• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua za wasikilizaji 0407

    (GMT+08:00) 2009-04-07 15:07:47

    Leo tunawaletea barua tulizotumiwa kutoka kwa wasikilizaji wetu na maelezo kuhusu China yakamilisha siku hadi siku mfumo wa kinga na udhibiti wa maambukizi ya mafua ya homa ya ndege kati ya binadamu na ndege.

    Sasa tunawaletea barua tulizotumiwa kutoka kwa wasikilizaji wetu. Msikilizaji wetu Geoffrey Wandera,wa sanduku la barua 57333,Nairobi Kenya ametuletea barua akianza kwa kusema kuwa, kwa kweli nakipenda sana kipindi cha mazungumzo kati ya bwana Fadhili,Jane na mama Chen,yaliyopeperushwa hewani na kusikika kwenye 91.9 fm hapa mjini Nairobi saa sita adhuhuri, huwa yananifurahisha sana na kunichangamsha sana.

    Jukumu langu ni kuendeleza uhusiano na urafiki bora kwa kuendelea kusikiliza na kufuatilia matangazo ya CRI kila mara.Kipindi cha leo, ambacho pia huwa kinazungumzia suala la utamaduni wa sanaa mbalimbali za kichina, ambapo mazungumzo hayo yalitaja aina 3 za sanaa. Sanaa ya kwanza ambayo ni sanaa ya picha za kukatwa ,imekuwa na maelezo yake ambayo yamezungumziwa kwa kina sana. Sanaa ya pili ambayo pia imezungumzia kwa ufasaha ni ile sanaa ya kuweka urembo kwenye nguo kwa kutumia utaa ambao unafahamika kama chemichemi ya milimani. Sanaa hii ya kuweka urembo kwenye nguo ni mojawapo ya sehemu za utamaduni wa watu wa eneo fulani lililoko kasikazini mwa China. Sanaa nyingine ambayo ni ya tatu na imeshamiri na kuwa kivutio zaidi nchini china ni ile sanaa ya uchoraji wa picha za paka kwenye tunguri.Haya ni maajabu na vitendo vya kusifu sana jamii ya wachina. Jambo ambalo limenishangaza ni kuwa ujuzi na akili nyingi ambazo mchina anatumia kutafakari zaidi hali ya kujishighulisha na mambo kama haya yanayoingizia taifa kipato.

    Ningali natafakari mambo mengi kuhusu utamaduni wa wachina kwa maana ukilizungumzia suala la sanaa kwa kweli linamuhusu kila mchina kwa ujumla.Pia ukizungumzia swala la sarakasi lazima mchina atajwe kwani jamii ya wachina ni ya watu amabo wanapenda sana kujishughulisha na mambo kama hayo.

    Kwa hiyo mama Chen iwapo nitafanikiwa kufika china usikose kunionesha picha za kukatwa na picha za paka kwenye tunguri pamoja na nguo zenye urembo.

    Bwana Geoffrey Wandera Namachi anasema katika barua yake nyingine kuwa, kwa kufuatiliya zaidi na kwa ukaribu kuhusu China kunatokanan na kuwepo kwa ushirikiano mzuri wa karibu kati yangu na CRI pamoja na marafiki zangu wa kichina waliopo hapa Kenya. Ingawa CRI imenielimisha mambo mengi , lakini pia rafiki nilionao hapa Nairobi wamechangia kwa kiasi kikubwa sana kunielimisha kuhusu China hasa mkoa huu ujulikanao kama Guangzhou. Walinifahamisha kuwa mkoa huo ni mahali ambapo biashara nyingi hufanyika. Mmoja wao alinifahamisha kuwa mkoa wa Guangzhou ni mojawapo ya mkoa mkubwa sana ulio na umaarufu nchini China.

    Aliongeza kuwa Guangzhou ni mkoa unaojiendesha wenyewe kibiashara siku hadi siku. Kwa kweli walinipasha vidokezo muhimu kuwa mji huo ni mlango wa baharini unaoingia na kutokea sehemu nyingi za nchi ya China.Wamenieleza kuwa kuna viwanda vingi vinapatikana mkoani humo ambapo kuna biashara za kila aina.Waliweza kunipa mfano wa kiwanda cha BHACHU ambacho kinatengeneza vyuma na vilevile kuna kiwanda cha kutengeneza betri.

    Mmoja wa rafiki zangu hao alinieleza kuwa wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya china hufurika kwa wingi mkoani Guangzhou kufanya urafiki na ushirikiano wa kibiashara na wenyeji wao.Walisema kuwa mkoa huo ni mahali ambapo ndege hutua mara kwa mara zinazoleta watalii pamoja na wafanya biashara kutoka pande zote za dunia

    Baada ya mimi kuwaeleza kuwa nina ushirikiano mzuri na CRI waliniahidi kuwa iwapo nitakapofanikiwa kufika china nimueleze mama Chen asikose kunipeleka matembezi mkoani Guanzhou.

    Tunakushukuru sana Geoffrey Wandera kwa barua zako yenye sifa kemkem kuhusu sanaa za China pamoja na mji wa Guanzhou, kweli sanaa ni kitu muhimu sana maishani mwa watu na jamii ya China inapenda sana sanaa kwani hiki ni kipaji ambacho sio kama kila mtu anaweza kuwanacho, hivyo ukifanikiwa kufika China tutakupeleka ili ujionee mwenyewe sanaa za China.

    Richard Wekesa Wekoyi wa sanduku la posta 1031 Bungoma Kenya ametuletea barua pepe anasema angependa salamu zake ziwafikie wafuatao:

    1.Catherine Nelly macheso wa Bwake, Bungoma

    2.Joseph Mukaburu wa Bwake, Bungoma.

    3.Xavier Telly Wambwa wa Bungoma

    4.Stephen magoyeKumalija wa Shinyanga Tanzania.

    5.Yaagub Saidi Indambira wa Kakamega, Kenya

    6.Ali Hamisi Kimani wa Kadongo, Kenya

    7.Dominic Nduku Muholowa Kakamega, Kenya.

    8.Okongo Okeya wa Iganga, Uganda

    9.John Samvura wa Ruhengeri, Rwanda.

    Ujumbe wake unasema: Tuendelee kusikiliza Radio China Kimataifa.

    Msikilizaji wetu Mbarouk Msabaha wa Al Ghassani Dubai Emirates ametuletea barua pepe akiomba salamu zake za kheri na baraka ziwafikie wafuatao:

    1. Bi. Nuru Ahmed Al Farsi na Bi. Mariyam Ahmed Al Farsi Pamoja na watoto wao wote wakiwa Mkunazini Zanzibar Tanzania.

    2. Bw. Salim Msabah Al Ghassani akiwa Kigoma Tanzania

    3.Bw. Issa Msabah Al Ghassani na familia yake wakiwa Mkunazini ZanzibarTanzania.

    4."Brown Girl" Rukiya H.Mohammed wa Riyadh Saudi Arabia

    5.Mzee Gulam Hajji Karim na familia yake wakiwa Lindi Mtwara Tanzania

    Mwisho kwa ndugu, jamaa na marafiki wote waliopo Zanzibar,Oman na hapo Emirates. Ujumbe wake unasema, nyote nakutakieni kila la kheri na mafanikio katika maisha yenu.

    John Nganga, anuani yake ni johnmiracho@yahoo.com ametuletea barua akisema, kwanza ni salamu nyingi kutoka hapa Nakuru Kenya. Mimi husikiliza vipindi vya Radio China kimataifa kupitia kwenye idhaa ya kiswahili ya KBC Nairobi. Mimi hupendelea sana kusikiliza vipindi mbalimbali vya Radio China Kimataifa kwani vinatupa mwangaza kuhusu jamhuri ya watu ya China kwa mapana na marefu kuhusu vivutio mbali mbali vya kale vinavyo pendeza.

    Sauti nyororo za watangazaji wa Radio China Kimataifa hutufanya tuendelee kuisikiliza na kuipenda idhaa hiyo zaidi na zaidi. Muendelee na moyo huo huo na bila shaka mtayaona matunda ya kazi yenu njema. Mwisho naitakia Radio China Kimataifa kila la heri kwenye matangazo yake ya kila siku.

    Pili nilishiriki kwenye chemsha bongo je mliipokea na nilikuwa nambari ngapi.

    Tatu ningeomba mnitumie jarida la 'CHINA TODAY' ili niweze kufahamu mengi kuhusu China na picha maridadi. Nne ningeomba Radio China inialike huko Beijing na idhamini safari yangu kwani mimi sina uwezo wa kifedha wa kugharamia na nitashukuru. Na tano ningeomba mnitumie majibu ya barua hii kupitia kwa anuani yangu ya barua pepe na mnipigie simu. Asanteni.

    Tunakushukuru sana msikilizaji wetu ingawa hukutuandikia jina lakini barua yako tumeipata na tunakujibu kupitia kipindi hiki cha sanduku la barua, kuhusu chemsha bongo kama ulikuwa unafuatilia matangazo yetu hasa kipindi cha chemsha bongo ambacho kimemalizika kwa muda sasa, basi ungepata majibu yote kama ulishinda na umepata nafasi ya ngapi. Suala la kupata udhamini wa safari tunakuambia kuwa usichoke kusikiliza CRI kwani kuna vipindi kama chemshabongo ambapo ukifanikiwa kujibu vizuri masuali basi utapata fursa ya kutembelea China.

    Na Wasikilizaji wetu Mogire O Machuki na Rose Moraa Mogire wa Bogeka Village sanduku la posta 646 Kisii Kenya ametuletea barua akiomba salamu zao za ushirikiano kutoka Kisii Kenya ziwaendeea Joseph Miroro na Rebecca Kwamboka, Nicholas Mokaya Magasi, Willam Mekenye Nyambono na Jane Kerubo, Philip Machuki, Kefa O Gichana na familia yake wote walioko Kisii Kenya.

    Mbarouk Alli Ghassan, Rukia H. Mohammed na B enedicto Gisemba wakiwa United Arab Emiratesl; Ras Franz Manko Ngogo, Kaziro Dutwa, Kilulu Kulwa, Liz Richie, Onesmo H.Mponda, Hussein Mirachi, Paroko wa Paroko, Mchana J Mchana, Geoffrey P.Njereka, Emmanuel S.Kapela na Mtoto Happyness Julius wote walioko Tanzania, ujumbe wake unasema, CRI ndio kituo muhimu cha kujuliana hali.

    China yaendelea kukamilisha mfumo wa kuzuia na kudhibiti maambukizi ya homa ya mafua ya ndege

    Mwezi Januari mwaka 2009 China ilitoa ripoti ikithibitisha wagonjwa wanane walioambukizwa homa ya mafua ya ndege. Mpaka sasa watu zaidi ya mia mbili kote duniani wamekufa kutokana na ugonjwa huo. Kwenye mikutano miwili ya mwaka iliyofanyika mwezi Machi hapa Beijing, homa ya mafua ya ndege kwa binadamu pia ni suala lililofuatiliwa na wajumbe wengi waliohudhuria mikutano hiyo. Mjumbe kutoka taasisi ya kinga na udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza ya China Bw. Wang Yu alisema, hivi sasa China imeanzisha utaratibu wa kuzuia na kudhibiti maambukizi ya homa ya mafua ya ndege, na inafuatilia kwa karibu hali ya maambukizi ya ugonjwa huo. katika hali ya kawaida uwezekano wa binadamu kuambikizwa ugonjwa huo ni mdogo.

    Katika duka moja la supermarket mjini Beijing, mwandishi wetu wa habari alimkuta mama Su aliyekuwa ananunua nyama ya ndege katika duka hilo. Alipozungumzia homa ya mafua ya ndege alisema, zamani pia alikuwa na wasiwasi na hakuthubutu kula nyama ya kuku na bata. Sasa amefahamu zaidi kuhusu ugonjwa huo na kujua kwamba nyama ya ndege iliyoshughulikiwa katika hali ya joto kubwa haiwezi kubeba virusi vya ugonjwa huo. Mama Su alisema:

    Sauti 1

    "sasa nakula nyama ya kuku mara kwa mara, sina wasiwasi hata kidogo, kwa kuwa niliona mara kwa mara wasimamizi wakiifanyia upimaji nyama hiyo. Sasa nadhani nchi yetu inaweka mkazo katika kazi za upimaji. Kama ugonjwa huo ukigunduliwa, habari zitatolewa moja kwa moja na hatua mbalimbali zitachukuliwa kwa wakati."

    Mlipuko wa ugonjwa wa SARS uliotokea mwaka 2003 nchini China ulileta hofu kubwa kwa China na hata dunia nzima. Kutokana na sababu hiyo wakati kifo cha kwanza cha mgonjwa wa homa ya mafua ya ndege kilipotangazwa, watu waliingiwa tena na wasiwasi kwamba ugonjwa wa SARS umerudi tena? Wakati huo watu hawakuthubutu kula nyama ya kuku na bata, waliogopa kuona ndege kwa hofu kwamba wataambukizwa ghafla ugonjwa huo. Hivi karibuni mjumbe wa Baraza la mashauriano ya siasa la China ambaye ni naibu kiongozi wa kikundi cha kinga na udhibiti wa ugonjwa wa SARS katika wizara ya afya ya China Bi. Sun Tieying alitoa makala iitwayo 'hofu ya homa ya mafua ya ndege'. Alipozungumzia nia ya kuandika mahala hiyo Bi. Sun Tieying alisema:

    Sauti 2

    "nia ya makala hiyo ni kufuatilia kwamba kama homa ya mafua ya ndege italipuka au la, kama italeta hofu na wasiwasi kama ulivyokuwa mlipuko wa ugonjwa wa SARS mwaka 2003."

    Bi. Sun Tieying alianza kufuatilia hali ya maambukizi ya homa ya mafua ya ndege mwaka 2003, pia amejitahidi kufanya utafiti kuhusu ugonjwa huo. Bi. Sun Tieying alisema:

    Sauti 3

    "Binadamu akiambukizwa homa ya mafua ya ndege, wengi watakufa. Sababu ya kwanza ni kuwa hatufahamu kuhusu dalili za ugonjwa huo na zinachelewa kujitokeza; ya pili ni kuwa ugonjwa huo unalipuka ghafla, na unabadilika kuwa nimonia kwa muda mfupi, halafu unasababisha mfumo wa kupumua kutofanya kazi."

    Homa ya mafua ya ndege ni ugonjwa mkali namna hii, kwa nini mpaka sasa bado haujalipuka nchini China? Kwa mujibu wa mkurugenzi wa taasisi ya kinga na udhibiti wa magonjwa ya China Bw. Wang Yu alisema, hali hiyo inatokana na umaalumu wa virusi vya ugonjwa huo na hatua zilizochukuliwa na serikali ya China kuzuia na kudhibiti ugonjwa huo.

    Bw. Wang Yu alifahamisha kuwa, binadamu kuambukizwa homa ya mafua ya ndege kunatokana na kugusana na ndege walioambukizwa ugonjwa huo. Mpaka sasa ugonjwa huo bado hauwezi kuambukiza kati ya binadamu. Hata kwa ndege walioambukizwa ugonjwa huo kama nyama yake ikichemshwa, virusi vitauawa na havitadhuru afya ya binadamu. Kwa hivyo uwezekano kwa watu wa kawaida kuambukizwa ugonjwa huo ni mdogo.

    Ingawa homa ya mafua ya ndege haijalipuka nchini China, lakini kutokana na kuwa asilimia kubwa ya wagonjwa wa ugonjwa huo wanakufa, hatari yake haiwezi kupuuzwa. Baada ya ugonjwa wa SARS kulipuka nchini China mwaka 2003, wajumbe wengi wa bunge la umma la China waliwasilisha mada na miswada kuhusu kuanzisha mfumo wa kinga na udhibiti wa magonjwa, na zimetiliwa maanani na idara husika za serikali ya China. Kuanzia mwaka 2004, China ilianzisha mtandao wa usimamizi na kufuatilia hali ya maambukizi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo homa ya mafua ya ndege.

    Kuhusu homa ya mafua ya ndege kwa binadamu, mbali na kazi za usimamizi, kazi za kuuzuia kabla haujalipuka ni muhimu zaidi. Aidha China pia imeongeza nguvu katika utafiti wa chanjo ya ugonjwa huo. Bw. Wang Yu alisema:

    Sauti 7

    "taasisi ya udhibiti wa magonjwa ya China imetoa chanjo ya kizazi cha kwanza cha homa ya mafua ya ndege kwa binadamu, hivi sasa majaribio yote ya kliniki ya chanjo hiyo yamemalizika, na tumeanza kutengeneza chanjo hiyo na kuweka akiba. Pia tumeimarisha utafiti wa virusi vinavyoendelea kubadilika. Utafiti wa kurekebisha jini ya aina ya virusi vya ugonjwa huo vilivyopatikana China bara pia utaingia kwenye kipindi cha majaribio ya kliniki. Baada ya kazi hiyo kumalizika, China itakuwa nchi pekee duniani iliyoweza kumaliza kazi za kutenganisha virusi vya ugonjwa huo, kupima na kurekebisha jini yake na kufanya utafiti wa chanjo na kuweka akiba ya chanjo ya ugonjwa huo. Huu ni mfumo unaotarajiwa kuanzishwa kote duniani."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako