• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkusanyaji wa vitu vya sanaa vya Afrika Bw. Guo Dong

    (GMT+08:00) 2009-04-20 16:40:13

    Hapa Beijing siku hizi kituo cha sanaa kiitwacho Qiao kinafanya maonesho ya sanaa ya Afrika, vitu vinavyooneshwa katika maonesho hayo karibu vyote vinatolewa na Bw. Guo Dong aliyewahi kuishi nchini Uganda kwa miaka 18.

    Maonesho hayo yanaitwa "Sanaa ya asili na Maisha ya Leo", yanaonesha vitu adimu zaidi ya 500 vya Afrika vikiwemo vyombo vinavyotumika maishani, ala za muziki na vitu vya ibada vilivyotumiwa na jamaa wa watemi na raia wa kawaida. Bw. Guo Dong ni mwandalizi wa maonesho hayo. Alisema,

      "Hii ni fursa nzuri kwa Wachina kuifahamu Afrika, watazamaji wanapojionea kwa karibu vitu hivyo huguswa hisia kwa nguvu."

      Bw. Guo Dong mwenye umri wa miaka 45 ni mzaliwa wa Beijing, anapenda sanaa toka alipokuwa mtoto na aliwahi kufundishwa kuchora picha na mwalimu wake aliyekuwa maarufu nchini China, na baadhi ya picha alizochora zilinunuliwa na kuhifadhiwa katika taasisi ya sanaa.

    Katika miaka ya 80 ya karne iliyopita, China ilianza kufungua mlango na kufanya mageuzi ya kiuchumi, watu wengi wa nchi za nje walikuja China kusoma au kufanya kazi, katika miaka hiyo Bw. Guo Dong alifahamiana na wanafunzi kadhaa wa nchi za nje wakiwemo wanafunzi wa Uganda. Bw. Guo Dong alikuwa na uhusiano mzuri na wanafunzi wa Afrika na mara kwa mara alifahamishwa nao kuhusu hali ilivyo ya Afrika. Bw. Guo Dong alisema,

      "Marafiki wa Afrika wameniachia picha nzuri kichwani mwangu, waliniambia 'bara lao ni zuri sana'. Lakini wakati huo uelewa wangu ulikuwa kwamba Afrika ni bara lililoko nyuma kimaendeleo, hata hivyo nilishikwa na hamu ya kwenda huko nione kwa macho yangu Afrika ilivyo."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako