• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • London-Marais wa China na Marekani wakutana

    (GMT+08:00) 2009-04-02 09:46:48

    Rais Hu Jintao wa China tarehe 1 Aprili amekutana na rais Barack Obama wa Marekani. Hii ni mara ya kwanza kwa marais wa China na Marekani kukutana baada ya rais Obama aingie madarakani mwezi Januari mwaka huu.

    Katika mazungumzo kati yao, rais Hu Jintao amesema, tangu rais Obama aingie madarakani, uhusiano kati ya China na Marekani ulionekana na mwanzo mzuri na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili pia walitembeleana siku chache zilizopita. Vile vile China na Marekani zilifikia mwafaka katika kutathmini uhusiano kati yao na kuanzisha mazungumzo ya mkakati na uchumi kati ya nchi hizo mbili.

    Rais Hu Jintao amesisitiza kuwa, uhusiano mzuri kati ya China na Marekani si kama tu unalingana na maslahi ya kimsingi ya nchi hizo mbili na wananchi wao, bali pia unasaidia amani, utulivu na ustawi wa kanda ya Asia na Pasifiki na dunia nzima.

    Rais Obama amesisitiza umuhimu wa uhusiano kati ya Marekani na China, na kueleza imani yake kuwa, hakika uhusiano huo utakuwa imara zaidi katika siku za usoni.

    Katika mazungumzo hayo, marais hao pia walibadilishana maoni kuhusu masuala ya kikanda na ya kimataifa yanayofuatiliwa na pande hizo mbili,  uhusiano kati ya China na Marekani, na  namna ya kukabiliana na msukosuko wa fedha duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako