• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua za wasikilizaji 0414

    (GMT+08:00) 2009-04-14 14:47:34

    Msikilizaji wetu Kilulu Kulwa wa sanduku la posta 161, Bariadi, Shinyanga, Tanzania ametuletea barua akisema kuwa, Marafiki wapendwa wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio China Kimataifa, salamu nyingi ziwafikie kutoka kwangu hapa nchini Tanzania. Ni furaha kubwa iliyoje ninapowaandika barua hii, niliwashukuru sana kwa zawadi nzuri mliyonitumia ikiwa pamoja na cheti maalum cha kuvutia, (certificate of honour) vikiwa ni tuzo mliyonipatia kutokana na mashindano ya chemsha bongo ya ujuzi wa vivutio vya mkoa wa Guangxi, nchini China ambayo yaliandaliwa na kufadhiliwa na Radio China Kimataifa. Vile vile ninawashukuru kutokana na kipindi na habari hii ya CRI. CRI ni mojawapo ya radio na stesheni kubwa kabisa humu duniani. Ni ukweli usiopingwa kuwa CRI inawashirikisha ipasavyo wasikilizaji wake popote walipo humu duniani.

    Radio China Kimataifa inatutangazia kwa uhakika na ufasaha matukio mengi yanayojiri nchini China na ulimwenguni kote. Vipindi maalum kama vile Daraja la Urafiki kati ya China na Afrika, Safari nchini China, Sanduku la Barua, Kuwa nasi jifunze Kichina, Kipindi cha Salaamu na Mashindano ya chemsha bongo ya ujuzi wa masuala ya China ambayo huandaliwa takribani kila mwaka na CRI na kuwashirikisha moja kwa moja wasikilizaji wake, imeleta mvuto na hamasa kubwa kwa wasikilizaji wa CRI, na ni kazi nzuri inayostahili kupongezwa na kisifiwa sana.

    Kwa sababu hii, CRI tutaiunga mkono sana, ikiwa imebeba majukumu muhimu kama daraja la kujenga urafiki na ushirikiano kati ya wananchi wa China na wa nchi na mataifa mengine kote duniani.

    Marafiki wapendwa, ninawashukuru pia kwa ajili ya jambo zuri mnalolifanya katika kipindi cha "Sanduku la Barua" ambapo huzisoma barua na barua pepe zinazotoka kwa wasikilizaji wenu, zikiwemo barua zangu ambazo mmekuwa mkizinukuu kila mara mpatapo nafasi, hii hututia moyo sana sisi wasikilizaji na inatuongezea ari na nguvu ya kuendeleza ushirikiano wetu ulio imara zaidi. Nami naahidi kuendelea kusikiliza na kuiandikia Radio China Kimataifa na pia kudumisha na kuendeleza urafiki na ushirikiano wetu bila vikwazo vyovyote. Asanteni.

    Bwana Kulwa anasema katika barua yake nyingine kuwa, wapenzi marafiki, wahariri na watangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio China Kimataifa, nafurahi sana kuwaandikia, kwani siku zilizopita niliahidi kuandika makala kuhusu mwaka wa ng′ombe. Kwa nini nimevutiwa na alama ya mnyama huyu wa kufugwa ambaye hufugwa na watu wengi duniani? Kwenye matangazo yetu ya Kipindi Maalum cha Maadhimisho ya mwaka mpya wa jadi wa China, pamoja na mambo mengine mengi mazuri, pia mlituelezea kwa kifupi kuhusu mwaka huu wa 2009 kuwa ni mwaka wa ng′ombe wa kichina.


    1 2 3 4 5
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako