• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Qingming, siku ya jadi kwa Wachina kukaribisha majira ya mchipuko na kuwakumbuka marehemu

    (GMT+08:00) 2009-04-08 21:08:29

    Siku ya Qingming ni siku ya jadi kwa Wachina kukaribisha majira ya mchipuko na kuwafanyia tambiko marehemu, siku hiyo huwa kati ya tarehe 4,5, na 6 Aprili, mwaka huu siku hiyo ni tarehe 4. Kwa sababu siku hiyo iko katika kipindi cha majani kuchipuka na maua kuchanua, na watu hufanya mandari.

    Katika kalenda ya kilimo ya China, Qingming ni siku ya kuanza kwa kipindi kimoja kati ya vipindi 24 vya mabadiliko ya hali ya hewa katika mwaka mzima, maana yake ni "kipindi kiangavu". Kutokana na utamaduni wa jadi, siku hiyo pia ni siku ya kusafisha makaburi kwa Wachina na mila hiyo imekuwa na historia ya miaka 2500 hivi.

    Katika siku hiyo watu wa kabila la Wahan na watu wa makabila fulani madogo madogo huwa wanakwenda kwenye makaburi ya jamaa zao waliofariki dunia kuwafanyia tambiko kwa kumwaga pombe, kufukiza udi, kuweka matunda na keki, na kupiga magoti, kisha wakaongeza udongo kwenye makaburi. Kuanzia siku za Qingming China imeingia katika majira ya mvua toka sehemu ya kusini hadi kaskazini, mvua za rasharasha zinachangia huzuni ya watu kwa marehemu. Mshairi mkubwa Du Mu wa Enzi ya Tang ya China katika karne ya 9 kwenye mashairi yake alieleza mazingira ya siku hiyo akisema, "Siku ya Qingming mvua za rasharasha zinazonyesha huchangia zaidi huzuni waliyonayo waendao kusafisha makaburi ya jamaa zao waliokufa."


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako