• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utamaduni wa chai nchini China

    (GMT+08:00) 2009-04-20 16:21:43

      

    Chai ni kitu kisichoweza kukosekana katika maisha ya Wachina, utamaduni wa chai umekuwa na historia ndefu nchini China. Kila ifikapo katikati ya mwezi Aprili wa majira ya Mchipuko, ndipo majani mapya ya chai yanapoanza kuuzwa sokoni, wakati huo watu huburudika na chai nzuri bila kuchelewa.

      China ni chimbuko ya miti ya chai, na pia ni nchi inayozalisha majani ya chai kwa wingi, ambapo wachina walianza kunywa chai mapema zaidi kuliko wengine duniani. Kitabu cha kwanza duniani kuhusu elimu ya chai kiliandikwa na Lu Yu wa Enzi ya Tang zaidi ya miaka elfu moja iliyopita. Kitabu hicho kimeeleza mambo mbalimbali kuhusu chai ikiwa ni pamoja na historia ya chai, ufundi wa kutengeneza majani ya chai na utamaduni wa kunywa chai. Kitabu hicho kimepeleka kitendo cha kunywa chai kwenye utamaduni na kimesukuma mbele maendeleo ya utamaduni huo nchini China, kutokana na kitabu hicho, mwandishi huyo Bw. Lu Yu alisifiwa na kuheshimiwa sana na watu.

    Nchini China chai inasifiwa kuwa ni "kinywaji cha kitaifa". Mambo ya kupiga kinanda, kucheza chesi, sanaa ya kuandika kwa brashi ya wino na kuchora picha, kutunga mashairi, kunywa pombe na kunywa chai, hayo ni mambo saba yasiyokosekana katika maisha ya wasomi, kwa hiyo chai imekuwa aina moja ya utamaduni wa jadi nchini China. Katika enzi mbalimbali za kifalme za zama za kale nchini China, mashairi kuhusu chai ni mengi na mchezo wa mashindano ya uzuri wa chai ulikuwa ni maingiliano ya kijamii yaliyopendwa na wasomi.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako