• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima waliopoteza ajira mijini waanzisha shughuli zao

    (GMT+08:00) 2009-04-16 15:36:22

    Miongoni mwa wakulima wapatao elfu 50 waliopoteza ajira na kurudi kwao wilayani Kaixian, baadhi yao wanajitahidi kutafuta ajira na wengine wenye uzoefu na akiba wameanza kuanzisha shughuli zao zinazolingana na hali halisi ya kwao. Bw. Zhao Chaoxing ni mmoja kati yao.

    Anasema "Mwaka jana niliporudi, nilianza mara moja kufuga kuku, nilifuga kuku 200 na kuwauza wote kwa bei ya Yuan 60 kwa kuku mmoja. Baadaye nilianza kufuga sungura, ambao wanazaliana haraka zaidi, na kuna mahitaji sokoni, kwa hiyo ni shughuli zenye hatari ndogo ya kupata hasara."

    Baada ya kushindwa kwa biashara ya dawa za mitishamba, mwishoni mwa mwaka jana, Bw. Zhao Chaoxing mwenye umri wa miaka 39 alirudi kwenye maskani yake akiwa na akiba ya Yuan zaidi ya laki moja, na kuziwekeza kwenye shughuli za ufugaji.

    Katika ua wa nyumba yake, anafuga kuku na bata, hususan sungura anawachunga kwa ajili ya kuzaliana. Bw. Zhao aliweka lengo la kufuga vizimba 800 vya sungura, baadaye ataanza kufuga samaki na kutoa huduma za chakula na malazi kwa watalii wanaotembelea vijijini. Alisema bado anahitaji pesa nyingi zaidi za kuanzisha shughuli hizo, ana mpango wa kuomba mikopo maalumu ya riba nafuu inayotolewa na serikali kwa ajili ya wakulima waliopunguzwa kazi mijini wanaporudi vijijini na kuanzisha shughuli zao binafsi.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako