• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • "Waandishi chipukizi" mkoani Shaanxi China

    (GMT+08:00) 2009-04-08 21:07:27
    Mkoa wa Shaanxi ni sehemu yenye rutuba nyingi za utamaduni magharibi mwa China. Tokea katikati ya karne iliyopita waandishi wa vitabu waliozaliwa na kukulia katika sehemu hiyo wanakua kwa nguvu kutokana na mazingira ya utamaduni wa huko na wameandika riwaya nyingi zinazoeleza mabadiliko ya historia huko waliko. Waandishi hao wa vitabu ni hodari ambao kwa kalamu na jasho lao wameandika vitabu vingi vizito ambavyo vinastahili kukumbukwa katika historia. Katika miongo kadhaa iliyopita, waandishi hao ambao pia wanaitwa "waandishi chipukizi" wamekuwa nguvu muhimu katika nyanja ya uandishi wa vitabu.

    Hivi karibuni "tuzo ya fasihi ya Mao Dun" ambayo ni tuzo ya heshima kubwa kwa waandishi wa vitabu ilitolewa kwa riwaya ya "Mabadiliko Makubwa Mkoani Shaanxi". Mwandishi wa riwaya hiyo ni mmoja kati ya "waandishi chipukizi" mkoani Shaanxi anayeitwa Jia Pingao. Kwenye sherehe ya kutoa tuzo hiyo mjumbe wa waamuzi alisema,

    "Riwaya ya 'Mabadiliko Makubwa Mkoani Shaansi' kwa melezo ya kina na ya makini imeeleza matatizo na mfadhaiko wa wakulima wa vijijini katika miaka yenye mabadiliko makubwa nchini China."

    "Mabadiliko Makubwa Mkoani Shaanxi" ni riwaya ya 12 aliyoandika Bw. Jia Pingao, ambayo imeeleza jinsi hali ya vijijini ilivyobadilika kutokana na maendeleo ya kasi ya uchumi nchini China. Katika sherehe hiyo mwandishi Jia Pingao alisema hakutarajia hata kidogo kupewa tuzo hiyo. Alisema,

    "Riwaya ya 'Mabadiliko Makubwa Mkoani Shaanxi' ni kitabu nilichotaka zaidi kukiandika na nimekiandika kwa muda mrefu. Nilipoanza kuandika kitabu hicho sikuwa na uhakika kwamba nini hatima yake, lakini niliwahi kuapa mbele ya kaburi la baba yangu kwamba nitakamilisha riwaya hiyo kama ni jiwe la kukumbuka hali ya zamani ya maskani yangu."

    "Tuzo ya fasihi ya Mao Dun" ilianzishwa mwanzoni mwa miaka ya 80 ya karne iliyopita, Hayati Mao Dun alikuwa mwandishi maarufu wa vitabu nchini China, hadi leo tuzo hiyo imewahi kutolewa mara saba. Kabla ya Jia Pingao waandishi wengine wawili wa mkoani Shaanxi pia walipewa tuzo hiyo, nao ni Lu Yao na Chen Zhongshi.

    Si ajabu kuibuka kwa waandishi wa vitabu hodari mkoani Shaanxi. Mapema katika miaka ya 50 ya karne iliyopita kitabu cha "Historia ya Uvumbuzi wa Shughuli" kilichoandikwa na Liu Qing kuhusu mabadiliko makubwa vijijini China kilisifiwa kuwa ni kitabu kizito katika fasihi ya China. Mhakiki Bw. He Xilai alisema, waandishi wa vitabu walioathiriwa zaidi na kitabu hicho cha Liu Qing ni Lu Yao, Chen Zhongshi na Jia Pingao. Alisema,

    "Waandishi hawa watatu waliopewa tuzo ya fasihi ya Mao Dun wote walipata taathira kutoka kitabu cha 'Historia ya Uvumbuzi wa Shughuli", kitabu hicho kina ushawishi mkubwa mkoani Shaanxi katika maandishi ya kueleza hali ilivyo na mtindo wa lugha."

    Baada ya mwandishi Liu Qing, Bw. Lu Yao amekuwa kama mtangulizi wa waandishi wa vitabu mkoani Shaanxi. Mwanzoni mwa miaka ya 80 ya karne iliyopita Bw. Lu Yao aliandika kitabu cha riwaya ya "Maisha", baadaye hadithi ya kitabu hicho ilitumika kwa kupigwa filamu ambayo iliwavutia watazamaji wengi.

    Riwaya ya "Maisha" inaeleza kijana mmoja wa vijijini mkoani Shaanxi asiyekubali hali ya umaskini na kutulia katika kijiji chake kilichotengwa jinsi alivyojitahidi kujipatia maisha ya aina mpya katika miaka ya mageuzi nchini China. Riwaya hiyo imeonesha watu waliotaka kufuta umaskini walivyokuwa na wasiwasi bila uhakika katika mapambano dhidi ya hali yao mbaya. Mhakiki Bw. He Xilai alisema,

    "Sababu ya riwaya hiyo kuvutia sana ni uelewa wa kina wa mwandishi kuhusu matatizo ya mabadiliko ya hadhi kutoka wakulima na kuwa wakazi wa mijini."

    Bw. Lu Yao hakuandika vitabu vingi, lakini kila kitabu chake kilisifiwa sana na watu. Kitabu chake kingine cha riwaya ya "Dunia ya watu wa Kawaida" pia kimeonesha mabadiliko makubwa ya kimaisha na ya kifikra ya watu vijijini na mijini katika miaka ya mageuzi ya kiuchumi mkoani Shaanxi. Kitabu hicho kimegusa hisia za wasomaji wengi na kimepata tuzo ya fasihi ya Mao Dun. Baada ya kitabu hicho, kitabu kingine kilichopewa tuzo ya Mao Dun ni kitabu cha "Mbuga za Paa Weupe" kilichoandikwa na Chen Zhongshi kwa miaka mingi. Kitabu hicho pia kinaeleza taifa la China lilivyopambana na hali ya umaskini kwa kupitia kueleza mabadiliko ya ukoo wake. Kitabu hicho kimehaririwa kuwa hadithi ya filamu na opera.

    Wachina husema "mahali tofauti huwa na utamaduni tofauti", hali kadhalika waandishi wa vitabu. Kwa kupata rutuba ya utamaduni mkoani Shaanxi waandishi wengi wa vitabu wamekua kwa nguvu, ikilinganishwa na waandishi wengine, waandishi wa vitabu vya sehemu hiyo wanathubutu kukabiliana uso kwa uso na masuala yaliyokuwepo, na wana msingi imara wa kimaisha na walibeba majukumu ya kihistoria. Mhakiki He Xilai alisema,

    "Kwa kifupi, uzoefu wa waandishi hao wa vitabu mkoani Shaanxi ni kuandika hali ilivyo ya jamii, mambo waliyoandika ama ya zamani au ya sasa yote yanakuwa sambamba na nyayo za historia."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako