• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua za wasikilizaji

    (GMT+08:00) 2009-03-31 15:59:27
    Kwanza tunawaletea barua tulizotumiwa na wasikililzaji wetu.

    Msikilizaji wetu Eveready Security Guardy wa sanduku la posta 57333 Nairobi Kenya ametuandikia barua kueleza maoni yake juu ya vipindi vyetu akisema, katika pilikapilika zangu za ufuatiliaji na usikivu wa matangazo ya Radio China Kiamtaifa kila mara, huwa napenda sana kufuatilia vipindi vya mazungumzo kuhusu vivutio maalum nchini China haswa vilivyoko mjini Beijing. Beijing ni mojawapo ya miji mashuhuri sana nchini China. Hata hivyo kuna waimbaji wengi walioimba nyimbo nyingi zinazoeleza mandhari na maumbile mazuri ya mjini Beijing. Beijing ni mahali ambapo kunapatikana mambo mengi ya kihistoria, kwa mfano kuna vichochoro mjini Beijing, kuna ukuta mkuu na vilele kuna kasiri za majira ya joto yaani Summar Palace, kulingana na historia na kuwa ukuta mkuu unapatikana mjini Beijing na umetambaa kutoka mashariki hadi magharibi mwa Beijing. Wachina wanasema kuwa ukuta mkuu ni fahari ya taifa la China na pia ni kivutio cha maumbile chenye ustadi maalumu.

    Anasema, siyo hayo tu pia ni kama mgongo wa China na kwa dunia unaonesha moyo wa China moja, akili na nguvu kazi nyingi zilitumika kwa ujenzi wa ukuta mkuu, eneo la ukuta mkuu wote ni wa kijani kibichi yaani kuna miti mingi pamoja na nyasi. Na inasemekana kuwa ukuta mkuu umejengwa kwenye matofali ya udongo uliochomwa wenye kustahamili upepo na mvua. Katika historia ya dunia, ukuta mkuu wa China umeorodheshwa kuwa moja wapo ya mali ya urithi duniani. Kuna msemo wa kichina usemao kuwa sio shujaa bila kufika kwenye ukuta mkuu. Naamini kuwa Mama Chen siku moja iwapo nitafanikiwa kufika Beijing, China, unipeleke kwenye ukuta mkuu ili nihesabiwe kuwa nimefika Beijing China. Mwisho matangazo ya CRI kwa kila upande nayafuatilia kwa kasi sana.

    Tunakushukuru sana msikilizaji wetu kwa barua yako yenye maoni kuhusu jinsi unavyofuatilia vipindi vyetu na ulivyovutiwa zaidi na ukuta mkuu wa Beujing, sisi tunakukaribisha kwa mikono miwili na ukifika Beijing bila shaka tutakupeleka kutembelea ukuta mkuu wa Beijing.

    Barua inatoka kwa msikilizaji wetu ,Emmanuel Meng'anyi Mseti wa Nyaibara Sec School, sanduku la barua 376,Tarime Tanzania.Anaanza kwa kusema, salaamu zangu za dhati ziwafikie enyi wahusika na ninawaombeni mzipokee kwa mikono miwili.Mimi hapa ni mzima wa afya njema kama kigongo,hofu na mashaka ni kwenu watanagzaji wa idhaa ya kiswahili ya Rado china kimataifa,Je hamjambo?

    Jisikieni kama mko kwenye hekaya ya mwenyezi mungu, kwani bila nyie mitamaboni sisi hatupo katika usikilizaji.

    Dhumuni la barua hii ni kuwafahamisha kuwa mimi hapa nilipo, katika upande wa usikilizaji ni makini sana, ila katika upande wa kutuma salaamu ninayo hitilafu kubwa. Nalazimika kusema hivyo kwa sababu mnanisababishia kushikwa na upweke pale ninapowasikiliza washabiki wenzangu wanawasalimia wapendwa wao, lakni mimi inakuwa kikwazo kwa kufanya hivyo.

    Mimi sina uwezo ila uwezo mnao nyie, ombi langu ni kuwa mbona hamnitumii kadi za salamu? Najihisi kubaguliwa pale ninapokosa kadi za salaamu kutoka mtambo mkubwa wa dunia China Swahili service-25, wapendwa nawaombeni kadi kwa wingi. kwani wahenga walinena ya kwamba salamu ni nusu ya kuonana. Nami najisikia kuwa nipo juu ya hii dunia pale ninaposikiliza kipindi cha salamu zetu.

    Mungu awajalie katika kazi njema na nzito.Ila inahitajika bidii na moyo katika kutekeleza.Jipeni moyo enyi watangazaji wetu wapendwa kwani nyie ndio nguvu yetu.Tunafurahi tunapowasikia muwazima mukisikika mitamboni tunawajali, tunawapenda na tunawatakia maisha mema na msituache mbali hasa sisi wanafunzi watanzania.

    Ahsante sana msikilizaji wetu Emmanuel Meng'anyi Mseti kwa masikitiko yako nasi tunasema tumesikia kilio chako ila tunakuomba uvute subira kidogo tutakutumia kadi ili umalize kiu yako.

    Barua inatoka kwa msikilizaji wetu .Paul Mungai Mwangi,wa sanduku la barua 69 Injini-north Kinangop-Kenya.

    Anaanza salamu zake kwa kusema,natuma salamu za dhati wa moyo wangu ziwafikie watangazaji na wafanyakazi wote wa idhaa ya kiswahili ya CRI. Aidha nisingeweza kuwasahau wasikilizaji wenzangu ambao pamoja na watangazaji na wafanyakzi wengine wa idhaa hii, sote ni wana wa jamii moja pana ya rado china kimataifa. Hongereni nyote kwa undugu huo na ni matumaini yangu kuwa uhusiano huu utadumu milele na kuzaa matunda mema.

    Napenda kuchukua fursa hii kutoa maoni na mapendekezo yangu kuhusu nyakati zilizoratibiwa vipindi vya idhaa ya kiswahili ya Radio China Kimataifa. Kwa maoni yangu saa nne hadi saa tano za usiku kwa kweli ni usiku sana na kwamba wasikilizaji wengie huwa wamelaa wakati huo. Ningependa kupendekeza kwamba nyakati hizo zibadilishwe na kuwa saa kumi na moja mpaka kumi na mbili za jioni kama ilivyokuwa hapo awali. Pendekezo jingine ni saa mbili hadi saa tatu za usiku.

    Mwisho naishukuru Radio China kimataifa kwa mashindano ya chemsha bongo kuhusu ujuzi wa vivutio vya utalii mkoani Guanxi, China amabayo kamati ya uthibitishaji ilinichagua kama mmojawapo wa washindi wa nafasi ya pili. Niliifurahia sana zawadi na cheti mlizoniletea kwa ushindi huo, hata hivyo nitafurahi zaidi siku nitakayoshinda nafasi maalum ili niweze kupata nafasi ya kutembelea China.Nina matumaini makubwa kuwa nitapata nafasi hiyo baada ya kushinda chemsha bongo kuhusu "vivutio vya Sichuan".

    Tunakushukuru sana Paul Mungai Mwangi, kwa maoni yako kuhusu muda wa vipindi vyetu kwa kweli suala hilo tumelipokea kwani pia lilitolewa maoni na wengi na tumeshaanza kulishughulikia hivyo usiwe na wasiwasi.

    Msikilizaji wetu Thabiti Muge Mangango Voice Of Africa 93.5 Kigali

    Idhaa hii inajitahidi sana kwa habari mpya. Lakini habari za michezo haziendi na wakati. Nafikiri tunaweza tukawasaidia mkihitaji. kwa sababu mi ni mwandishi wa habari na mtangazaji. Ninakuwa na habari nyingi mpya za michezo n.k.Tuwasiliane basi!

    Ahsante sana Thabit Muge kwa barua yako, ila tutakapo hitaji msaada wako tutakuambia.

    Msikilizaji kutoka Itangishaka Alain pascal itangishaka2003@ yahoo.com ameacha ujumbe wake kwenye tovuti yetu ya mtandao wa internet akisema, mimi mwanafunzi wa chuo kikuu cha BURUNDI, mjumbe wa club ya kujifunza lugha la kiswahili hapa chuoni. Nilipogundua uwanja huu wa habari kadhaa, nilifurahi sana. Pongezi kwenu ninyi nyote wafanyakazi wa CRI. Wachina munajitahidi na juhudi munazo ili muboreshe ulimwengu.

    eunadema@yahoo.com eunice adema manyengo, s.l.p 225, kitale Kenya kwanza ni salamu zangu ziwafikie wafanyikazi na watangazaji wa cri nchini china,nawapongeza kwa kazi nzuri munayofanya, pia nashukuru kwa zawadi muliyonitumia zawadi hii imevutia wengi sana nimeiweka ukutani.

    Nilifurahi nilipopata zawadi hata imefanya wengi kutamani nao pia wapate zawadi kama hiyo kwenye ploti ninayo ishi nimepewa heshima kutokana na zawadi kutoka china. ila ningeomba munitumie kitabu cha kujifunza lugha ya china na kitabu cha picha za vyakula vya kichina mukinitumia nitafurahi sana mwisho napenda salamu zangu ziwafikie wafuatao--mume wangu mpendwa osborne manyengo, Mike Wanga Oranga, Meshack Kilao Litembeko wote wakiwa maize gardens Kitale Kenya. mama na babangu Joseph Lanya na Ronicah Wambui Lanya wakiwa Shivagala idakho kakamega Kenya.ujumbe mashabiki tuendelee kusikiliza radio china kimataifa.

    Juma M Magimba,box 2122 Tr-Lib jumamagimba2001@yahoo.com

    Kwa Mhe.Mhusika,kwa kweli sina maoni, ila ninatoa shukrani kwa kazi ngumu na muhimu muifanyayo ya kuelimisha jamii. Naomba uanachama na cd mbalimbali zenu, hasa za video, zikiwemo za michezo ya redio, ili kufarijika zaidi na juhudi zenu. Mwisho natoa shukrani kwa ushirikiano mwema, huku nikiomba msamaha kwa usumbufu.

    lenusi kingalu"

    lenusi kingalu wa slp 24 new muungano salam club- morogoro tanzania.

    Katika matangazo ya tarehe 25 /2/09 nimesikia kuwa jamii ya watibeti siku hii kwao ndiyo wanasherehekea siku kuu ya mwaka mpya, je ina maana kuwa wao kalenda yao ni tofauti na ya dunia nzima? kwani dunia nzima sherehe ya mwaka mpya ni tarehe 1/1!

    Pili kuhusu kujiunga na Kenya inaonyesha wazi ni namna gani mna kiu ya kutufikishia huduma ya usikivu wasikilizaji wenu kwa mapana ili kuondoa usumbufu kwa wale wanaoona ni ngumu kutafuta idhaa hii,

    nawatakia kazi njema na salamu nyigi kwenu, kisha kwa wasikilizaji woote wa idhaa hii bora yenye matangazo yakinifu

    Selemani Mkonje smkonje@yahoo.com nashukuru leo ndio nimeikumbuka anuani ya radio china kwa sababu huku niliko hakuna mawimbi ya radio china. lakini sasa tutakuwa bega kwa bega katika kuimarisha uhusiano wetu wachina na watanzania kupitia maboresho ambayo tutayapata kupitia maoni mbali mbali. Asante sana. ni mimi seleman mkonje wa chuo cha ualimu mpuguso MBEYA TANZANIA.

    Mwangi Peter Nderitu mwapende@gmail.com anasema katika ujumbe wake kwenye tovuti yetu ya mtandao wa internet kuwa, natumai hamjambo. Mie ni Mwangi Peter Nderitu, mwanamume raia wa Kenya. Napenda kuwapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kutupasha habari za kuaminika za kila siku. Mie ni msikilizaji shupavu wa matangazo yenu kupitia idhaa ya Kiswahili ya Kenya (KBC)

    MILTONE OSES P.O.BOX 40439 DAR ES SALAAM, TANZANIA

    naomba kufahamishwa namna ya ufugaji wa samaki kisasa nina eneo amabalo ni heka kumi na naomba nipatiwe maelekezo ya kutosha

    EMAIL YANGU NI tonnytz@yahoo.com

    Tunawashukuru sana wasikilizaji wetu wote kwa naoni yenu mbalimbali kuhusu redio yetu, tukimjibu lenusi kingalu ni kwamba huu ni mwaka mpya wa jadi kwa kalenda ya Tibet hivyo hauhusiani na tarehe mosi Januari inayosherehekewa na ulimwengu mzima.

    Niliyoona kwenye Shule ya msingi ya No. 1 ya Lhasa

    Wasikilizaji wapendwa, huu ni mwaka wa 50 tangu mageuzi ya kidemokrasia yafanyike mkoani Tibet. Katika miaka hiyo 50, mambo ya elimu ya mkoa huo yamepata maendeleo makubwa; katika Tibet ya zamani iliyotawaliwa kwa mfumo wa kimwinyi wa wakulima watumwa, watoto wa makabaila na mabwanyenye tu walikuwa na haki ya kupata elimu; hivi sasa watoto wa makabila mbalimbali wanaweza kusoma pamoja na kupata elimu kwa usawa.Sasa tufuate kutembelea kwenye shule ya msingi ya No. 1 ya Lhasa.

    Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1952 ni shule ya kwanza ya msingi ya kiserikali mkoani Tibet baada ya China mpya kuanzishwa. Hivi sasa shule hiyo ina wanafunzi zaidi ya 1800, wengi wao ni watibeti, theluthi moja ni wahan, pia wako wachache kutoka makabila mengine.

    Hivi karibuni shule hiyo ilianza muhula mpya wa masomo. Mwandishi wetu wa habari alipoingia kwenye shule hiyo aliona wanafunzi wakicheza kwa furaha kwenye kiwanja cha michezo.Baada ya muda mfupi, kengele ya darasa ililia na watoto wakaingia darasani.

    Siku za mchipuko ni majira yenye matumaini. Hasa kwa wanafunzi wa darasa la sita watakaohitimu masomo kwenye shule ya msingi, mtihani wa kuingia shule ya sekondari ni changamoto, na pia ni fursa. Mwanafunzi mtibet Danzengpingcuo anasoma katika darasa la sita la shule hiyo. Alisema:

    "sasa nakaribia kuhitimu masomo na nitafanya mtihani wa kuingia shule ya sekondari, nataka kudurusu kwa makini masomo yote niliyojifunza kwa ajili ya mtihani huo. Nina matumaini kuwa naweza kuingia shule nzuri ya sehemu za ndani za China."

    Imefahamika kuwa ili kuunga mkono mambo ya elimu ya Tibet, mikoa na miji ya ndani ya China yenye hali nzuri ya elimu yote imeanzisha madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa Tibet na kuweka sera zenye unafuu kwa wanafunzi hao. Danzengpingcuo alieleza matumaini kuwa ataweza kuingia darasa la wanafunzi wa Tibet mjini Shanghai, kwa kuwa shanghai ni moja ya miji iliyoendelea zaidi nchini China, kwa hiyo kiwango cha elimu cha darasa la wanafunzi wa Tibet pia kiko juu kabisa kote nchini China. Danzengpingcuo alisema kuwa ana imani ya kufanya vizuri mtihani huo.

    Shule ya msingi ya No. 1 ya Lhasa si kama tu inatilia maanani masomo ya kwenye vitabu, bali pia inazingatia kuongeza uwezo wa jumla wa wanafunzi. mwalimu anayeshughulikia mambo ya ufundishaji Bw. Wu Shucong alisema, wakati wanafunzi walipoandikishwa katika shule hiyo, mambo wanayopenda yaliorodheshwa, halafu wakagawanyika katika madarasa yenye somo maalumu kutokana na upendeleo wao. Mwalimu Wu alisema:

    "kila darasa lina somo maalumu, ikiwemo ala na muziki wa jadi, somo la muziki wa jadi la shule yetu linajulikana sana."

    Katika darasa la kwanza No. 5 analoongoza mwalimu Lu Linhua, Mwalimu Lu alisema:

    "wakati wa kutilia maanani masomo ya kwenye vitabu, pia tunazingatia kuendeleza uwezo wao maalumu. Kwa mfano katika darasa letu wavulana wanafundishwa kupiga zumari, na wasichana wanafundishwa kupiga kinanda cha kichina Guzheng, wanafunzi wana hamu kubwa. Mbali na hayo, kila mwanafunzi pia anaweza kuchagua somo jingine kwa hiari kama vile kucheza dansi na kuchora."

    Mwalimu Wu Shuchong alisema, mbali na hayo kazi nyingine muhimu ya mwaka huu ni kuimarisha zaidi elimu kuhusu mambo ya usalama. Mwalimu Wu alisema, tarehe 14 Machi mwaka jana, wahalifu wachache walizusha vurugu ya kimabavu mjini Lhasa na kusababisha hasara kubwa za mali na maisha ya wakazi wa huko, utaratibu wa jamii uliharibiwa vibaya. Wakati huo ingawa kutokana na juhudi za walimu, hakukuwa na mwanafunzi aliyejeruhwa katika ghasia hizo, lakini shule hiyo pia ilikumbwa na hasara za mali. Mwalimu Wu Shuchong alisema katika muhula huo mpya, shule hiyo itaimarisha elimu ya usalama kwa wanafunzi ili kukabiliana na matukio ya dharura.

    Hivi sasa mji wa Lhasa umerejea kwenye hali ya utulivu. Mwalimu Lu Linhua alisema, katika muhula wa majira ya mchipuko, wanafunzi na walimu wote wana ari kubwa na matumaini mapya. Mwalimu Lu alisema:

    "baada ya mapumziko ya likizo ya siku za baridi, walimu wamekuwa na sura mpya, wazazi wa wanafunzi pia wana uchangamfu mkubwa, kila mwanafunzi na mwalimu wote wana mwanzo mpya, na wanatumai kufanya vizuri zaidi kuliko mwaka uliopita."

    Mwishoni wasichana wawili wa shule hiyo Danzengyuzhen na Gangbai waliimba wimbo mpya waliojifunza unaoitwa 'Msichana wa mti wa willow'.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako