili. Hivi sasa shule ya sekondari ya juu ya Liupanshan ina wanafunzi elfu sita, shule ya Yucai ina wanafunzi elfu kumi.

    Katibu wa kamati ya chama cha mkoa huo Bw. Chen Jianguo alisema, mbinu hii ya kuendeleza mambo ya elimu ya sehemu zilizoko nyuma kiuchumi kwa kutegemea raslimali bora za miji imepata mafanikio. Katika siku za baadaye, mkoa wa Ningxia utatumia mbinu hiyo kujenga shule nyingi mijini kwa ajili ya watoto kutoka sehemu za milimani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako